Mlenda wa unga unatokana na majani gani na yanapatikana wapi?

ndio ni majani ya maboga a.k.a msusa na yakifanywa hivyo unavyosema huitwa nswalu, pia huweza kupikwa yakiwa mabichi ila ili uwe mlenda lazima uweke bamia!.
Kuna mlenda na kuna bamia ,mlenda OG hautokani na majani ya maboga
 
Asante mkuu,nimekuwa interested na matango,yanahifadhiwaje?
Hiyo michembe niliwahi kuila Mwanza
 
Asante mkuu,nimekuwa interested na matango,yanahifadhiwaje?
Hiyo michembe niliwahi kuila Mwanza
Matango hasa ya kienyeji,yalikuwa yanamenywa na kukatwa vipande vipande kama vya kachumbali ila size itategemeana na mkataji.
vipande hivyo viliwekwa juani takribani siku 14 au chini ya hapo,baada ya hapo vitasinyaa.
Tyr kuhifadhiwa store ya vyakula.
Wkt wowote mwaka mzima utakapohitaji kutumia vipande vilitumika kama vile mpishi anavyoongeza vipande vya karoti,au hoho kwenye mboga ndivyo vipande vya tango viliwekwa kwenye mboga (tofauti na mlenda mfano nyama n.k)Wkt ikiandaliwa jikoni.

Kwenye kukausha hakukuishia hapo tu member mmoja akasema pia mihogo-makopa, pilipili, uyoga, nyanya na ngogwe zote hukaushwa.
Binafsi nimejionea Nyanya pia,pilipili&uyoga n.k
Karibu
 
Ule unga unaitwa mwage, waluguru ndio mboga zao
 
Duh, mkuu na wewe ni wa kwetu nini?
 
Kumbe hata huo wa unga huwa wanachanganya na majani ya maboga!
Hayo majani yako yenyewe tu.watu naona wanachanganya na mlenda wa bamia na majani ya maboga.Hayo uliyouliza ni majani ya size ya kati unayakausha unasaga.Ukitaka kupika unachemsha maji kidogo unachotea huo unga unakoroga. ukitafuna mabichi au kuyaloweka yana ukakasi na yanatoa uji mzito rangi ya maji unaovutika.sijawai kuyala mabichi ila nayafahamu vizuri.Kijijin tulikua tunayachuma vichakani sio kuyanunua sokoni.
 
ndio ni majani ya maboga a.k.a msusa na yakifanywa hivyo unavyosema huitwa nswalu, pia huweza kupikwa yakiwa mabichi ila ili uwe mlenda lazima uweke bamia!.
hujamwelewa mkuu ,kuna mmea flani unakaushwa then unasagwa sasa ule unga unaweka kwenye chungu chenye maji ya uvuguvugu jikoni then unaupekecha na mwiko na kuwa mlenda though unaweza kuchanganywa na majani ya maboga ila kwa kukaushwa sio ukiwa mbichi,bahati mbaya sina picha ya huo mmea
 
kuna ule unatokana na majani pori yana miba ,yanakaushwa kwa jua baada ya hapo unatwangwa kwa kinu au kusagwa mashineni unakuwa unga wa kijani , kwa watu wamkoa wa Kilimanjaro wanauita msele.
 
Asante Sana mkuu,nimepata somo hapo,kweli tunajifunza kila leo
 
Reactions: 1gb
ndio ni majani ya maboga a.k.a msusa na yakifanywa hivyo unavyosema huitwa nswalu, pia huweza kupikwa yakiwa mabichi ila ili uwe mlenda lazima uweke bamia!.
Hahaha aisee kazi kwelikweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…