Mlioko kwenye ndoa naomba ushauri hasa wanawake: Nilifumaniwa na mtoto wangu wa kiume

Mlioko kwenye ndoa naomba ushauri hasa wanawake: Nilifumaniwa na mtoto wangu wa kiume

Upo kwenye hard time inabidi uipokee tu,tubu tu kwa Mola wako inatosha huwezi mlazimisha afute Hilo tukio mawazoni mwake
 
Maoni na comment kwenye mada hii ni kipimo tosha cha utakatifu kwa wengi!
Hizo dhambi zinazo semekena zimezidi kwenye jamii mbona hazilingani na maoni ya wengi?
Si wanasema mdomo hunena yaliyo moyoni, mbona kwenye mada hii utakatifu wa wadau ni mkubwa sana.
 
Mzazi kakosea sehemu za biashara unaleta nuksi.
Mungu uleta tukio kupitia Hilo tukio uache Tabia Fulani
Wadau wapo humu na huu uzi wameusoma haya matukio wanayajua mabwana wa mama zao wameishia waita uncle uncle ila wanajua siyo uncle ila hawawambiii baba zao maana mama zao wakorofi wanaishia kuumia kimya kimya
 
Tatizo una malezi ya kumdekeza dekeza ndio maana unambembeleza bembeleza uku kwetu uswahilini mama anafumaniwa na watoto, mama anaomba radhi watoto watoto wakijifanya wajuaji mama anawaita anawambia hivi nyie mnakili kweli mnakili baba yenu sasa hawezi nitia nguvu ndogo haya mtanitia nyie nauliza mtanitia nyie tena unambiwa makavu ole wenu nisikie kwa baba yenu miye si ndio nimewazaa mtajua miye nani mama uyo anaondoka watoto mnapouwa wote mnaanza kuwaza kumbe baba apigi show
Sure, ishu hapa ni kumbembeleza na kumpetipeti mtoto kama mume!
Mtoto wa kumzaa amuweke kihoro kiasi hicho mzazi!
Kwanza huyu dogo hajawa mwanaume bado.
 
Sure, ishu hapa ni kumbembeleza na kumpetipeti mtoto kama mume!
Mtoto wa kumzaa amuweke kihoro kiasi hicho mzazi!
Kwanza huyu dogo hajawa mwanaume bado.

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
Siye hao tunawambia tuwaite uncle full stop, na michepuko ya baba tunaita anti unabaki unaumia tu rohoni ila mama na baba basi tu
 
Habari za jioni.

Mimi ni mama mtu mzima nina watoto 4 kwa mume wangu wa ndoa kabisa.

Niende kwenye mada.

Miaka 10 iliyopita nilifumaniwa na mtoto wangu wa kiume(my first born). Sikuamini kilichotokea nilishituka sana kwa hile tukio lilotokea.

Mimi nafanya kazi kwenye wizara moja hivi nipo hapa dsm mpaka sasa. Miaka iliyopita niliingia mahusiano na Baba mmoja hivi anafanya kazi wizara nyingine tofauti na yetu nilikutananae kwenye kikao vya ofisini.

Mimi ni kawaida yangu kumcheat mume wangu, japo hajawahi kunitilia hofu kama nimewahi kumcheat maana mara nyingi navizia akiwa safarini ndo ninafanya hivyo. Maana ninajua kumcheta mwanaume ni hatari sana kwani wanaume wanawivu sana na hasira, kama mume wangu namfahamu ni mtu mwenye hasira sana , so nilijitahidi asijue kabisa.

Sasa kuna siku mimi nilienda kwenye duka langu maana kwenye duka langu kabla jioni ijafika lazima niwepo ndo nifunge na wafanyakazi waondoke pale. Sasa kipindi tunamaliza yule Baba alinipigia simu nikamwambia nipo sehemu falani , nikamuelekeza akafika na alipofika wafanya kazi wangu nao wakawa wanaondoka mda huo huo. Mimi nikamkaribisha mchepuka ndani , sasa kwenye duka kuna ofisi kwa ndani si nikaenda nae mapaka kwenye ofisi katika kuongea kama 20 minutes, kwa sababu ni mchepuka tukajisahau akaanza kunishika na kuanza kukiss each other katika kunishikashika nikajisahau.

Kumbe mtoto wangu wa kwanza alikuja pale dukani aliingia baada ya kuona mlango wa flemu moja ujarudishiwa mpaka chini kabisa so akajua kuna mtu ndani. Aliingia moja kwa moja mpaka ofisini kwenye ndani ya duka, na mlango wa ofisi sikufunga , nilishituka sana mpaka kumtuja (mmiliki wa vyote) ile siku nilitetemeka pale pale , isitoshe mapaja yangu yote yalikuwa nje , japo nashukuru hatukufika ile stage ya kusexy.

