Mlevi aua Wanafunzi Watatu wa UDOM, Mama mjamzito na bodaboda wawili Dodoma

Mlevi aua Wanafunzi Watatu wa UDOM, Mama mjamzito na bodaboda wawili Dodoma

Hapana,
Huyo anafunguliwa kesi ya kuua kwa kukusudia, hio ni murder case,
Picha linaanza anakosa dhamana

Kakusudia vipi kwani anawajua hao aliowagonga? Punguzeni mihemko, hamuwezi jua alipatwa na nini!
 
Hao wana leseni ya kuua siku hizi.Yaani tangu upite ule muswada wanaweza kufanya chochote kile.

Kuna mmoja kule Chato miezi 2 iliyopita alimgonga Mtumishi wa Tanesco aliyekuwa kwenye Bodaboda. Yaani Bodaboda iko kwenye right truck wakashtukia wanagongwa na gari iliyokuwa inakuja kasi nyuma yao. Na Wakazi wa kule wanasema mgongaji ni maarufu kwa kuendesha roughly na alishagonga watu kadhaa mwaka jana.
 
Sasa inahusiana nini ya mlevi na ccm? Kwahiyo ccm ndio imemtuma mlevi akawagonge!
Labda Kwa kuwa tumerudi zama zile za unanijua Mimi ni nani.... Matukio mengi ya ajabu ajabu yametokea tangu aingie "Mama"... Na kesi zinaenda tu kimsegasega ... Labda ndio sababu yake.
 
Mlevi mmoja akiendesha gari huku amelewa amewagonga na kuwaua Wanafunzi wa Tatu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Mama mjamzito na boda boda wawili maeneo ya Makulu opposite na ofisi za TISS na makutano ya Shoppers mkoani Dodoma, baada ya ajali wananchi nao walimshikisha adabu kidogo kwa kumpa kipondo kizito na kuharibu vibaya gari lake.

=================

Watu wawili inasemekana wamefariki dunia na wengine 10 wamejeruhiwa Jijini Dodoma, baada ya kugongwa mfululizo na gari aina ya RAVA 4 lenye namba za usajili T156 EJJ.

Dereva wa gari hilo anadaiwa kuanza kuwagonga watu hao kuanzia eneo la Makulu Majumba Sita mpaka Makulu Darajani majira ya saa mbili usiku wa Novemba 03, 2024.

Watu walioshuhudia tukio hilo wamesema chanzo chake ni uzembe wa dereva aliyekuwa akiendesha gari hilo huku akidaiwa amelewa.

Chanzo: TBC
Tuanze kushughulika na aliyempa pombe
 
Sasa inahusiana nini ya mlevi na ccm? Kwahiyo ccm ndio imemtuma mlevi akawagonge!
Huyu bila shaka ni mtu wa ovyo. Hata ajali ambazo kiuhalisia zinahitaji umakini na kujijali ili kuziepuka ye anaisingizia CCM
 
Huku Arusha eneo la Mapambazuko kuna Mwehi jana pia kalewa kagonga Bajaj na kusababisha kifo cha baba wa watu aliyekuwa anarejea nyumbani.
 
Mlevi mmoja akiendesha gari huku amelewa amewagonga na kuwaua Wanafunzi wa Tatu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Mama mjamzito na boda boda wawili maeneo ya Makulu opposite na ofisi za TISS na makutano ya Shoppers mkoani Dodoma, baada ya ajali wananchi nao walimshikisha adabu kidogo kwa kumpa kipondo kizito na kuharibu vibaya gari lake.

=================

Watu wawili inasemekana wamefariki dunia na wengine 10 wamejeruhiwa Jijini Dodoma, baada ya kugongwa mfululizo na gari aina ya RAVA 4 lenye namba za usajili T156 EJJ.

Dereva wa gari hilo anadaiwa kuanza kuwagonga watu hao kuanzia eneo la Makulu Majumba Sita mpaka Makulu Darajani majira ya saa mbili usiku wa Novemba 03, 2024.

Watu walioshuhudia tukio hilo wamesema chanzo chake ni uzembe wa dereva aliyekuwa akiendesha gari hilo huku akidaiwa amelewa.

Chanzo: TBC

Mlevi hatari sana huyo. sasa anajipanga huko kwa sero
 
Back
Top Bottom