Jirani yetu zamani alikua bibi mmoja wa kale kabisa.
Pale kwake alikua na ghorofa la wakoloni,si tumejenga hapo nyuma kwake na kuipata barabara lazima upite pale.
Sasa ye na mdingi walikua hawaelewani lugha.
Anampangia mdingi njia ya kupita na usafiri wake.
Mdingi afisa mipango miji yani anamletea mazereu ile kwamba "wewe nani nikitaka hapo kesho hata wewe unaondoka"
Kumbe ilikua sio utani,yule bibi onyo la kwanza,
Mzee kapita nalo palepale,kapiga mzinga mbele,onyo la pili mzee kasahau kapita tena palepale.kala mzinga mjini,onyo la tatu mzee kasahau kapita border yake ile ile kala mzinga kimoja.
Ndo kwaheri mpaka leo.
Cha ajabu mle kwa yule bibi nilikua nakatiza humo ndani sana tu,mapera yake naiba sana tu pale mbele kuna mwembe mkubwa mi naenda nachuma maembe yangu natoka baru mchana kweupe.
Hakunifanya lolote.
Ila kwa mzee ilikua tofauti.