Nilitetemeka sana na moyo kwenda mbio kwani yule ni mtoto wangu wa kumzaa. Alituangalia afu akaondoka, mchepuko akaniulize yule ni nani nikamwambia mwanangu, yeye mwenyewe alishituka. Akanishahauri kuwa tulia tuu tuongee tuyamalize nikamwambia subiri niende home kwani namjua atakuwa anaenda home. Akili iliruka siku ile. Nikafunga duka.

Nilikimbilia nyumbani ili kumuwahi mtoto maana Baba yake alikuwa Bagamoyo anarudi kesho , nilifikili ataenda kupiga simu ya nyumbani na kumwambia mume wangu, nilipofika home nilimkuta hajafika bado nilimsubiri alilofika. Nilimuita nje nikaongea nae sana. Nikajua yameisha. Kesho yake nikamwambia unataka nini nikununulie akasema hataki chochote .

Yule Baba akanipigia simu tukaongea sana akaniambia njoo uchukue pesa tumpe mtoto atajamaza tuu , yule Baba alinila 1,000,000 nimpe mtoto wangu niliasiseme nilimpa zile pesa nikajua yameisha.

Sasa kadri siku zinazidi kwenda mtoto wangu alikuwa aninichukia sana kuna kipindi alikuwa hata kunisalimia hataki kabisa. Nikimtuma hataki kabisa hata kwenda. Ila mimi niliewa kuwa ni lile tukio. Kuna siku alinisikia namuita mume wangu kipenzi, kijana wangu si akasikia aliniangalia sana. Mpaka mimi nikashituka, na nikajua yeye jinsi anavyo jisikia.

Kuna kipindi nililazwa hakuja hata kuniangali hospital. Mara nyingi tukiwa pekeetu nakuwa nakaa nae naongea nae namwambia mimi ni mama yako naomba unisahame nimemkosea Baba yako, nimeacha sijarudia tena. Ila hanijibu chochote ananyamaza tuu. Najitahidi kumfanyia mambo mazuri ilimradi nirudishe mahusiano na mtoto wangu. Lakini inashidikana. Kuna siku namwambia unapenda nikufanyia nini mwanangu hanasema tuu mimi nipo sawa mama. Tangu lile tukio niliacha kucheat.

Ki ukweli ananichukia sana mimi mama yake uwa nakaa ne mara nyingi naongea nae ila inashindikiana.
Mwaka juzi nilimuona kuna rafiki yake anagari , na mimi nikasema ngoja nimnunulia kagari mtoto wangu , kwa vile mimi nimeajiriwa na nina mshahara mzuri, nilijikusanya na kuchukua pesa baadhi kwenye biashara zetu na mume wangu, mwaka jana mwezi wa 8 nikaenda mlimani pale nikanunua gari , nikamfanyia kama surprise hivi alisema tuu Asante akachukua.

Ila nilishangaa aliendesha kama 2 weeks baadae alilirudisha nyumbani na kuweka funguo mezani ajariendesha mpaka leo, mume aliniuliza gari vipi nikazuga zuga tu. Nilishangaa sana nilimuuliza kuwa unajua mimi ni mama yako nimekosa ila kumbuka mimi ni mama yako. Yeye sasa anaumri wa miaka 26.

Sasa wiki 2 zilizopita mume wangu aliniambia kuwa ninaona wewe na first born hamna mahusiano mazuri nawafatilia mda mrefu sana sijajua shida ni nini. Nimeshituka sana kwani sitaki mume wangu hajue hii ishu japo ilitokea 10 years ago ila baada ya kujiambia hivyo niliishiwa nguvu kabisa. Juzi nilijaribu kumuuita mtoto wangu niongee nae lakini still bado anahasira nami.

SASA JAMANI Naomba msaada wenu kimawazo nideal vipi na hii kesi. Najua hawezi kumwambia Baba yake ila na mimi nikikaa kinywa , mume wangu atajua tuu **** something tunamficha maana hata juzi katoka kusema shida yenu ni nini nimemrukaruka tu. Mtoto wangu hataki kabisa kunisikiliza.

Nilitaka kushirikisha kiongozi wa dini mmoja ni mwanamke, tumuite ili tuongee nae ila naona haitakuwa siri tena inatavuja tu.

Msaada wa mawazo Nahitaji.

Lipa tu gharama, mwite mumeo, na ukiri, uanaume alionao mumeo ndio anao mwanao, anaona Baba yake kazulumiwa. Sasa ngoja mtoto amwambie, itakuwa ngumu sana
 
Najua hilo kuna kipindi nilipuuza tuu. Ila si unajua yule ni mtoto wangu, sasa mahusiano naye yamekufa kabisa kwa sasa.

