Mliokaririshwa uongo kuwa mishahara ya walimu ni midogo kuliko watumishi wengine wa serikali, nawaanikia hapa

Mliokaririshwa uongo kuwa mishahara ya walimu ni midogo kuliko watumishi wengine wa serikali, nawaanikia hapa

Hiyo basic yako mimi kwangu ndiyo allowance yangu, yani kwa mwezi sikosi at least 500k ya posho, na mm ni yule lowest rank staff.

Lakini kwenye haya maisha ya utumishi kupata pesa nyingi si kitu, kitu cha msingi ni jinsi gani unapangilia matumizi yako, sababu kuna wanaolipwa mamilioni wanastaafu bila hata kajumba, na wapo wanaolipwa vilaki kadhaa lakini wanafanya vitu vikubwa.
 
Katika ajira nadhani walimu ni watani wa kila mwajiriwa
IMG-20220116-WA0004.jpg
 
hii ni posho kwenye baadhi ya mashirika ya umma

sio ajabu mtu anawezalipwa posho kubwa kuliko mshahara.

mfano huyu polisi kama anafanya kazi nje ya kituo cha kazi posho inavuka huo mshahara.
 
Nina demu mwalim mnasemaje niendelee nae au nipige chini??
 
Ualimu sio kazi ngumu ya kumlipa hela nyingi, wanakula bata sana hawa...
Diploma kwetu wanalipa 1,000,000 dgree 1,355,000 hiyo ni basics...
Sasa degree ya mwl.ni 710,000/= take home bei gani kama hiyo ni basics..
Hawana kazi ngumu, kufundisha tu watoto na hawana side effects za kazi afu unataka hela nyingi
Ulitaka walipwe kiasi gani? Ingekuwa wewe ndo unapanga mishahara.
 
Walimu Hawana dili Wala marupurupu ya ziada Kama kada nyingine, hiki Ndo kinawafanya kua maskini Sana

1. Dreva wa halmashaur ana mshahara mdg kuliko mwalimu ila atapiga dili za vifusi,mchanga,kokoto n.k night za misafara n.k

2. Afisa biashara au ardhi wa halmashaur ana mshahara mdg kuliko mwalimu,
Ila atapiga rushwa za leseni za kufa mtu.

3. Afisa mifugo au kilimo atapiga elfu tano tano za sindano mifugo ya watu au atalima mashamba yake uko uchochoroni kwa kutumia dawa au pembejeo za ruzuku za serikali.

4. Mfamasia atakula laki tano tano kila mwezi for free za cheti chake tu kutumika kwny maduka ya dawa ya watu uko mitaani uku katulia tu..

5. Daktar au nesi wa halmashaur,
Hawa dili za semina,mafunzo n.k Ni nyingi mno(covid 19, chanjo, ukoma, malelia n.k). Hapo bado hawajaiba vifaa Tiba na kuviingiza mtaani kwenye hospital binafs.
[emoji117] Kuna na mabwana afya kaam matrafiki TU, wanatupiga Sana elfu hamsin hamsi Za faini uku mitaani

6. Wahasibu na maafisa manunuzi wa halmashaur wanapiga Sana dili za kimahesabu na 10% wakishirikiana na maboss wao (wakurugenz) ili Kupiga Cha juu kwenye tenda na matumiz mbalimbali ya fedha kwny halmashaur.

7. Maengineer wa halmashaur Ndo kabsaa wezi wakubwa, wao kila mradi wa serikali wakipewa kusimamia Lazima umalizike na yeye tayar ana kijumba keshakijenga kwa material zile zile za mradi.

8. Maafisa masjala wao Ni Kama matrafiki au madalali wa viunga vya halmashaur, una faili lako pale kwa mkurugenz au mkuu wa wilaya,ili likimbie chap chap Lazima utamwachia elfu 2 au elfu 5 ya maji.

9. Afisa maliasili wa halmashaur Hawa Ni wazee wa madili na rushwa za misitu,mikaa,mbao na magendo mbalimbali ya serikali.

