lee Vladimir cleef
JF-Expert Member
- Feb 5, 2013
- 9,571
- 35,475
- Thread starter
-
- #41
Unajua walevi ndio wanaoongoza kulipa Kodi kihalali.Kumbe Lissu anasubiri kupigiwa kura na walevi!!! ha ha ha ha ha!! lakini ni sawa tu, yeye mwenyewe chizi wanaomtaka walevi, iko poa tu
Mmekuwa mkinufaika na kura za walevi. Sasa hivi kibao kimegeuka zile hongoKweli Lissu ni wakuljnganishwa na walevi wasiojitambua kama huyo.
Ndugu mbona wewe unapenda Sana migogoro?
Kwani Mimi nikekufanyaje?
Mimi nimeandika nilichoshuhudia kosa langu Ni Nini?
Mbona unataka kuninyang'anya Uhuru wangu wa kutoa maoni au habari.
Wewe nitendee utakavyo weza ila
Mungu hapendi.Atajibu tu.
Ha ha haa wazo lako zuri Sana ,lakini laki moja atashindwa kufanya kampeni anaweza lewa akazima.Huyu mlevi anastahili fungi la kampeni kutoka Team Lissu, lakini asipewe kwa mlipuko. Tutampa laki moja kila weekend mpaka kampeni zimalizike.
Watu Wana machungu Bro.safi sana Mlevi,kumpigia Lissu ni lazima sio ombi
Ndugu mbona wewe unapenda Sana migogoro?
Kwani Mimi nikekufanyaje?
Mimi nimeandika nilichoshuhudia kosa langu Ni Nini?
Mbona unataka kuninyang'anya Uhuru wangu wa kutoa maoni au habari.
Wewe nitendee utakavyo weza ila
Mungu hapendi.Atajibu tu.
Na wanyonge wenyewe ndio ho.Lissu cni chaguo la wanyonge!!
Ni kweli kabisa ubongoni kwangu Kuna walakini lakini haiondoi Haki yangu ya kuishi na kujumuika na wanyonge wenzangu.Ukiona 'nakung'ang'ania' hivi jua nimeshagundua kuwa 'Ubongoni' mwako kuna walakini mkubwa sana, hivyo Mimi ninakusaidia tu kukuweka sawa.
Ni kweli kabisa ubongoni kwangu Kuna walakini lakini haiondoi Haki yangu ya kuishi na kujumuika na wanyonge wenzangu.
Mimi nimeishia darasa la Saba wewe Ni dokta wa filosofia tutafanana vipi.
Ila tu naomba uniachie Uhuru wangu wa kuishi na kushirikiana na wanyonge wenzangu.
Tokea lini uliwahi ona mtu mwenye shida ya ubongo akaweza kujenga hoja.Jenga Hoja acha kutafuta 'Huruma' ya 'Members' hapa tafadhali sawa? Kujiita Mnyonge na Kuukubali Unyonge ni sehemu pia na Shida ya Ubongo.
Hali Ni teteMaisha yapo hovyo sana tusiwe wanafiki pesa hakuna mtaani,mazao:yote ya kilimo,biashara vyote vimeanguka..bado hujaenda kwenye utumishi mishahara haijawahi kupanda..miaka mitano
Watu tunaishi kwa marejesho!
Wana mambo mengi Sana mioyoni mwao,hivyo vitu wanavyotumini Ni kujipunguzia machungu tu.Ukitaka uhalisia na ukweli usio na unafiki ndani yake,jaribu kupiga story na wavuta bangi na walevi.
Alikua akitembea huku akipepesuka njia nzima mida ya saa tatu usiku.
Alikua akiongea peke yake muda mwingi,lakini kila aliyekutana nae alimshirikisha furaha yake bila kujali anamshirikisha Nani.
Alipokutana na Mimi,simjui hanijui,sikumpuuza Kama wengine walivyokua wakimpuuza.
Maneneo aliyokua akiyarudiarudia kwa furaha ya kilevi, Ni haya.
"Aaah nitampigia kampeni Dar es salaam yote".
Nikamuuliza Nani?
Akajibu" tayari wameshampitisha nakwambia"
Nikamuuliza Tena wamempitisha Nani?
Akanijibu kwa kunifokea" si Lissu!"
Nikamuuliza,wewe utamchagua Lissu?akajibu,"Tayari nimeisha Anza kumpigia kampeni kwenye vilabu viwili na ninaenda kwingine,nitafanya hivi Dar es salaam yote."
Na huko nilikotoka wamenielewa na wamekubali kumpigia,na huko nakoenda watanikubalia tu kwa sababu wananijua Sana,najulikan a Sana.
Kwa Nini unajulikana?
Akaanza kufunguka.
Kaka yangu amekufa.
Kabla hajafa alikua na nyumba nzuri tu Kimara.
nyumba yake ya Kimara ilibomolewa hakulipwa,
Familia ikakosa mahala pa kuishi.
Akarudi nyumbani mke na watoto akaacha kwangu,Mimi nimepanga chumba kimoja cha kuishi na ninafanya kazi ya kutembeza mitumba.
Kaka alikua mfanyabiashara wa korosho,akanyang'anywa korosho zake huko Mtwara kwa sababu hakua na shamba.
Kaka yangu akachanganyikiwa kabisa,akaugua "stroku" Hadi mauti yakamkuta.
Mke wake yaani Shemeji yangu yeye naye aliachishwa kazi kwa sababu eti walimwambia Hana Cheti,wakati aliajiliwa na serikali hiyihiyo,Sasa Kama Hana cheti walimwajilije? Aliuza mlevi.
Baada ya kuachishwa kazi na mme wake kunyang'anywa korosho na kwa kuwa nyumba Yao ilibomolewa bila kulipwa, na yeye kufukuzwa kazi Shemeji yangu nae akaanza kuumwa "Stroku"na yeye kafa.
Sasa nimebaki Mimi na watoto wao wanne,wawili wameacha kusoma chuo,wawili nawasomesha mimi ila Shule waliokua wanasomeshwa na wazazi wao niliwatoa.
Maisha yangu yamekua magumu,Sasa nimeamua kulewa tu,
Sina kazi,nilisomea ufundi wa mashine ( fitter Turner)
Nimemaliza chuo 2014 nimetafuta kazi miaka mitano sijapata.nimeamua kutembeza mitumba na kulewa tu.nina mke na watoto wawili wangu na wa Kaka wanne,jumla Nina watoto sita.
Nitamchagua Lissu na nitampigia kampeni vilabu vyote Dar es salaam.
Vilabu vyote nilivyopitia kabla hajapitishwa na baada ya kupitishwa wanamkubali Lissu.
Nilimtia moyo nikampa Sha 10,000=,nikaondoka yangu
Hiyo ndio hali halisi huko mitaani.
Kweli kabisa mkuu usione mtu anatumia pombe kupitiliza muulize nini chanzo kwanza ndio umuhukumu.Wana mambo mengi Sana mioyoni mwao,hivyo vitu wanavyotumini Ni kujipunguzia machungu tu.