Mliofanikiwa kutoa Zaka asilimia 10% ya vipato vyenu mmewezaje? Binafsi naishia kusaidia 2% hadi 4%

Mliofanikiwa kutoa Zaka asilimia 10% ya vipato vyenu mmewezaje? Binafsi naishia kusaidia 2% hadi 4%

NetMaster

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2022
Posts
1,454
Reaction score
4,925
Kwangu mimi kwa lgha nyepesi Zaka ni kutoa 10% ya ulichopata kwa jasho lako kihalali kiende kubeba wenye shida, binafsi naiona ni kama kodi fair kabisa ya kuweza kuishi na kupata rizki kwenye dunia hii ambayo ina mwenye nae alieiumba.

Nadhani huwa inahesabiwa zaidi unapomsaidia mtu mwenye shida na hawana ukaribu na wewe ama mnajuana kwa mbali, wale mnaojuana karibu huwa ni msaada na si zaka.

Ni adaka pekee huwa natoa kanisani lakini kuhusu Zaka huwa najaribu kuitoa kwa watu wenye shida naokutana nao ila hadi sasa sijawai toa 10%>

Binafsi nineshindwa kuweza kufikia hio asilimia 10, huwa bili zinanizonga najikuta bili zangu inabidi ziwe na kipaumbele kuliko hii zaka ambayo naichukulia kama kodi ya Sir God alienipa uhai moaka sasa.

Tangu naanza kupata elf 30 kwa mwezi hadi sasa nikiwa naweza kupata milioni 2 hadi 3 kila mwezi nikiri wazi nilikuwa nahitahidi kutoa fungu la kumi ila sijaweza mpaka sasa.

Mfano kwa mwezi uliopita nilipata kama milioni 2 na laki 3 hibi hivi ila nikajikuta naishia kutoa zaka kama elf 80 hivi, Mtindo wangu wa kutoa zaka Huwa nagawa gawa hizi buku buku na elf 2 kwa watoto wa mtaani, nikikuta mtu anauza miwa na karanga kwenye ungo nampa elf 2 nasema ntapitia baadae ila sirudi, n.k.

Yani kiufupi nakuta matumizi yananibana sana na naanza kujidanganya yana umuhimu sana kuzidi zaka, mlioweza kufikisha hio 10% ya kipato kile halali naombeni ujuzi.
 
Hadi hapo nakutangazia amani malangoni pako na wanao watajaa amani .Milango unayoitikisa kwa hicho unachoita kidogo ikumbuke comment hii ndani ya 2 to 5 yrs utakuwa mwingine kabisaaa.
 
Kasome Malaki 3:8-10... Pia umesema unalipa Kodi kwa anaekupa pumzi afu unamwibia Tena anekupa uhai,ume ahi jiuliza he akiitoa hiyo pumzi unayovuta utapata wapi uwezo wa kupata iyo 2m? Watu wanapata 300k na wanatoa zaka ndo iwe 2m mkuu? Mrudie MUNGU wako acha kumwibia
 
Mkuu jitahidi sana kutohukumu .huyu mpendwa amejieleza ukweli na anayoyatamania .kumcha mungu ni jambo la kujiboresha kwa bidiii kila siku .kupeana moyo kuombeana mnafika hatua za juu.nilipwe mil 1 mwanangu ahitaji mil 1 ya operation ya moyo unataka nizoe laki 1 kwa yatima wale soda mwanangu afe??
 
Kuwa na imani kwa hicho kidogo unachokitoa
Acha kumdanganya mwenzio mkuu
Mkuu jitahidi sana kutohukumu .huyu mpendwa amejieleza ukweli na anayoyatamania .kumcha mungu ni jambo la kujiboresha kwa bidiii kila siku .kupeana moyo kuombeana mnafika hatua za juu.nilipwe mil 1 mwanangu ahitaji mil 1 ya operation ya moyo unataka nizoe laki 1 kwa yatima wale soda mwanangu afe??
Sina maana hiyo mkuu sijamhukumu hapo, laiti ningehukumu ngesema direct kwamba sbr kuchomwa Moto au ww ni wajehanam hapna.. na ndio maana nimempa na mifano ya mistari kwny bible....
 
Kasome Malaki 3:8-10... Pia umesema unalipa Kodi kwa anaekupa pumzi afu unamwibia Tena anekupa uhai,ume ahi jiuliza he akiitoa hiyo pumzi unayovuta utapata wapi uwezo wa kupata iyo 2m? Watu wanapata 300k na wanatoa zaka ndo iwe 2m mkuu? Mrudie MUNGU wako acha kumwibia
Brother kumwibia Mungu kwa kile kidogo ninachopata ambacho hata hakikidhi haja, then hata hiyo pumzi inayosemea kwamba anatuuzia au, kwamba tuli request kwake atupe hio pumzi kisha tumlipe kupitia kwa wachungaji wake ambao wanaishi kitajiri?

Definition ya zaka bado haijaeleweka na haita eleweka kamwe kwa aina ya mafundisho tulio nayo
 
Daah aisee... Zaka Ni amri sio hiari ujue? Hata kiwe kidgo vipi Ni lazima utoe!! Lengo la zaka Ni kumwonesha Mwenyezi Mungu utii wetu je tutamheshimu kwa kila Pato letu? Kimbula imeandikwa mheshimu Bwana MUNGU wako kwa Mali yako yote... Hivyo Zaka ni agano la MUNGU na mwanadamu lililoasisiwa na Yakobo.... Zaka imekua shida ivi je Malimbuko itakuaje sasa😄
 
Hiyo siyo Zaka unayofanya ni msaada kama kuwasaidia wajane na yatima na wasiojiweza

Zaka inapelekwa Nyumban mwa Bwana

Malaki 3:10
Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema BWANA wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.
 
Mkuu hongera kwa kuupiga mwingi mpaka unamwagika, binafsi nikushauri kama wewe ni Mtumishi wa Serikali tayari unakuwa umetoa fungu la kumi kupitia Income Tax (PAYE) ambao hiyo fedha inarudi kwa jamii katika kuboresha huduma mbalimbali kama afya na elimu. Kwahiyo usipasue kichwa mzee kwa hizi taasisi za dini zilizojikita kuhubiri matoleo badala ya kazi zao za Msingi kuhubiri neno. Naamini sadaka inawatosha sana. Tambua ya kuwa Mungu wetu si masikini kusema usipotoa hiyo anapoteza mapato.

Ndiyo maana hata mafundisho yanahimiza kurarua mioyo yetu na si mavazi yetu, pia yanahimiza kujikita katika usafi wa Moyo na sio wingi wa matoleo yetu.

Sent from my TECNO KC6 using JamiiForums mobile app
 
Kama unapotoa hiyo asilimia kumi unaumia kutoka moyoni na kibaya zaidi bado hata yenyewe huitoi kikamilifu basi tambua si wewe bali ni shetani ndiye hataki wewe umtolee Mungu kwa uaminifu,shetani mara zote huchukizwa na mtu anapokuwa muaminifu kwa Mungu.

Inapaswa ujiulize kwanini hiyo asilimia kumi ikuume sana kuliko fedha nyingine ambazo unapoteza na kuharibu kwa mambo yasiyokuwa na faida?
 
Back
Top Bottom