10. Afisa utumiishi Hawa ndio wazee wa madili ya watumishi hewa.
[emoji117]Mtu anafariki, ripoti haiendi hazina kusitisha mshahara. Inatolewa ripoti ya mwajiriwa kubadili account yake, mshahara wa marahemu wanaula hata miaka 10 mfulurizo bila yeyote kujua.
[emoji117]mtu anamakosa ya kinidhamu,kasimamishiwa mshahara. Ripoti haiendi hazina, inabadilishwa tu account. Wanaupiga kimya kimya. Ukisamehewa ukarudishiwa mshahara, ule wa nyuma hata uulizii.
[emoji117]mtu anaripoti Ila haendi kituo Cha KAZI, au anaacha kazi anaenda zake private kwa muda.
wanakula dili na afisa utumishi, wanaugawana nusu nusu huku yeye Yuko zake private sector anapiga Ela nyingine.

Kama Kuna mtumish mwngne wa halmashaur nmemsahau nikumbushe.

Ila kiuhaisia mwalimu nje ya mshahara sijui atapiga dili gani atoboe,

ukiachilia mbali suala la twisheni ambalo bado kipato chenyewe Ni kidg mno na jasho linalomtoka Ni jingi mno

Sijui atapiga dili gan jingine maana vitabu vyote vya serikali vimeandikwa "HAKIUZWI", boksi lenyewe la chaki Mtaani halizidi hata elfu 2.
hahahahhahahahahahahah we jamaa umechambua kila angle, any way umeupiga mwingi
 
TUNAOMBA MISHAHARA YA WALIMU WENYE MASTERS Degree IANGALIWE UPYA IKIWEZEKANA NAJUA KUNA WAHUSIKA HUMU🙏🏼🙏🏼
 
TUNAOMBA MISHAHARA YA WALIMU WENYE MASTERS Degree IANGALIWE UPYA IKIWEZEKANA NAJUA KUNA WAHUSIKA HUMU🙏🏼🙏🏼
Masters haitambuliki kwenye mifumo ya utendaji isipokuwa baadhi ya Kada tu
 
Masters haitambuliki kwenye mifumo ya utendaji isipokuwa baadhi ya Kada tu
Tuiombe serikali Kama kuna uwezekano iwasaidie walimu wenye masters haya mambo yanawezekana kabisa
 
Sasa huo ni wizi!! Ni mtu mjinga peke yake anayeweza kufurahia kipato cha wizi na cha udanganyifu kisicho halali!! Fikiria msichana anayemkubali mtu anayeonekana ana kipato kikubwa lakini kumbe chanzo chake ni wizi, halafu ni kweli mtupu kuwa siku za mwizi ni arobaini! Kuna siku atakamatwa na kufukuzwa kazi na kifungo juu!! Walimu wana maisha mazuri, wanajua kulea watoto wao vizuri na wana maadili sana!! Inasikitisha watanzania kujivunia kazi kwa kuwa ina "fursa" za wizi na udanganyifu!!
Mkuu wanajipa moyo skuizi kama wasemavyo PESA HALALI NI YA SERIKALI TU ZINGINEZO SIO HALALI PITA NAZO TU..wizi hautaisha
 
HATA WAKIONGEZEWA DARAJA MOJA LA MSHAHARA Mara baada ya kumaliza masomo yao, kuliko kuwaacha bila chochote Kama ilivyo Sasa. TUNAOMBA wenye mamlaka waliangalie hili swala. Kwa walimu WENYE MASTERS Degree
 
-tunaongeza madaraja wenye CPA
 
Sasa huo ni wizi!! Ni mtu mjinga peke yake anayeweza kufurahia kipato cha wizi na cha udanganyifu kisicho halali!! Fikiria msichana anayemkubali mtu anayeonekana ana kipato kikubwa lakini kumbe chanzo chake ni wizi, halafu ni kweli mtupu kuwa siku za mwizi ni arobaini! Kuna siku atakamatwa na kufukuzwa kazi na kifungo juu!! Walimu wana maisha mazuri, wanajua kulea watoto wao vizuri na wana maadili sana!! Inasikitisha watanzania kujivunia kazi kwa kuwa ina "fursa" za wizi na udanganyifu!!

Kama wewe ni mwizi basi usisahau kuwa ipo siku utafukuzwa Kazi.
Hivyo ishi kama Kazi itaisha kesho yaani WEKEZA.

#YNWA
 
Back
Top Bottom