Mlioko Uingereza, msaidieni huyu mama kufahamu wanawe walipo

Mlioko Uingereza, msaidieni huyu mama kufahamu wanawe walipo

mama naye??? miaka 22 bila mawasiliano na wanawe???
Hili pia linashangaza sana Mkuu,

Hawa watoto walichukuliwa miaka 22 iliyopita,mmoja wao akiwa na umri wa miaka 7 na mwingine miaka 10, hii ina maana umri wa hawa watoto kwa sasa hivi,mmoja ana umri wa miaka 29 na mwingine 32,

So,hawa sio watoto wadogo tena bali ni watu wazima na kwa kawaida ya maisha ya Europe,watoto wengi wakifika umriwa kuanzia miaka 18 huanza kujitegemea, kwahiyo hawa "watoto" si ajabu wameshakua na miji/familia zao tayari,

Nikutakie kila la kheri mama wa watoto na Mungu akufanyie wepesi kuwapata wanao na kuonana nao tena.
 
pole zake, kwanini alikubali watoto waondoke,kwanini asingesaidiwa ada wasome wakiwa kwake kama shida ni uwezo.mmmh

Kuna harufu ya CHILD TRAFFICING BUSINESS.Huyo mama anatakiwa kuhojiwa vizuri.Kuna wazazi huzaa na kuuza watoto nje ya nchi kwa kushirikiana na mawakala wa biashara hizo.Kuna kilichojificha.Huyo msomali walikuwa na ukaribu upi hadi wamkabidhi watoto wadogo kama hao kama hawakumwuuzia? Waanzie kwa huyo mama halafu wafuatilie kwa huyo msomali.Waweza kuwa mtandao wa CHILD TRAFFICKING
 
Kwa mtazamo wangu, kama unawapenda watoto wako na unawajibika kwao kwa 100% kamwe huwezi kumkabidhi mtu akulelee watoto, na ukifanya hivyo ni njia mojawapo ya kukwepa majukumu na kutafuta urahisi wa maisha. Pamoja na kuwa tunamhurumia huyu mama kwa kutenganishwa na watoto wake lakini hata kwa upande wake kuna uzembe wa hali ya juu ambao ameufanya na kinachotokea muda huu ni malipo ya huo uzembe, nimejaribu ku google na kwenye facebook haya majina sijayaona.
 
Lefu = refu

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
Wengine Kiswahili ni Lugha ya pili baada ya lugha zetu Mama.
Hii ni lugha tuliyojifunzia shuleni na tuliporudi nyumbani tuliendelea na lugha Mama.
Moja ya athari ya lugha ya pili,ni kuchanganya na lugha mama katika maandishi na matamshi.

Wataalamu wote wa lugha hujua jinsi ilivyo rahisi kwa mtu aliyeathirika na lugha Mama kuchanganya herufi na matamshi na lugha ya kujifunza,ndio maana hata kesho ukimwambia Magufuli aseme "Ng'ombe" atasema "Ngombe",Lugha Mama yake haina Ng'

Ukienda Nyanda za juu kusini hawana "Nt" bali "nd"...ndio maana hutamka "Intelligend" badala ya "intelligent"

Unaweza kukosoa/kusahihisha bila kuhusisha na shule,maana sio wote walioenda shule kusomea lugha tu.
 
Wewe ni mke wa marehemu Abbas wa Bondeni Arusha....????
Huyo Msomali Mahmood kwao ni Ngarnaro .....???
Nauliza hivyo ili nasi tuanze kukusaidia kupitia ndugu na jamaa wa Mahmood
Hebu msaidieni kama mnaweza, nadhani hao ndugu wa huyo Abbas wanaweza kufahamu suala hilo na endapo itaonekana hawataki kutoa ushirikiano basi suala hilo lifikishwe polisi na kuunganisha suala hilo kwenye upelelezi wa interpool kwa kushirikiana na ubalozi wa uingereza nchini Tanzania. Huwezi sema watoto wako Uingereza kwa sababu tu walipelekwa huko kusoma wala hakuna ajuaye wako katika hali gani sasa zaidi ya huyo msomali, kwahiyo suala hili linapaswa kushuhulikiwa kwa haraka zaidi wakati huyo msomali akiwa bado yu hai.[/QUOTE]
 
Kuna harufu ya CHILD TRAFFICING BUSINESS.Huyo mama anatakiwa kuhojiwa vizuri.Kuna wazazi huzaa na kuuza watoto nje ya nchi kwa kushirikiana na mawakala wa biashara hizo.Kuna kilichojificha.Huyo msomali walikuwa na ukaribu upi hadi wamkabidhi watoto wadogo kama hao kama hawakumwuuzia? Waanzie kwa huyo mama halafu wafuatilie kwa huyo msomali.Waweza kuwa mtandao wa CHILD TRAFFICKING
miaka 22 duh
 
Mkuu "bond" inaanzia tumboni,unaweza kutenga kila siku asubuhi uamkapo,na jioni ulalapo ukawa unashika tumbo la Mama na kumwambia mtoto maneno ya heri,ukimwambia kuwa unamsubiri kwa hamu aje,unamfurahia kama zawadi na huku ukimsisitiza akuombee heri upate riziki ya kuja kumtunza vyema.

Siku akizaliwa,angali mchanga,unachukua faragha naye na kuongea naye kuwa wewe ni mzazi wake,unamtakia maisha mema ktk dunia,unamtakia heri na afya ili akikua akukute na uone utu uzima wake.Yaani unamsemesha kama vile ni mtu mzima.Hii inakuwa ni "Spiritual Bonding"....Sababu ni mawasiliano ya kiroho kati ya wewe na mtoto.

