Mliokaririshwa uongo kuwa mishahara ya walimu ni midogo kuliko watumishi wengine wa serikali, nawaanikia hapa

Mliokaririshwa uongo kuwa mishahara ya walimu ni midogo kuliko watumishi wengine wa serikali, nawaanikia hapa

Hizi thread za kuwadhihaki walimu nna uhakika zinaandikwa na majobless,Its either walifeli shule kwa uzembe wao Ama wanassbabu zingine lwzima zitakua baseless tu.

Walimu wanamishahara madogo ama mikubwa how is that your concern? Walimu ni watumishi kama watumishi wengine wanastahili kuheshimiwa kama watumishi wengine,Sioni afya kabisa kila siku mkiwadhihaki Walimu, Haiwezekani kila mtu akawa wakili,daktari ama engineer sasa mnasumbuka nn nao? Unasema laki 7 ni ndogo think twice wewe unaingiza sh ngap
 
Hilo pia siyo kweli! Mtumishi lazima abaki na theluthi moja ya mshahara wake katika mazingira yoyote yale! Nimetoa mfano wa mwalimu graduate ambaya kwa sasa atakuwa anapata 771,000/=. Huyo akikopa sana lazima abakize sh 257,000/= kwenye mshahara wake. Lakini pia wengi wanakopa siku hizi kwa ajili ya kuendesha miradi mbalimbali kama kuku wa mayai au nyama, ng'ombe wa maziwa, shamba nk. Kwa hiyo japo anabakiza mshahara kidogo lakini ana kipato kingine cha pembeni na cha halali kuliko wale wanaojisifia wizi!!

Walimu wana maisha mazuri sana kwa kutumia akili yao kwa halali. Nenda shule yoyote iwe ya msingi au ya sekondari uangalie magari ya walimu waliyopaki hapo. Walimu wengi wamejenga nyumba zao za kisasa na wana miradi mbali mbali na watoto wao wanasoma vizuri kwenye shule nzuri. Tatizo mmekaririshwa matango pori!
Magari mengi ni ya walimu wanawake wamehongwa au kununuliwa na waume zao
 
Mikopo wanayo watumishi wote! Kama ni mikopo ya bodi ya elimu ya juu wanayo watumishi wa kada zote, kama ni mikopo ya benki na sakosi wanayo pia watumishi wote! Hayo ndiyo mambo waliyokaririshwa kuwa eti ni walimu tu wenye mikopo wakati siyo!
Unajitahidi sana kutetea kada ya ualimu lakn ukweli unabaki pale pale tu.!

Hata walimu wanafanya kazi shingo upande.!
 
kama wana mshahara mkubwa kwanini wao ndio wanaoongoza kwa kulialia?
Walimu hawaongozi kwa kulialia ila yeyote anayelialia jamii husema kwa makosa kuwa hutyo ni mwalimu. Hatujasema kuwa walimu wana mishahara mikubwa kwa maana watumishi wengi wa serikali wakiwemo walimu mishahara yao ni kidogo. Ila ukiilinganisha hiyo mishahara kidogo mshahara wa mwalimu uko juu kidogo kuliko wa kada nyingine (ukiacha madaktari, wafamasia, wahandisi wanaosoma kwa miaka mingi zaidi kuliko kada zingine)
 
Mkuu hii analysis ni balaaa 🤣🤣🤣🤣🤣
Walimu Hawana dili Wala marupurupu ya ziada Kama kada nyingine, hiki Ndo kinawafanya kua maskini Sana

1. Dreva wa halmashaur ana mshahara mdg kuliko mwalimu ila atapiga dili za vifusi,mchanga,kokoto n.k night za misafara n.k

2. Afisa biashara au ardhi wa halmashaur ana mshahara mdg kuliko mwalimu,
Ila atapiga rushwa za leseni za kufa mtu.

3. Afisa mifugo au kilimo atapiga elfu tano tano za sindano mifugo ya watu au atalima mashamba yake uko uchochoroni kwa kutumia dawa au pembejeo za ruzuku za serikali.

4. Mfamasia atakula laki tano tano kila mwezi for free za cheti chake tu kutumika kwny maduka ya dawa ya watu uko mitaani uku katulia tu..

5. Daktar au nesi wa halmashaur,
Hawa dili za semina,mafunzo n.k Ni nyingi mno(covid 19, chanjo, ukoma, malelia n.k). Hapo bado hawajaiba vifaa Tiba na kuviingiza mtaani kwenye hospital binafs.
[emoji117] Kuna na mabwana afya kaam matrafiki TU, wanatupiga Sana elfu hamsin hamsi Za faini uku mitaani

6. Wahasibu na maafisa manunuzi wa halmashaur wanapiga Sana dili za kimahesabu na 10% wakishirikiana na maboss wao (wakurugenz) ili Kupiga Cha juu kwenye tenda na matumiz mbalimbali ya fedha kwny halmashaur.

