Uchaguzi 2020 Mlevi mmoja aapa kumpigia kampeni Lissu kwenye vilabu vyote vya pombe za kienyeji DSM nzima

Uchaguzi 2020 Mlevi mmoja aapa kumpigia kampeni Lissu kwenye vilabu vyote vya pombe za kienyeji DSM nzima

Kumbe Lissu anasubiri kupigiwa kura na walevi!!! ha ha ha ha ha!! lakini ni sawa tu, yeye mwenyewe chizi wanaomtaka walevi, iko poa tu
Unajua walevi ndio wanaoongoza kulipa Kodi kihalali.
Kila mwaka Kodi huongezwa kwenye vileo.na hawajaacha kunywa.Mechi zote za Ulaya walevi ndio watazamaji wakubwa wakiwa Bar,mahotelini,au vilabuni.
Hawa jamaa taarifa za habari zote wanaangalia kwa hiyo wko informed kuliko wewe na Mimi.
Kwa mfano Mimi siangalii TBC lakini wao wanaangalia.
 
Ndugu mbona wewe unapenda Sana migogoro?
Kwani Mimi nikekufanyaje?
Mimi nimeandika nilichoshuhudia kosa langu Ni Nini?
Mbona unataka kuninyang'anya Uhuru wangu wa kutoa maoni au habari.
Wewe nitendee utakavyo weza ila
Mungu hapendi.Atajibu tu.

Ukiona 'nakung'ang'ania' hivi jua nimeshagundua kuwa 'Ubongoni' mwako kuna walakini mkubwa sana, hivyo Mimi ninakusaidia tu kukuweka sawa.
 
Huyu mlevi anastahili fungi la kampeni kutoka Team Lissu, lakini asipewe kwa mlipuko. Tutampa laki moja kila weekend mpaka kampeni zimalizike.
Ha ha haa wazo lako zuri Sana ,lakini laki moja atashindwa kufanya kampeni anaweza lewa akazima.
Kinachotakiwa kufanyika Ni kila jioni baada ya kampeni anunuliwe laga na michemsho, mpaka Uchaguzi utakapoisha.
Halafu mwisho kabisa ndio apewe malipo yake ya mwisho kwa jumla.
Ila msiache kuipelekea familia yake chakuala.
 
Ndugu mbona wewe unapenda Sana migogoro?
Kwani Mimi nikekufanyaje?
Mimi nimeandika nilichoshuhudia kosa langu Ni Nini?
Mbona unataka kuninyang'anya Uhuru wangu wa kutoa maoni au habari.
Wewe nitendee utakavyo weza ila
Mungu hapendi.Atajibu tu.

Ukiona 'nakung'ang'ania' hivi jua nimeshagundua kuwa 'Ubongoni' mwako kuna walakini mkubwa sana, hivyo Mimi ninakusaidia tu kukuweka sawa.
 
Lissu cni chaguo la wanyonge!!
Na wanyonge wenyewe ndio ho.
Mtu kapitia Calamity zote yaani Natural calamity na Artificial calamity.
Ila artificial calamity hua haitoki kichwani.hapa namaanisha kubomolewa,vyeti na korosho watu hawatakaa wasamehe hasira zao Ni oktoba.
 
Kweli watanzania wengi ni "zero brain" hakuna binadamu asiyekuwa na kiburudisho/kilevi chake...vile vile hakuna mtu anayekunywa pombe 24/7 kwa mwaka mzima....huyo bwana ana lake la "moyoni" wala sio mlevi .....!ni njia yake ya kufikisha ujumbe kwa wahusika !pombe ni kisingizio tu
 
Ukiona 'nakung'ang'ania' hivi jua nimeshagundua kuwa 'Ubongoni' mwako kuna walakini mkubwa sana, hivyo Mimi ninakusaidia tu kukuweka sawa.
Ni kweli kabisa ubongoni kwangu Kuna walakini lakini haiondoi Haki yangu ya kuishi na kujumuika na wanyonge wenzangu.
Mimi nimeishia darasa la Saba wewe Ni dokta wa filosofia tutafanana vipi.
Ila tu naomba uniachie Uhuru wangu wa kuishi na kushirikiana na wanyonge wenzangu.
 
Jenga Hoja acha kutafuta 'Huruma' ya 'Members' hapa tafadhali sawa? Kujiita Mnyonge na Kuukubali Unyonge ni sehemu pia na Shida ya Ubongo.
 
Maisha yapo hovyo sana tusiwe wanafiki pesa hakuna mtaani,mazao:yote ya kilimo,biashara vyote vimeanguka..bado hujaenda kwenye utumishi mishahara haijawahi kupanda..miaka mitano
Watu tunaishi kwa marejesho!
 