Baadaye ndani ya miaka 02-06 unaanza kujenga taswira yako ktk ubongo wa mtoto,ndio pale anaanza kukuita baba bila yeye kujua alianzaje kukuita baba.

Miaka 06 -16 ndio haswaa "physical bond" inaimalika.Hapa mtoto anaona kama ni Mama basi anaona ule Umama wako,kama ni baba basi anaona ule ubaba wako,ana-feel ile protection,akipigwa na wenzake anatoka mbio anakuja kusema baba nimepigwa na huyu,kama ni kwa Mama basi anaenda kusema Mama hapa panawasha nikune.

Hii ya Baba nimepigwa inakuja kwako sbb anaanza kujifunza "sense of protectionism" hutoka kwa baba,anasema Mama hapa nimeumia au hapa panawasha,sbb tayari amejifunz kuwa "sense of Sympathy(?) and Care" hutoka kwa Mama.

Ndio maana unaona ukitaka pesa ya kununulia vibama unaenda kwa Mama,lakini hela ya daftari au kalamu unamwambia Baba.Hapo ubongo wa mtoto umekuwa na kujua nani ni nani...,

Ni somo lefu sana...,Ambalo sisi tuliozaliwa na Wazee wa 1920's hatukulipata sana,ila sisi tunapaswa kuwapa upendo huu watoto wetu,iwe wa kike au kiume.


Barikiwa sana Mkuu barafu. Huwa najifunza mengi kutoka kwako. Ahsante

-Kaveli-
 
sikilizeni huyu jamaa inawezekana wamekubaliana na baba yao mtoto, kuwa awafanye kama wanawe,
na hivyo wanafanya watu wengi sana tuu, sio kwenda ubalozini ndio solution. Inawezekana majina yao wamebadilishwa wana majina mengine kabisa na ikawa vigumu zaidi kuwapata.
ni kuchukua muda kwanza kutoa hili tangazo na liingizwe kwenye facebook na media nyengine kabla ya kwenda ubalozini.
maana watoto wenyewe inawezekana wakamkataa mzazi wao ni kuomba Mungu tuu, wawe watoto wazuri na wenye kufikiria.
Uingereza sio Africa hâta wabadilishe Majina n'a Mahali pa kuishi watapatikana tu labda wawe wamehama nchi n'a nchi waliyoenda iwe Africa hasa Somalia. Cha msingi ni tuombe wawe hai, nakubaliana n'a suluhisho ulilotoa la kwenda ubalozini. Wenzetu wanauwezo mkubwa kufuatilia watu wao hasa kutumia anuani za makazi na ukihama ukurupuki tu lazima ubadilishe kwenye mfumo Mzima hasa police.
Naamini atawapata watoto wake kama wapo Uingereza tena wala sio kwa kutumia Nguyu nyingi hivyo.
 
Watoto Box limewakolea Hadi Bi mdashi wamemsahau,..
Cc. RRONDO
Kama waliondoka na miaka 7-10 miaka 22-iliopita ukiwaona sasa hivi hutaweza kuwatofautisha na Waingereza weusi kuanzia accent,mavazi,utamaduni.

Kama waliwekea msingi mzuri watakuwa sehemu nzuri.
 
Kama waliondoka na miaka 7-10 miaka 22-iliopita ukiwaona sasa hivi hutaweza kuwatofautisha na Waingereza weusi kuanzia accent,mavazi,utamaduni.

Kama waliwekea msingi mzuri watakuwa sehemu nzuri.
Wangekuwa wapo Marekani Huenda wangekumbuka kwao japo kwa kipindi hiki
 
Wizara ya mambo ya ndani ipo, Tanzania ina ubalozi Uingereza kwa sasa chini ya Dr. Asha-Rose Migiro si ufuate tu taratibu. Kwanza kuwafahamu hao watoto kwa sasa ni ngumu kwa kutumia hizo picha kwani watakuwa wamekua sana. Na labda wameisha hamia kwingine.
 
Wangekuwa wapo Marekani Huenda wangekumbuka kwao japo kwa kipindi hiki
Hao waliondoka wadogo ni wazi wamepoteza connection na mzazi wao na wako more connected na mlezi wao.

Kama ana jina na address za aliewachukua atawapata, ila unaweza kukuta hao watoto wana IDs mpya.
 
Hii habari ya huyu mama ina ukakasi mwingi, na hapa watu wanahukumu kwa maelezo ya upande mmoja tu huyu mama. Katika ndoa kuna mambo mengi sana.. mmoja sio mtoto wake wa kumzaa ni wa ndg wa mume na huyo mwingine ndio wake.! Inawezekana kabisa huyu mama alimkana huyo mtt sio wake akamzilia marehemu mume wake nae alipozidiwa na majukumu ndio kafanya yake na msomali.! Mama mwenye mapenzi ya dhati kwa mtoto wake huwezi muacha 22 years ndio ujitokeze huyu mama kanusa harufu ya pesa tu huu usawa wa JPM watu wanatafuta fursa.. Haiwezekani huyo mume hana ndg wa kifatilia pia. Ninahisi huyu mama alimkimbia mumewe na mtoto na ndo haya yakatokea. Hebu tusome na upande wa piili wa sarafu kuna mengi yamejificha kwenye hii story ya huyu mama ambayo hata huo ubalozi mnaomshauri aende watamuuliza wazungu hawafanyi kazi kiswahili: Tahadhari pia akawekwa chini ya ulinzi kwa child trafficking maana mumewe ni marehemu na yy ndio atwajibishwa.
 
Back
Top Bottom