Mlio karibu na Tundu Lissu mumkanye aache mara moja kuropoka ropoka!

Mlio karibu na Tundu Lissu mumkanye aache mara moja kuropoka ropoka!

Lisu ni mwanasiasa mzuri ila huwa hachagui cha kuongea na muda mwingi huchambua watu au matukio kuliko sera yaani hucheza na fursa, hizi ni tabia za wanaharakati. Mfano kwa sasa anazungumzia zaidi Ngorongoro na bandari kuliko kutangaza sera yao, na hii ndio imekuwa tabia ya chadema kwa muda mrefu yaani wanapata wafuasi kwa kuwa ccm imewaudhi watu sasa siku ccm ikirekebisha makosa yake kama enzi za JPM na wafuasi wakianza kurudi nyumbani wanasema wananunuliwa, wanasau kuwa kila mtanzania by default ni mwana ccm huko upinzani hua wanaenda baada ya kuchukizwa na baadhi ya tabia za ccm.

Hivi sasa wao wanafurahia wananchi kurudisha kadi za ccm wanadhani wamewaelewa sana sera zao za majimbo kumbe ni hasira tu zinazotokana na kuchikizwa na baadhi ya mambo ya ccm, siku wakianza kurudi nyumbani wasianze kulalamika tena wanapaswa watangaze sera zao wananchi wazielewa ndipo wafanye maamuzi ya kuhama chama. Huu ni ushauri tu.
 
Back
Top Bottom