7. Maengineer wa halmashaur Ndo kabsaa wezi wakubwa, wao kila mradi wa serikali wakipewa kusimamia Lazima umalizike na yeye tayar ana kijumba keshakijenga kwa material zile zile za mradi.

8. Maafisa masjala wao Ni Kama matrafiki au madalali wa viunga vya halmashaur, una faili lako pale kwa mkurugenz au mkuu wa wilaya,ili likimbie chap chap Lazima utamwachia elfu 2 au elfu 5 ya maji.

9. Afisa maliasili wa halmashaur Hawa Ni wazee wa madili na rushwa za misitu,mikaa,mbao na magendo mbalimbali ya serikali.

10. Afisa utumiishi Hawa ndio wazee wa madili ya watumishi hewa.
[emoji117]Mtu anafariki, ripoti haiendi hazina kusitisha mshahara. Inatolewa ripoti ya mwajiriwa kubadili account yake, mshahara wa marahemu wanaula hata miaka 10 mfulurizo bila yeyote kujua.
[emoji117]mtu anamakosa ya kinidhamu,kasimamishiwa mshahara. Ripoti haiendi hazina, inabadilishwa tu account. Wanaupiga kimya kimya. Ukisamehewa ukarudishiwa mshahara, ule wa nyuma hata uulizii.
[emoji117]mtu anaripoti Ila haendi kituo Cha KAZI, au anaacha kazi anaenda zake private kwa muda.
wanakula dili na afisa utumishi, wanaugawana nusu nusu huku yeye Yuko zake private sector anapiga Ela nyingine.

Kama Kuna mtumish mwngne wa halmashaur nmemsahau nikumbushe.

Ila kiuhaisia mwalimu nje ya mshahara sijui atapiga dili gani atoboe,

ukiachilia mbali suala la twisheni ambalo bado kipato chenyewe Ni kidg mno na jasho linalomtoka Ni jingi mno

Sijui atapiga dili gan jingine maana vitabu vyote vya serikali vimeandikwa "HAKIUZWI", boksi lenyewe la chaki Mtaani halizidi hata elfu 2.
 
Jamii ya watanzania wanavyoelewa ni kwamba kazi ya ualimu ndiyo yenye mshahara mdogo kuliko kazi zingine zote. Hivyo hii imepelekea hadhi ya mwalimu kwenye jamii kushuka sana na mwalimu kuhesabika kuwa ni duni katika jamii. Lakini hii si kweli hata kidogo. Msichana akitaka kuchumbiwa na mwalimu anajisikia mnyonge, na mara nyingi hukataa labda akihisi kuwa umri unamtupa mkono au akiona hajapata chaguo la moyo wake.

Ukweli ni kwamba watumishi wote wa serikali (walimu na kada zingine) mishahara yao iko chini sana! Lakini ukiilinganisha hiyo mishahara yao midogo, mshahara wa mwalimu unakuwa juu kidogo kuliko kada zingine isipokuwa kwa kada ambazo wanasoma miaka mingi zaidi kama madaktari, wafamasia na wahandisi.

Ngoja niwaanikie hapa:

Mishahara ya walimu wanaoanza wenye digrii ya kwanza:
Hadi Juni 2022 walikuwa kwenye TGTS D1 = 716,000/=
Kuanzia Julai 2022 wanakuwa kwenye TGTS D1 = 771,000/=

Mishahara ya kada zingine wasio walimu wenye digrii ya kwanza:
Hadi June 2022 walikuwa kwenye TGS D1 = 710,000/=
Kuanzia Julai 2022 wanakuwa kwenye TGS D1 = 765,000/=

Kwa hiyo hadi Juni 2022 mshahara wa mwalimu ulikuwa unazidi mshahara wa kada nyingine kwa sh 6,000/=.
Kuanzia Julai 2022 mshahara waq mwalimu unazidi mshahara wa kada zingine kwa sh 6,000/= pia.

Kwa wastani mishahara ni midogo kwa wote japo jamii inaamini kuwa mwalimu ndiye mwenye mshahara mdogo wakati siyo kweli. Wahanga wa uongo huu wamekuwa ni wasichana kukataa kuolewa na walimu na kushobokea kada zingine kwa kigezo cha mshahara.

Mtumishi wa serikali akilalamika kuwa mshahara ni mdogo watu wanakimbilia kusema kuwa huyo lazima atakuwa ni mwalimu.

Nashauri tuwaheshimu sana walimu wetu, tusiwabeze bali tuwatie moyo maana kazi yao ni ngumu na ni muhimu sana. Kinachoendelea kwenye mitandao ya kijamii kwa sasa ni kukejeli walimu eti ndio wanaolalamikia nyongeza kiduchu ya mshahara mwaka huu kinyume na matarajio yao.

