Mliofanikiwa kwenye Network Marketing tunawaomba mtoe Ushuhuda hapa

Me nawaza kuanza kuuza maharage kuna mtu anakuja kukwambia biashara za kuwa bilionea ghafla..ingekuwa hivyo kila mtu angekuwa bilionnea...no pain no gain....tujitume hakuna shortcut
 
Wiki 4 zilizopita aliyekuwa classmate wangu alinisumbja sana, alinambia kuna ishu ya investment inaweza kuniingizia mamilion, mimi nikadhan ni true investment, maybe ana project proposal ambayo tunaweza kuingiza pesa tukapata pesa hv

Au maybe kuna kampuni unadhamin mikopo hivi, nikamwuliza ni ishu gani? Akasema haitoshi kuongea kwenye smu maana ni ishu pana.... dah nikatafakari... nikamwuliza, ni forever living? Akasema No, nikamwuliza ni Alliance? Akasena NO... doh.... nikamwambia nidokeze, akasema tuonane....

Sasa kwa kuwa nina miaka sjaonana naye tangu tulivyomaliza chuo, ikanbd niwapigie watu wake wa karibu, mmoja akasema alisikia anafanya kaz kampuni ya mikopo... nikasema oh bas huenda kuna mikopo huku, na kwa kuwa mimi siogopi mikopo na nina shida na pesa za kuingiza kwenye miradi... nikasema ngoja niende..........


Sku imefika, nikachukua usafiri.... fuuuuuuuu mpaka mwege...

Lahaula, kufika kule ananambia hii ishu inaweza kukuingizia had m. 15 kwa mwezi na hata kwa siku

Ishu gani mama???? Q_Net...... mimi lohhhhhh ehz inakuwaje.... oh unanunua bidhA hata moja, unajiunga, na ww unatafuta watu wanajiunga.... aseh, nikafanyiwa semina na watu karibu wanne..... mara kuoneshwa mapicha sjui nini

Dahhhh nilimwangalia classmate wangu nikamhurumia sana, nikawatazama wale vijana wengne wanaosema unapata hata m. 15 kwa wiki, mavazi yao hayafanani hata kidogo, ni watu wanaoonekana bado wanahangaika na kufungwa kifikra......

Sikutaka kuwaudhi, nikawaambia mimi nafanya miradi binafsi.. hata hvyo, nitawasiliana nanyi kesho...... ikawa kimoja

SHIME VIJANA, TUACHE SHORTCUT, PESA ZIPO KAMA TUTAJIINGIZA KTK MIRAD HALISI, KUTHUBUTU PASIPO KUJATA TAMAA. HAKUNA SLOPE KTK KUTAFUTA PESA, TUKUMBUKE MUDA UNAKWENDA

ni heri ukakodi shamba upande mpunga, uvune uuze
 
Hahahahaha Story yako inachekesha na kufundisha
 
Me nawaza kuanza kuuza maharage kuna mtu anakuja kukwambia biashara za kuwa bilionea ghafla..ingekuwa hivyo kila mtu angekuwa bilionnea...no pain no gain....tujitume hakuna shortcut
Yaah kwakweli. Asee!!
 
Damn!!!
 
Hii upuuzi inachukua sana wale vijana ambao ndio wamemaliza chuo na wako desperate na ajira,

Mzazi mkanye mwanao, utapeli umeingia mjini
 
Kuna moja hiyo rafiki yangu alinipeleka huko, ofisi zao zilikuwa pale kinondoni sijui sasa kama bado wapo! maana ilikuwa 2yrs ago.
Ile kuingia tu kwa ofisi naona kila mtu ananisalimia GOOD MORNING na wakati huo ni jioni ya saa tisa, Duh walinipotezea muda wale watu siku ile, na ndicho walichofanikiwa kunipotozea muda, ila kwa kifupi sikuwahi kurudi tena, na huyo rafiki yangu urafiki ulikufa imebaki kujuana tu sababu alikuwa anajua kabisa yale ni masinema ila alitupoint watu ambao angalau tulikuwa na chochote kitu ili yeye apate fungu lake,
Kifupi hakuna pesa ya mtelemko.
 
