Mliofika China hivi bado mnawaamini hawa wanasiasa walioko madarakani kwamba kuna siku watafikia maendeleo ya Wachina hata kwa asilimia 3%?

Mliofika China hivi bado mnawaamini hawa wanasiasa walioko madarakani kwamba kuna siku watafikia maendeleo ya Wachina hata kwa asilimia 3%?

kambagasa

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2014
Posts
2,269
Reaction score
1,803
Naamini kuna Watanzania wengi mliofika China inasemakana kipindi cha miaka ya 1960 tulikuwa sawa kimaendeleo.

Hatua waliyofikia hawa watu hususani katika nyaja ya miundo mbinu, viwanda na usalama katika nchi yao hivi kuna Mtanzania yoyote anaota kuna siku tutawafikia hata asilimia 3 tu hawa Wachina.

Hakuna trafiki barabarani ni camera tupu na hakuna bango la Raisi wa China mitaani, jinsi Wachina walivyo busy kazini, hakuna muda wa kucheza Pool table Wala foleni iliyosababiahwa na kiongozi kwamba anapita.

Kwa kifupi sioni hata umuhimu wa kuwepo bunge nimevurugwa kweli.
 
Ya wachina tuwaachie wachina, walishatupita, na Sisi tuangalia namna gani ya kufika mbali pasi na kuwaangalia wao sababu kwa sasa sisi na wao ni mbingu na ardhi.
 
China walipata zali la mentali/ bahati ya kuwa na kiongozi Rais mzuri aliitwa Deng Xiaoping ndio alifanya mageuzi makubwa ya uchumi wa China.


Kamgugo Deng Xiaoping ndio utaelewa
 
Trust me inawezekana. Mpaka sisi tunaosema inawezekana tuamue iwezekane.

Rasilimali tunazo na sehemu za kuweka hiyo miundombinu tunazo. Nia ya dhati na uelekeo ndio tumekosa.

Afrika tuna Agenda 2063 ina malengo mazuri mno, Tanzania tuna Dira ya Taifa ya Maendeleo ina vitu vizuri vilevile isipokuwa kwenye kutekeleza ndio tumewaachia wale wasio na nia ya kufikia hayo malengo.
 
Sio Maendeleo To Hata ngono wanatuzidi


Wako wengi kichizi🤣
 
China walipata zali la mentali/ bahati ya kuwa na kiongozi Rais mzuri aliitwa Deng Xiaoping ndio alifanya mageuzi makubwa ya uchumi wa China.


Kamgugo Deng Xiaoping ndio utaelewa
Hakuna zali la mentali kwenye uongozi hata China ya kabla ya huyo kiongozi haikuwa sawa na Tanzania.
 
Back
Top Bottom