Huu ulibuniwa kuliwa kiangazi huko kwetu tunaopata mvua moja kwa mwaka. Tembele nalo hukaushwa inaitwa nsasa, uyoga nao hukaushwa.Mlenda wa kuchanganya majani ya maboga na bamia naujua vizuri, huu wa unga ndio siufahamu vizuri.
Majani pori yapo ya aina kama tatu, yanatambaa chini.Hayo malendi yanalimwa kama mboga au ni majani pori/mwitu?
ndio ni majani ya maboga a.k.a msusa na yakifanywa hivyo unavyosema huitwa nswalu, pia huweza kupikwa yakiwa mabichi ila ili uwe mlenda lazima uweke bamia!.
Niliukuta Mombo cku nikwa naenda kaskazini,uliwekwa maharage meupe sijui yanaitwaje lakini ni meupe nilikula samaki na huo mlenda duh ulikua mtamu sana,mjini yale maharage sijawahi yaonaHapana.Yanakuwa mlenda bila hata bamia.
Mlenda na bamia ni vitu viwili tofauti.
ni majani ya porini, huota sehemu isiyokuwa na vichaka, yanafanana na ufuta ila ni madogo, ni jamii moja ya mimea aina hiyoHayo malendi yanalimwa kama mboga au ni majani pori/mwitu?
Hayo maharage yanaitwa "ndongauchee"!Nikiukuta Mombo cku nikwa naenda kaskazini,uliweka maharage meupe sijui yanaitwaje lakini ni meupe nilikula samaki na huo mlenda duh ulikua mtamu sana,mjini yale maharage sijawahi yaona
ndio, pia unaweza kuchanganya hayo majani makavu ukachanganya na unga ukasaga au kutuanga, unaweza kuongeza karanga, mbengu za mafuta ukatuanga na kuchekechaKumbe hata huo wa unga huwa wanachanganya na majani ya maboga!
ndioYakikauka yanatengeneza mlenda bila bamia ila yakiwa mabichi ili yatengeneze mlenda inabidi kutumia na bamia?
πππππ Wewe ni mgogo kabisa eti irende,safwe,chipali,chiwandagulu,nyamhuzha,nyapembe.Wana singida na dodoma...
Wanaita irende au nswalu kwa wanyamwezi,
Majani yake ni kama majani ya mmea wa ufuta...
Yaaani kama unavyouona mmea wa ufuta na huo mlenda uko hivyo hivyo unafanana 90%
Cha kufanya kama ukiuona chuma majani yake uloweke kwenye maji...utaona yana toa mlenda mwingi na mzito ukiushika tofauti na majani ya mmea wa ufuta.
Hayo majani membamba ndo huanikwa yakikauka yana sagwa au kutwangwa na kutoa poda line tyr kwa matumizi ya mboga.
Ni tamaduni za ukanda wa kati wao wanategemea mvua ya msimu wa masika tu kwa hivuo mboga mbichi hupatikana kwa wingi kipindi cha mvua kwa hivyo ili kuhifadhi mboga kwa msimu wa kiangazi.
Walikuwa wana kausha mboga mbali mbali ikiwemo
huo mlenda,majani ya kunde(nyafwe/safwe)Chipali,Chiwandagulu,mitanda( nyama)nk
bila kusahau nyanya mshenzi na matango n.k pia nayo yalikuwa yanakaushwa juani na kuhifadhiwa.
Ukanda Juu kusini na mikoa ya Pwani hawajui mambo hayo kwa sabb wao wanapata misimu miwili ya mvua..
Kwaivyo mbogamboga na viungo fresh hawaishiwi kabisa.
Kumbuka si hivyo tu mpk viazi vitamu humenywa na kuanikwa kwaajili ya kuhifadhi kwa matumizi ya kiangazi.
Huitwa Michembe,yakichemshwa na kuanikwa yanaitwa matoolwa(matoborwa)
Ni matunda pekee sijawahi ona yaliyohifadhiwa kwa kuanikwa kama yapo watasema wakongwe.
Mlenda na maharage mixer au sijaelewa.Niliukuta Mombo cku nikwa naenda kaskazini,uliweka maharage meupe sijui yanaitwaje lakini ni meupe nilikula samaki na huo mlenda duh ulikua mtamu sana,mjini yale maharage sijawahi yaona
Hawa wachina watatuua....mlenda wa unga?Kuna ule mlenda huwa unapikwa kutokana na majani fulani yanayosagwa kama unga, unaitwa mlenda wa unga.
Haya majani yanayotengeneza huu mlenda wa unga yanapatikana wapi?
Yanauzwa sokoni kama mboga ?
Unaweza kuyapikia mlenda yakiwa mabichi(hayajakauka) kama mboga nyingine za majani?
Nyanya mshenzi ndo zile ndogo? Ila umeongea ukweli mtupu. Mihogo-makopa, pilipili, uyoga, nyanya na ngogwe zote hukaushwa.Wana singida na dodoma...
Wanaita irende au nswalu kwa wanyamwezi,
Majani yake ni kama majani ya mmea wa ufuta...
Yaaani kama unavyouona mmea wa ufuta na huo mlenda uko hivyo hivyo unafanana 90%
Cha kufanya kama ukiuona chuma majani yake uloweke kwenye maji...utaona yana toa mlenda mwingi na mzito ukiushika tofauti na majani ya mmea wa ufuta.
Hayo majani membamba ndo huanikwa yakikauka yana sagwa au kutwangwa na kutoa poda line tyr kwa matumizi ya mboga.
Ni tamaduni za ukanda wa kati wao wanategemea mvua ya msimu wa masika tu kwa hivuo mboga mbichi hupatikana kwa wingi kipindi cha mvua kwa hivyo ili kuhifadhi mboga kwa msimu wa kiangazi.
Walikuwa wana kausha mboga mbali mbali ikiwemo
huo mlenda,majani ya kunde(nyafwe/safwe)Chipali,Chiwandagulu,mitanda( nyama)nk
bila kusahau nyanya mshenzi na matango n.k pia nayo yalikuwa yanakaushwa juani na kuhifadhiwa.
Ukanda Juu kusini na mikoa ya Pwani hawajui mambo hayo kwa sabb wao wanapata misimu miwili ya mvua..
Kwaivyo mbogamboga na viungo fresh hawaishiwi kabisa.
Kumbuka si hivyo tu mpk viazi vitamu humenywa na kuanikwa kwaajili ya kuhifadhi kwa matumizi ya kiangazi.
Huitwa Michembe,yakichemshwa na kuanikwa yanaitwa matoolwa(matoborwa)
Ni matunda pekee sijawahi ona yaliyohifadhiwa kwa kuanikwa kama yapo watasema wakongwe.
Huo ni wa asili si mchina, na hawezi fanya biashara hii kwa sababu si popular.Hawa wachina watatuua....mlenda wa unga?
Maswali YOTE jibu NI Ndiyo.Kuna ule mlenda huwa unapikwa kutokana na majani fulani yanayosagwa kama unga, unaitwa mlenda wa unga.
Haya majani yanayotengeneza huu mlenda wa unga yanapatikana wapi?
Yanauzwa sokoni kama mboga ?
Unaweza kuyapikia mlenda yakiwa mabichi(hayajakauka) kama mboga nyingine za majani?