Mliokaririshwa uongo kuwa mishahara ya walimu ni midogo kuliko watumishi wengine wa serikali, nawaanikia hapa

Waliokuwa na akili kama zako saa hii wanasota!! Mfano wa karibu ni Sabaya!
 
Mkuu wewe unawatetea kwa maneno tu lakini huku mtaani hali zinawaumbua.

Waalimu ndio watu wasioamika kukopeshwa kwenye mabar huko, yaani akikopeshwa mwalimu basi muuzaji anahesabia maumivu tu.
 
Mikopo wanayo watumishi wote! Kama ni mikopo ya bodi ya elimu ya juu wanayo watumishi wa kada zote, kama ni mikopo ya benki na sakosi wanayo pia watumishi wote! Hayo ndiyo mambo waliyokaririshwa kuwa eti ni walimu tu wenye mikopo wakati siyo!
Shikamoo Mwalimu
 
Mkuu wewe unawatetea kwa maneno tu lakini huku mtaani hali zinawaumbua.

Waalimu ndio watu wasioamika kukopeshwa kwenye mabar huko, yaani akikopeshwa mwalimu basi muuzaji anahesabia maumivu tu.
Ni kwa sababu ya uelewa mdogo wa watu!! Walimu hawazidiwi chochote na kada zingine zaidi ya wizi na utapeli!! Nimehakikisha kuwa ndani ya miaka 10, walimu hufanikiwa na kuwa mbele sana katika maisha kuliko wenzao wa kada zingine!!

Huko vijijini wanalima sana, wala hawana shida ya maisha! Kuna mwalimu mmoja jirani yangu alijenga bonge la nyumba, watu hawakuamini kama ni nyumba yake, wakawa wanasema anasimamia nyumba ya mtu!!

Alipokuja kuhamia ndio wakaamini kuwa ni nyumba yake!! Wengine wakasema labda ni pesa ya kustaafu wakati bado ana miaka zaidi ya 15 ya kufanya kazi kabla ya kustaafu!! Alipojenga nyumba akaelekeza nguvu kwenye usafiri na sasa ana usafiri wake mzuri!! Akisikia watu wanadharau ualimu yeye anawachora tu!!
 
Mkuu hapa hatubishani kuhusu ukubwa wa mishahara bali unafuu wa maisha.
Sasa peaa ya wizi sio pesa ama??
 
Mwalimu mwenye degree Basic yake ni 771,000/=..? Kwan Askar Jesh au Polisi mwenye degree nae analipwa sh ngap nliwahi sikia wao wana mishahara miwili na katikat ya mwez wanalipwa
 
Nataka jamii ibadili kabisa mtazamo hasi na potofu kuhusu walimu!! Mwalimu si fukara, mwalimu si maskini, japo mwalimu anapunjwa mshahara (japo uko juu kuliko wengine) kulingana na ugumu wa kazi yake1! Kwenye nchi zilizoendelea mwalimu ndiye hulipwa mshahara mkubwa sana!

Mabinti msiogope kuolewa na walimu! walimu wanajua maisha, walimu wana mipango bora ya maisha! Ukitaka kulijua hilo linganisha walimu wastaafu na watumishi wastaafu wa kada zingine!! Mwisho wa siku mwalimu yuko juu!!
 
Watumishi wengine wanalipwa overtime kwa siku 15 kwa mwezi ambazo hazikatwi kodi , kwa rate ya sasa 60,000 × 15 = 900,000
Analipwa posho ys vikao na kazi, kupitia madokezo,
Mealimu ukitoa mshahara hana chochote kingine anachotegemea,akiukopea mshahara ndo kabisaaaaa utamuonea huruma!
 
Mwalimu mwenye degree Basic yake ni 771,000/=..? Kwan Askar Jesh au Polisi mwenye degree nae analipwa sh ngap nliwahi sikia wao wana mishahara miwili na katikat ya mwez wanalipwa
Kwa mwanajeshi sina uhakika, lakini kwa polisi wanapigwa gepu na walimu!! Halafu kupanda cheo kwenye upolisi ni ngumu sana!!Kwa zamani ukijiunga polisi na digrii autoimatically unakuwa afisa muda mfupi, lakini siyo leo!! Unabaki private na digrii yako hadi miaka ya kueleweka!! Hizo ndizo kazi zinazotegemea kipato ambacho si rahisi kukielezea kimaadili! rushwa, uonevu nk!1
 
Kujisifia wizi na madili kinyume na maadili kwa kada zingine ni aibu kwa Taifa na siku zote hakuna mwisho mzuri. WAlimu wana pesa za halali kwa mfano tuition ambazo ni nyingi sana mitaani. Mwalimu akistaafu bado taaluma yake inahitajika kwenye jamii na anaendelea kupiga pesa ya halali na yenye heshima! Lakini kichwa cha mwalimu kina chaji muda wote hadi uzeeni na anawasaidia sana watoto wake!! Ualimu ni mzuri na unastahili kuheshimiwa sana!
 
Of course, Walimu hawana mishahara midogo.

Mwalimu anazidiwa mshahara na kada za Afya, Engineering, na Sheria ( Advocate ) peke yake.
 
Ni afadhali niishi kwa kiwango kinachoendana na kipato changu kuliko kupokea rushwa na kujidanganya kuwa una kipato kikubwa, fainali ikifika kuna mmoja anaumbuka! Hivi mlishawahi kushuhudia maisha ya polisi wastaafu huko mitaani!!! Ni fedheha!! Wengi huishia kulinda kwenye majumba na maduka ya watu kwa kutumia virungu!! Mambo ya rushwa kwishney!!
 
Kwa haraka haraka tu, nimeelewa kwamba katika kada zote ni walimu pekee wasioiba Mali za umma, umasikini mkubwa kwa sisi wananchi unachombezwa na hao wezi uliowataja, TAKUKURU ingekuwa serious kushughulikia rushwa naamini serikali ingepata pesa nyingi mnooo!

Ila sasa TAKUKURU wapo busy kukimbizana na wanaoinanga CCM, nje ya hapo na wao wanalamba zao asali tu...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…