Wacha kuita watu waongo wakati akili zako ni finyu. Umeshindwa hata kufahamu comment yangu.
Sasa nimekupata ucjali mkuu! Lkn na mm nilihudhuria semina zote ukihitaji full data nitakupa. Ila sijajiunga kila siku wananipigia simu nikakope benki au niuze kiwanja
 
Habri zenu ,,wakuu ,, mwenye uelewa na kampuni ya forever living naomba kunijuza ,,ijihusiayo na online marketing
 
Adi September sijaona shuhuda dah

Mm ndo shuhuda wao sasa,

hizi kampuni za network marketing sijui, forever, Alliance, q net, Bf suma, n.k nikajua zipo kwa wizi Tanzania kumbe zimesajiliwa adi BRELA , TRA, kama distributor tu wa diet supplement, vitu vya urembo ndo saa, mikufu ( q net) na kuuuza na sio kutoa utajili wa bure kwa watu wanyonge


Ila kinachofanyika ndo tofauti na makubaliano ya leseni zao, wao wanatakiwa kusambaza diet supplement mfano forever living, alliance, ndo wanaziuza ila wao wanadanganya watu kuwa zinatibu magonjwa kama vile cancer, stroke, nk.


Wale walio na elimu kidogo ya madawa ya binadamu wanajua diet supplement ni tofauti na dawa za hospital ambazo MSD inasambaza kwa ajili ya kutibu ugonjwa wa vimelea vya mwilini.


Sasa ukifika pale kila mtu ni MD, na mphamacist kwa hizi kampuni utambiwa inatibu ichi mara ichi ila ukisoma leaflet (Ingredient ya dawa) wanasema tofauti not for therapeutic it's diet supplement.


Unachokipata kwa hawa watu ni commission kama M pesa tu baada ya kuuza na kuingiza watu hamna mujiza wa bilion wala nn.


Watu wanao jiunga sana ni watoto wa vyuo wengi sana wanakuta wametoka maporini wakitimba tu mjini wanambiwa utajili uko hapa unauziwa supplement na risiti juu ya efd, ukauze mwenyewe.


Nimeona watu wamejiunga kama 6 ivi mmoja ana miaka 3, wengine 2.5. Maskini tu adi leo wanaomba nauli ya dala dala hamna pesa rahisi kupata duniani na shortcut.


Ukiona mtu kafanikiwa uko ni wale chambo wa kwanza ili wavutie samaki wengine wavuliwe kisawa sawa,.

N.B Tanzania ukiitiwa fursa ujue ww ndo fursa kwao
 
Duhhj nomaa
 
Mimi mdada aliyekuja kunipanga nijunge nao aliniambia wanaimiliki timu ya man city... Nikamuuliza unaijua hata timu yenyewe na unamfahamu shehe Mansoor alibaki kutoa macho nikamfukuza.
Kakosea hakukariri vizuri, ila hawa wanatia huruma wakikujia ama kukualika ofisini kwao, wanatumia nguvu nyingi kupindukia kufanya ushawishi ili ujiunge, na istoshe ukiwatazama miongoni mwao utawakuta wamo partners ambao wameingizwa chaka na wenzao na wanajuta hadi kufikia kuumiza mioyo yao, hata sura zao utaziona wakati wanatoa ushuhuda wa mafanikio huwa wanalazimisha tabasamu, ila wengine hapohapo utagundua kuwa hawakubaliani na hiyo mikitu, ila basi tuu wamebakia ili kurejesha mitaji yao. Mm leo hii ndio narudi kupigwa shule ili nijiunge. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Oh hell no sio poa kabisa haki tena😂😂
 
Hahaaaa. Umejiunga au bado fursa hiyo
 
Kwa mwanza wapo pale pasiasi kuna rafiki yangu aliacha kazi kaenda kujiunga kwenye huu ujinga paka namuonea huruma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…