Mlenda wa unga unatokana na majani gani na yanapatikana wapi?

Nyanya mshenzi ndo zile ndogo? Ila umeongea ukweli mtupu. Mihogo-makopa, pilipili, uyoga, nyanya na ngogwe zote hukaushwa.
Yes ni vinyanya vidogoo sana.
Vilijulikana hivyo sehemu nyingi.
Kwa vyakula hivyo na namna ya uhifadhi watoto wa 2000 hawaelewi chochote.
Tumetoka mbali sana.
 
Huo wa Inga hutokana na mlenda WA asili AMBAO huitwa MBATA Unaoatikana Kwa wingi DODOMA kati.ni mzuri na mtamu pia unavirutubisho vingi kuliko wa bamian na maboga
 
Naam, yakiwa mabichi yanapikwa mlenda pia.

Huo mlenda wa kusagwa unaitwa 'nswalu'.

Unatokana na majani ya mmea unaoitwa mlenda, mmea huo unafanana na mmea wa ufuta pamoja na majani ya matango pori.

Ama kwa kutumia bamia pamoja na majani ya maboga.

Majani hayo huchumwa na kukaushwa kwa kuchanganywa pamoja ama kwa kutenganishwa na kuhifadhiwa.

Maandalizi yake ni kusaga pamoja huo mchanganyiko, tui la karanga kwa pembeni.
 
Inaonekana wengi hawaufahamu vizuri mlenda aliouulizia mleta mada, yale ni majani mwitu ya aina moja hayajachanganywa na majani mengine, na pia inawezekana kupikwa yakiwa mabichi, au yakiwa yamekaushwa na kusagwa kua unga, na yanapatikana zaidi mkoa wa dodoma.
 
Mkuu safi sana kwa kuweka hii, ndugu mleta mada aya majani ya huu mlenda wa unga yapo jike na dume kuna huu ambao mdau kauposti ni jike kuna majani mengine ambayo ni dume, aya unakausha kwa kutumia jua alafu unachanganya na majani ya maboga ambayo nayo ukaushwa pia aya maboga huitwa malumbu.
Baada ya hapo twanga vyote kwa pamoja alafu chekecha utaona mambo yalivyo na ugali wako wa DonaπŸ˜‹πŸ˜‹πŸ˜‹πŸ˜‹
Kingine aya majani ya mlenda msimu wa mvua ndio huwa yanachipua kwa wingi sana.
 
Mlenda wa huku ni tofauti, unaota porini pia ila unakua kama majani ya kawaida madogo madogo siyo mti. Unafanana na hiyo picha aliyoweka mdau.

Hatua za kupika sizijui, mwenye salio apige nimuulize mama unapikwaje, Akipika mama niπŸ˜‹, ila akipika bibi ni veryπŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯ sahani haioshwi, inalambwa...
 
Nswalu hiyo kisoda kimoja tu ,kinajaza sufuria nzima ,we ni kuongeza maji.Siupendi.
 
 

Attachments

  • FB_IMG_1704570536983.jpg
    143.8 KB · Views: 2
  • FB_IMG_1704570527134.jpg
    111.3 KB · Views: 3
Gentleman, nasikia ukila mlenda kisawasawa unakuwa na makalio laini na matamu kama Poshi Queen.

Hii imekaaje?
 
Kumbe umeathiriwa na mlenda ndio maana una...
 
Basi kila sehemu na taratibu zake.

Mlenda wa Singida, Tabora na Shinyanga, hutengenezwa kwa kutumia majani ya mmea wa mlenda pamoja na majani ya matango pori ama msusa(majani ya maboga).
Mchanganyiko huo ndiyo huzaa 'nswalu' yenye hadhi.

Usipochanganya jani la mlenda ama bamia mboga hiyo haitaweza kulendemka na kuwa kitu kingine.

Kina mama mko wapi msaidie ufafanuzi wa hii issue!

Nimekazana kutetea utadhani naingiaga hata jikoni kwenyewe!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…