Jenga Hoja acha kutafuta 'Huruma' ya 'Members' hapa tafadhali sawa? Kujiita Mnyonge na Kuukubali Unyonge ni sehemu pia na Shida ya Ubongo.
Tokea lini uliwahi ona mtu mwenye shida ya ubongo akaweza kujenga hoja.
Naogopa kuendelea kupokea ushauri wako maana mwisho wa siku watu watakuona wewe ndio mwenye shida katika ubongo kuliko Mimi.
Kwa sababu unanilazimisha Mimi mtu mwenye shida ya ubongo nijenge hoja,wewe Mtu timamu kabisa uliona wapi hiyo?

Ni sawasawa na Mtu kumpiga Simba risasi kisa kala Swala,watu watakuona una tatizo katika ubongo,kwa sababu Swala Ni chakula Cha Simba.
 
Maisha yapo hovyo sana tusiwe wanafiki pesa hakuna mtaani,mazao:yote ya kilimo,biashara vyote vimeanguka..bado hujaenda kwenye utumishi mishahara haijawahi kupanda..miaka mitano
Watu tunaishi kwa marejesho!
Hali Ni tete
 
Kama wewe si mlevi huwezi kumpigia kura Lissu,ndio maana Chadema wanajiita ukawa (pilsner)
Alikua akitembea huku akipepesuka njia nzima mida ya saa tatu usiku.

Alikua akiongea peke yake muda mwingi,lakini kila aliyekutana nae alimshirikisha furaha yake bila kujali anamshirikisha Nani.

Alipokutana na Mimi,simjui hanijui,sikumpuuza Kama wengine walivyokua wakimpuuza.

Maneneo aliyokua akiyarudiarudia kwa furaha ya kilevi, Ni haya.

"Aaah nitampigia kampeni Dar es salaam yote".

Nikamuuliza Nani?

Akajibu" tayari wameshampitisha nakwambia"

Nikamuuliza Tena wamempitisha Nani?
Akanijibu kwa kunifokea" si Lissu!"
Nikamuuliza,wewe utamchagua Lissu?akajibu,"Tayari nimeisha Anza kumpigia kampeni kwenye vilabu viwili na ninaenda kwingine,nitafanya hivi Dar es salaam yote."
Na huko nilikotoka wamenielewa na wamekubali kumpigia,na huko nakoenda watanikubalia tu kwa sababu wananijua Sana,najulikan a Sana.

Kwa Nini unajulikana?
Akaanza kufunguka.

Kaka yangu amekufa.
Kabla hajafa alikua na nyumba nzuri tu Kimara.
nyumba yake ya Kimara ilibomolewa hakulipwa,

Familia ikakosa mahala pa kuishi.

Akarudi nyumbani mke na watoto akaacha kwangu,Mimi nimepanga chumba kimoja cha kuishi na ninafanya kazi ya kutembeza mitumba.

Kaka alikua mfanyabiashara wa korosho,akanyang'anywa korosho zake huko Mtwara kwa sababu hakua na shamba.

Kaka yangu akachanganyikiwa kabisa,akaugua "stroku" Hadi mauti yakamkuta.

Mke wake yaani Shemeji yangu yeye naye aliachishwa kazi kwa sababu eti walimwambia Hana Cheti,wakati aliajiliwa na serikali hiyihiyo,Sasa Kama Hana cheti walimwajilije? Aliuza mlevi.

Baada ya kuachishwa kazi na mme wake kunyang'anywa korosho na kwa kuwa nyumba Yao ilibomolewa bila kulipwa, na yeye kufukuzwa kazi Shemeji yangu nae akaanza kuumwa "Stroku"na yeye kafa.
Sasa nimebaki Mimi na watoto wao wanne,wawili wameacha kusoma chuo,wawili nawasomesha mimi ila Shule waliokua wanasomeshwa na wazazi wao niliwatoa.

Maisha yangu yamekua magumu,Sasa nimeamua kulewa tu,
Sina kazi,nilisomea ufundi wa mashine ( fitter Turner)
Nimemaliza chuo 2014 nimetafuta kazi miaka mitano sijapata.nimeamua kutembeza mitumba na kulewa tu.nina mke na watoto wawili wangu na wa Kaka wanne,jumla Nina watoto sita.

Nitamchagua Lissu na nitampigia kampeni vilabu vyote Dar es salaam.
Vilabu vyote nilivyopitia kabla hajapitishwa na baada ya kupitishwa wanamkubali Lissu.
Nilimtia moyo nikampa Sha 10,000=,nikaondoka yangu
Hiyo ndio hali halisi huko mitaani.
 
Back
Top Bottom