Mlio Hamia nyumba zenu mpya, Majirani zenu Shwari au Vita?

Mlio Hamia nyumba zenu mpya, Majirani zenu Shwari au Vita?

Mimi alikuwa jamaa anahamia nyumba yake mitaa niliyopanga, sasa kufika mpaka lilipo geti lake kuna nyumba ipo barabarani na hio barabara ni ya huyo jamaa aliitoa tu watu wapite.
Siku ya kwanza ikapita kimya, after a week mke wa yule jamaa akamuambia mume wake, huyu mwanajeshi anapitisha gari lake.

Basi kesho asubuhi akamsubiri apite, alivyopita tu akamsimamisha akamwambia naomba hii njia ife sababu ni sehemu yangu halafu anaongea kwa nguvu. Yule mwanajeshi akasema haina shida ndugu alimjibu very humble.

Baada ya kama wiki kazaa yule mjeshi akamtuma mtu aongee na jamaa, yule mzee akagoma ikabidi mzee amfate kwake, akamwambia ndugu yangu naomba ninunue hii njia. Uwezi amini yule mjeshi alinunua ile njia kwa 2milion.
Na hakukataza mtu.

Baada ya muda yule mzee alikufa sababu alikuwa anakunywa sana pombe wanasema mapafu yalipata shida. Siku anazidiwa usiku wa manane walienda kumuomba usafiri yule mwanajeshi. Bila kinyongo jamaa alitoka usiku kumpeleka hosptali mpaka kwenye msiba jamaa alitoa maturubai yake.

Viumbe vzuri bado vipo duniani.
Kweli dawa ya ubaya ni wema
 
Kununiwa bila sababu, hujatukana wala kugombana na mtu ila unanuniwa tu na majirani.
 
Kabisa aisee na uwe mtata ila ukiwa mpole watakupanda kichwani ,majirani ni watu wa ajabu sana nimejifunza ww unaweza kuwa fea ila wakakukanyagia tu ,na hata ukisema ujitoe kwa kiasi gani kwa ajili ya ujirani malipo utayolipwa na maneno ya kuzushiwa hutakaa kuwa na hamu wala ushirikiano na hao majirani ,Mungu akikujaalia ,weka fensi piga geti m'baki salamu au kukutana kwenye msiba au shereha tu
Hahaaaaa kuishi na watu weusi ni kazi sana.
 
Kuna watu kwa lugha ya kizungu cha mtaani wanaitwa "KAREN" Hawa ni wale watu wanoko hawaridhiki mpaka wakikuona unateseka na wanajihisi wao ndio wao wengine wote hawastahili.

Ukipata jirani wa hivi utajua haujui.
 
Hahahah, Ila heshima huja kwa kuweka busara mbele.. huyo Mwanajesh ata cheo atapata kazin kwa urahisi maana hana ubabe wa kijinga bali amebarikiwa hekima.. ukifuatiloa utakuta ana cheo. na hicho cheo hupewi wajinga wasio na busara .ninamtabiria cheo kikubwa zaidi uko mbelen
Yes wangekuwa wale makuruta kesho yake jamaa angewaita wenzake wakajazana hapo kumtisha mwenye barabara
 
Back
Top Bottom