Mlioezeka paa contemporary mvua zimeanza hali ikoje kwako?

bora ulivyoamua kufanya hivyo
 
wakuu hiden roof au contemporary haina shida yoyote shida ipo kwenye mafundi wenu mnaowachukua hawajui kazi, ukiweka sinn roof(gundi ya kuzibia kwenye ukuta na bati) na wall flash cover kuvuja utakusikia kihama.
mnalalamika sababu ya kuchukua mafundi kanjanja ambao hawajui chochote
 
Mkuu nilikuta nyumba ya kiongozi wa mkoa X kajengewa nyumba ya mfumo huo wa hidden roof na injinia wa mkoa lakini ilikuwa inavuja kama meli ya Titanic. Tangu lile tukio mimi nahisi nyumba hizo zipauliwe kwa zege yani ziwe na msingi imara na nguzo za kutosha kubeba zege (ROOFING) yaan kama vile unataka kujenga ghorofa.
 
Kwa mvua nilivozishuhudia huku niliko, ukiwa na hizo nyumba za kuficha paa lazima utatoka mwenyewe humo ndani uende kutafuta sehemu salama ya kujificha maana mvua ni kali balaa na ina upepo mwingi hadi unahisi paa la nyumba linanyanyuka sasaivi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…