Nsoji go Nvaa
JF-Expert Member
- Oct 15, 2019
- 999
- 1,948
Mlevi mmoja akiendesha gari huku amelewa amewagonga na kuwaua Wanafunzi wa Tatu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Mama mjamzito na boda boda wawili maeneo ya Makulu opposite na ofisi za TISS na makutano ya Shoppers mkoani Dodoma, baada ya ajali wananchi nao walimshikisha adabu kidogo kwa kumpa kipondo kizito na kuharibu vibaya gari lake.
=================
Watu wawili inasemekana wamefariki dunia na wengine 10 wamejeruhiwa Jijini Dodoma, baada ya kugongwa mfululizo na gari aina ya RAVA 4 lenye namba za usajili T156 EJJ.
Dereva wa gari hilo anadaiwa kuanza kuwagonga watu hao kuanzia eneo la Makulu Majumba Sita mpaka Makulu Darajani majira ya saa mbili usiku wa Novemba 03, 2024.
Watu walioshuhudia tukio hilo wamesema chanzo chake ni uzembe wa dereva aliyekuwa akiendesha gari hilo huku akidaiwa amelewa.
Chanzo: TBC