BilioneaPATIGOO
JF-Expert Member
- Jun 23, 2012
- 12,320
- 11,327
Mkuu asante kwa ujumbe wako ..umeongea kitu cha kweliNimeisoma hii habari nimekumbuka mbali sana.Pole sana Mama...Tunaamini kwa umri huo wa miaka 07 na 10 bila shaka watakuwa na kumbukumbu ya mbali juu ya taswira ya Wazazi wao.
Kuna uhusiano mkubwa sana kati ya "Upendo" wa Wazazi na "Uono"(Sight).Ndio maana wazungu walisema "Out of Sight,Out of Mind".
Hata kama leo watakutana,lakini hakutakuwa na ile "bondism" ya Mama na Watoto,sbb kile kipindi cha kutengeneza hiyo bondism kilishapita.
Hii kwa wale wafuatiliaji wa mpira watakuwa wameiona kwa Mario Baloteli,wazazi wake walimpa Mzee Baloteli raia wa Italia kumlea Mario akiwa bado mtoto mdogo sana,kiasi Mario ana upendo wa kweli kwa baba wa kufikia kuliko kwa "Biological Parents" wake.
Miaka kadhaa iliyopita niliwahi kukutana na jamaa aliyelelewa na Watawa wa Kikatoliki huko Dodoma,baada ya Wazazi wake kuwa na umasikini kiasi alikuwa na utapiamlo,alikuja kuwaona Wazazi akiwa na miaka 20.Siku alipokufa mmoja wa Wazazi wake,hakulia kama alivyolia na kugalagala kama siku aliyokufa Mtawa aliyemlea.
Tumuombee Mama Kichawele awapate watoto wake,tuombe wawe wazima...Na sisi tukumbuke kujinyima na kufanya lolote kwa ajili ya kuwekeza kwa watoto...Hujawahi kwenda kwenye msiba wa mzazi wa mwenzako na ukakuta jamaa ana-behave kama aliyefariki ni jirani na si mzazi??Ni kwa sbb wakati wa umri wa "bondism",ile bond haikushimana vilivyo.
ndio mana binafs nilianzisha thread inayohusu mzazi kuweka bond na mwanawe tangu akiwa tumboni
wachache wameelewa ila wengine ndo ile kutupa lulu kwenye zizi la nguruwe.
Lakin nimekupata sawia.
Tuna imani mama atawaona wanawe japo wajue their mother is alive japo hio bond and love inaweza kua shida kidogo, ni mda mrefu sana na zaid hatujui huko kwa miaka 20+ walikua wanaambiwa nini