Mlio Hamia nyumba zenu mpya, Majirani zenu Shwari au Vita?

Kweli kabisa!
Yaan acha kabisa Ukiishi kwenye maisha ya kupanga unasema mwaka wa kupata kwangu ntatulia ,Sasa ngoja upate kwako ukutane na viama vya majirani ,kila Siku mnagombana mipaka kufungiana njia usiombe ukawa na kausafiri basi tafrani tu ,yaani haya maisha yanahitaji ujasiri sana na usipende mazoea na watu ,shiriki katika mambo mbali mbali ya kijamii inapotokea shida saidia ila mazoea yasizidi kabisaaa
 
Yaan mpaka mkosane ndio amani itakuwepo
 
Yaan mpaka mkosane ndio amani itakuwepo
Kabisa aisee na uwe mtata ila ukiwa mpole watakupanda kichwani ,majirani ni watu wa ajabu sana nimejifunza ww unaweza kuwa fea ila wakakukanyagia tu ,na hata ukisema ujitoe kwa kiasi gani kwa ajili ya ujirani malipo utayolipwa na maneno ya kuzushiwa hutakaa kuwa na hamu wala ushirikiano na hao majirani ,Mungu akikujaalia ,weka fensi piga geti m'baki salamu au kukutana kwenye msiba au shereha tu
 
Kabisa nilikuwa siwaelewi watu walopiga Fensi ndefu na kubwa ni majiran wa hovyo kabisaa mkitoka ni salamu tu hakuna kujuana juana
 
Unapenda sana udaku dogo. Deal na mambo ya nyumbani. Kwako kama si shwari unataka ukafanyeje? Ya kwako yanakushinda unataka na habari za wenzio. Fanya kazi uwe busy hutotaka kujua mambo yasiyokuhusu.
 
Kabisa nilikuwa siwaelewi watu walopiga Fensi ndefu na kubwa ni majiran wa hovyo kabisaa mkitoka ni salamu tu hakuna kujuana juana
Yaani haya mambo mpaka ya kukute ndo utaelewa ,maana kwa kusikia tu unaenza ona jamaa alopiga fensi ni anaroho mbaya hataki ujirani na watu n.k ,maana kawaida ya binaadamu na hasa majirani wanaanza kukuchokoa ukijibu mashambulizi ama kwa kujenga ukuta n.k wanaanza kuact kama wao ndo umewaonea ww ndo mkorofi ,

Mimi mzee wangu sikuwahi kumwelewa maana yeye alipiga kozi 15 nyumba nzima kuzunguka majirani yaani mlikuwa mkiwa ndani kama mko kisiwani [emoji23]
Ila nimekuja kumwelewa baada ya mimi kujenga na kukumbana na adha ya majirani nami nikafata nyayo zake [emoji23] sasa tuna amani mpaka mtu anakuonea hamu ,ukitoka uko kwenyw gari kioo juu full Tint ...yaani tunaishi nao aisee
 
Mbaya zaidi uwe umejenga nyumba inayoonekana bora kuliko wao. Hapo watakufyonza, kukusema eti unaringa nk
 
Safi sana aiseee
 
Point..jishushe...kuwa mnyenyekevu....
 
Unapenda sana udaku dogo. Deal na mambo ya nyumbani. Kwako kama si shwari unataka ukafanyeje? Ya kwako yanakushinda unataka na habari za wenzio. Fanya kazi uwe busy hutotaka kujua mambo yasiyokuhusu.
Kama jambo halikuhusu ukijihusisha nalo lazima uonekane mwehu.. kwamba hao wanao jibu matukio yenye mafunzo na hao wanaosema wamejifunza kupitia uzi huu wote ni wajinga wewe ndio mwerevu?? Ukiona huelewi sababu ya jambo pita mbali usitake hata kulisogelea utakuwa kama kituko.. ambayo wewe umekuwa kituko hapa.
 
Unapenda sana udaku dogo. Deal na mambo ya nyumbani. Kwako kama si shwari unataka ukafanyeje? Ya kwako yanakushinda unataka na habari za wenzio. Fanya kazi uwe busy hutotaka kujua mambo yasiyokuhusu.
Nahakika moja ya majirani wenye gilba na hila uko mtaan kwako wewe ni mmoja wao.. hivyo ina kuuma sana kuona tuna peana mbinu za kudeal na nyie. Wewe bila shaka ni mshirikina, mwenye wivu na mwenye roho mbaya sana.. hata uandishi wako una dhibitisha ulivyo nafsin mwako..
 
Dogo unapenda sana udaku
 
Unapeana mbinu ukiishi kwa shemeji yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…