Mlio Hamia nyumba zenu mpya, Majirani zenu Shwari au Vita?


mmepata bahati kuwa na uyo jirani mjeshi,
 
Aise hii kali. kama nimekuelewa mzee kafariki kwa ajali au ni gari tu ilipiga mzinga?
 
Dah. aisee kuna visa havi kwepeki ni Yesu tu aamue.. Embu I magine umejituma kwa jasho lako umejenga kwako jirani anaenda kwa mganga kuku tupia majin?? bora Yesu wako ali muwahi ..safi sana.. Pole pia kwa hicho kisa hatari sana
 
Mi nilipo hamia Majilani wakajua mi ni Usalama. Badae nilikaa om wakati wa korona nikawamafanyia kazi nyumbani wakajua nimefukuzwa kazi. Wakafurahi mno. Badae nikatoa sapoti ya kujenga Barabara, wengine wakanuna na wengine wakachekelea. Majilani ni watu wagumu sana kuwaelewa.
 
Bila shaka huyo bi mkubwa kajifunza kitu kama kweli zinachaji
 
Mie dadaangu mpaka leo nyumba yake hajaingia japokuwa ameshaimaliza yote na umeme ameweka sema ndo hvyo alimchukua jirani yake akamweka amlindie.

Mpaka leo kila anachogusa hamna kitu jirani kila akiambiwa mwez ujao ntahamia lazma itokee sababu ndug yang itayomfanya ahairishe leo nazungumzia mwaka wa 15 toka nyumba imalizwe jirani kagoma kutoka
 
Duh.. hii sasa hatari.. uchawi huo.. dada aende kwenye maombi apeleke Kiongoz wa kiroho haraka maana wana weza muondoa
 
Usiombe Upakane na Mhaya hawa watu wanatabu sana katika mipaka ,Kuna jamaa ni mhaya nimepakana naye aisee tumesumbuana sana mpaka nilipojenga ukuta ,ni watu wabinafsi wachoyo wa mimi na ukiwa legelege kila siku atakuwa anasogeza mpaka ,
Pia hawa wagogo nao sio waelewa kabisaaa ..Ila nilichojifunza ili kuishi kwa amani jitahidi ujenge fensi
 
Kweli kabisa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…