Nawaza sana sijui ananionaje mimi mama yake.

Anakuona Malaya, na wewe ni Malaya, na mchepuko ni mshenzy, ni watu wa aina gani mna tamaa kama ngurumwe au tu mbuzi? Mnalete balaa kwenye biashara!
 
Wadau wapo humu na huu uzi wameusoma haya matukio wanayajua mabwana wa mama zao wameishia waita uncle uncle ila wanajua siyo uncle ila hawawambiii baba zao maana mama zao wakorofi wanaishia kuumia kimya kimya
Wanawaharibu kisaikolojia watoto wao,zipo kesi za kina uncle kuuliwa na watoto wa michepuko Yao kwa kuwaletea dharau kisa wanawapanda mama zao.
Pana mpumbavu alionywa na watoto anawadhalilisha kuja kumpanda mama Yao Tena ndani ya nyumba Yao mpumbavu hakusikia Leo yupo kaburini.
Maandiko yanaposema ikimbieni zimaa waliona haya
 
Wanawake mliko kwenye ndoa ni laana kuu kumcheat mume wako, sbb hamsikii, sasa mkija kung'olewa meno kwa koleo na kutobolewa macho na kisu, msije lete kelele, utulie kimya, juzi Arusha mwanamke kapasuliwa kisa kumcheat mume wake, nyie viume wanawake, mko ktk ndoa, unatafuta nn kwa mwanaume nje ya ndoa yako.

Mwanamke aliye katika ndoa ni laana kuu ku cheat, wewe subiri mume wako atajua, ndio utapata ulichokitafuta.
 
Huyu ni mwanaume ni Mwanaume hivi karibuni amefungua ID mpya 2 na za zamani anazo 2. Mpuuzi tu anataka watu waanze mfuatilia uchunguzi bado unaendelea kujua kama anataka
1. Awe anabakwa na wanaume
2. Anataka awatapeli

bado vijana wangu wanamfanyia kazi ndani ya masaa 24 wataleta report kamili. Ila apuuzwe tu.
Asante kwa muhtasari kaka. Tunasubiria ripoti kamili.

Uongo umekithiri humu siku hizi
 
Daa hii kitu kinanikumbusha issue ya rafiki yangu mmoja wa church.
Daaa wao kwao wapo 4.

Sasa mama yao kipindi kapata ujauzito wa nne mpaka kujifungua.
Baba yao ni mtu wa kusafiri sana.
Sasa dogo kipindi anakuwa mtoto wake wa kwanza wa kiume akaanza kumfananisha na mzee wa kanisa. Kadri anavyokuwa yule mtoto kweli alifanana na mzee wa kanisa , Baba yao hakushituka .
Ila mtoto wa kwanza wa kiume alishituka.
Daaa mwishowe alishidwa kuvumilia si akamwambia Baba yake, kuwa huyu mdogo wetu mimi namfananisha na mzee wa kanisa.
Baba yake kuangalia vizuri akaona kweli kabisa.

Mwishowe ndoa ilivunjika maana mkewe alizaa nje.

Mama sisi wanaume tunawivu sana, sawa na mwanaume akioa single mother mwenye mtoto wa kiume , huyo mtoto ni ngumu kumpemda step father maana anaona kama unamla mama yake. Hasa baba yake mzazi akiwa hai , atakuchukia tuu.
Pole mama. Ngoja waje watu wazima watakushauri.
Kanisa tena!!!! [emoji2297] [emoji2297]
 
Huyo mtoto mwambie kuwa yule alokukuta naye ndo mdingi wake.
 
usaliti, usaliti, usaliti
Hekima za suleiman
"Mwanamke mwenye hekima huijenga nyumba yake Bali mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe"
 
Na Mimi nimeishtukia. Maana kuna point Uzi ni kama ume-terminate
Huyu ni mwanaume anaandika hivyo ili aonekane ni mwanamke anayeweza kumcheat mumewe watu waanze kumfuata inbox awatapeli. Mwanamke hawezi jisifia kua anamcheat mumewe alafu anajieleza sana ili tuamini stori ila hapo biashara inatangazwa ushoga haujifichi kabisa
 
Kinachomuumiza dogo ni kuwa baba yake ni responsible father. Anahudumia kila kitu na anajali welfare ya familia pamoja na kumuonesha mama yao highest degree of love and affection.

Laiti kama baba angekuwa hajali familia na irresponsible haoneshi upendo kwa mama na watoto hapo dogo asingemaindi kabisa. Tena angeona mama amefanya vile kama kutafta relief tu of which ingekuwa valid kulingana na uwajibikaji wa baba kwa familia.
Tatizo kubwa dago hawezi kujua kama baba anamridhisha mama.
Na ndio maana mama katoka nje ya ndoa.
 
Back
Top Bottom