Mkuu mbona hiyo 771000 ni muuguzi ngazi ya Diploma
 
Walimu Hawana dili Wala marupurupu ya ziada Kama kada nyingine, hiki Ndo kinawafanya kua maskini Sana

1. Dreva wa halmashaur ana mshahara mdg kuliko mwalimu ila atapiga dili za vifusi,mchanga,kokoto n.k night za misafara n.k

2. Afisa biashara au ardhi wa halmashaur ana mshahara mdg kuliko mwalimu,
Ila atapiga rushwa za leseni za kufa mtu.

3. Afisa mifugo au kilimo atapiga elfu tano tano za sindano mifugo ya watu au atalima mashamba yake uko uchochoroni kwa kutumia dawa au pembejeo za ruzuku za serikali.

4. Mfamasia atakula laki tano tano kila mwezi for free za cheti chake tu kutumika kwny maduka ya dawa ya watu uko mitaani uku katulia tu..

5. Daktar au nesi wa halmashaur,
Hawa dili za semina,mafunzo n.k Ni nyingi mno(covid 19, chanjo, ukoma, malelia n.k). Hapo bado hawajaiba vifaa Tiba na kuviingiza mtaani kwenye hospital binafs.
[emoji117] Kuna na mabwana afya kaam matrafiki TU, wanatupiga Sana elfu hamsin hamsi Za faini uku mitaani

6. Wahasibu na maafisa manunuzi wa halmashaur wanapiga Sana dili za kimahesabu na 10% wakishirikiana na maboss wao (wakurugenz) ili Kupiga Cha juu kwenye tenda na matumiz mbalimbali ya fedha kwny halmashaur.

7. Maengineer wa halmashaur Ndo kabsaa wezi wakubwa, wao kila mradi wa serikali wakipewa kusimamia Lazima umalizike na yeye tayar ana kijumba keshakijenga kwa material zile zile za mradi.

8. Maafisa masjala wao Ni Kama matrafiki au madalali wa viunga vya halmashaur, una faili lako pale kwa mkurugenz au mkuu wa wilaya,ili likimbie chap chap Lazima utamwachia elfu 2 au elfu 5 ya maji.

9. Afisa maliasili wa halmashaur Hawa Ni wazee wa madili na rushwa za misitu,mikaa,mbao na magendo mbalimbali ya serikali.

10. Afisa utumiishi Hawa ndio wazee wa madili ya watumishi hewa.
[emoji117]Mtu anafariki, ripoti haiendi hazina kusitisha mshahara. Inatolewa ripoti ya mwajiriwa kubadili account yake, mshahara wa marahemu wanaula hata miaka 10 mfulurizo bila yeyote kujua.
[emoji117]mtu anamakosa ya kinidhamu,kasimamishiwa mshahara. Ripoti haiendi hazina, inabadilishwa tu account. Wanaupiga kimya kimya. Ukisamehewa ukarudishiwa mshahara, ule wa nyuma hata uulizii.
[emoji117]mtu anaripoti Ila haendi kituo Cha KAZI, au anaacha kazi anaenda zake private kwa muda.
wanakula dili na afisa utumishi, wanaugawana nusu nusu huku yeye Yuko zake private sector anapiga Ela nyingine.

Kama Kuna mtumish mwngne wa halmashaur nmemsahau nikumbushe.

Ila kiuhaisia mwalimu nje ya mshahara sijui atapiga dili gani atoboe,

ukiachilia mbali suala la twisheni ambalo bado kipato chenyewe Ni kidg mno na jasho linalomtoka Ni jingi mno

Sijui atapiga dili gan jingine maana vitabu vyote vya serikali vimeandikwa "HAKIUZWI", boksi lenyewe la chaki Mtaani halizidi hata elfu 2.
Hapo hatuna neno
 
Huu upuuzi sijui tutauacha lini? Kama mtumishi wa umma unayefahamu mfumo wetu wa ajira za serikali utagundua kuwa Mwalimu anatofautiana kidogo sana na watumishi wa kada zingine .

Hizi ni tofauti chache sana.

1. Posho. Mwalimu hana posho ila kada zingine wanazo

2.Mianya ya rushwa. Hakika mashuleni rushwa ni ngumu sana kupatikana labda kwa mkuu wa shule.

Hizi tofauti mbili ndizo zinazomfanya Mwalimu aonekane ana njaa sana hasa tarehe za katikati.

OMBI KWA WALIMU

Wawekeze zaidi katika professionalism na hii sababu ndiyo inayowaumiza sana. Walimu wengi ni Incompentent , unskilled not well developed. Hawawezi hata kujibu hoja tu za kiutumishi . Mfano ukiomba barua zilizoandikwa na walimu kwa mikono yao🤣🤣🤣 Aisee utacheka . Kujielezea ni sifurii.
 
Mkuu mbona hiyo 771000 ni muuguzi ngazi ya Diploma
Kada ya afya sijaiweka kwenye mlinganisho! UJue wanapiga kitabu miaka 4 hao wauguzi kwa diploma na wanaitwa STAFF NURSE. Hata hivyo hiyo data yako sijui kama ndiyo mshahara wa kuanzia!!
 
Back
Top Bottom