Mlioko Uingereza, msaidieni huyu mama kufahamu wanawe walipo

Mlioko Uingereza, msaidieni huyu mama kufahamu wanawe walipo

Nimeisoma hii habari nimekumbuka mbali sana.Pole sana Mama...Tunaamini kwa umri huo wa miaka 07 na 10 bila shaka watakuwa na kumbukumbu ya mbali juu ya taswira ya Wazazi wao.

Kuna uhusiano mkubwa sana kati ya "Upendo" wa Wazazi na "Uono"(Sight).Ndio maana wazungu walisema "Out of Sight,Out of Mind".

Hata kama leo watakutana,lakini hakutakuwa na ile "bondism" ya Mama na Watoto,sbb kile kipindi cha kutengeneza hiyo bondism kilishapita.

Hii kwa wale wafuatiliaji wa mpira watakuwa wameiona kwa Mario Baloteli,wazazi wake walimpa Mzee Baloteli raia wa Italia kumlea Mario akiwa bado mtoto mdogo sana,kiasi Mario ana upendo wa kweli kwa baba wa kufikia kuliko kwa "Biological Parents" wake.

Miaka kadhaa iliyopita niliwahi kukutana na jamaa aliyelelewa na Watawa wa Kikatoliki huko Dodoma,baada ya Wazazi wake kuwa na umasikini kiasi alikuwa na utapiamlo,alikuja kuwaona Wazazi akiwa na miaka 20.Siku alipokufa mmoja wa Wazazi wake,hakulia kama alivyolia na kugalagala kama siku aliyokufa Mtawa aliyemlea.

Tumuombee Mama Kichawele awapate watoto wake,tuombe wawe wazima...Na sisi tukumbuke kujinyima na kufanya lolote kwa ajili ya kuwekeza kwa watoto...Hujawahi kwenda kwenye msiba wa mzazi wa mwenzako na ukakuta jamaa ana-behave kama aliyefariki ni jirani na si mzazi??Ni kwa sbb wakati wa umri wa "bondism",ile bond haikushimana vilivyo.
Uko sahihi mkuu ila lengo la wazazi lilikuwa kuwapatia fursa ya masomo, kilichotokea bahati mbaya.
Tunaomba msaada wako kuwakutanisha watoto na mzazi wao.
 
Ningekuwa sijaelewa nisingesahihisha.

Cheo cha utakatifu kwetu hakuna hicho. Huo utakatifu hata wanaolawitiana wanapewa huko kanisani, unabisha nikuwekee ushahidi?

Tatizo lako ni shule, ulisomea ujinga.
UNAKERA..
 
Hii habari imenikumbusha mbali sana.
Mwaka 2001 kuna mama mmoja mjerumani alitaka kunichukua kwa dhamira ya kunisomesha kutokana na kuona kuwa mama ana mzigo mzito wa kutulea watoto watano, kwa kweli mama alikataa,akamuomba kama ana dhamira ya kunisomesha basi anisomeshe huku huku bongo.

Mungu ampe maisha marefu mama yangu.
 
Pole mama kwa Hali unalopitia tumwombe Mungu watoto wawe salama , hakika tunapaswa kujitahidi kujinyima na kulea watoto Wetu katika Hali yoyote tunayopitia haijalishi kipato wala Hali zetu kumpa MTU watoto ni risk kubwa sana na tunapoteza nafasi ya kujenga upendo
Ni kweli mie wangu nitakufa nao hata ikibidi kulala njaa si kila anaemchukua mtoto huwa ana nia njema.
 
Bac na.yy alikaa kimyaaaa miaka yote hiyo mmh hata km alikuwa na moyo mgumu manake mumewake hakuchelewa alifariki bac angeanza utaratibu Wa kuuliza kipindi hicho angekwisha wapata kwa jinsi waingereza wanavyojali watoto
Lkn sense ubalozi Wa uingereza na a mini atafanikiwa
 
Nimeisoma hii habari nimekumbuka mbali sana.Pole sana Mama...Tunaamini kwa umri huo wa miaka 07 na 10 bila shaka watakuwa na kumbukumbu ya mbali juu ya taswira ya Wazazi wao.

Kuna uhusiano mkubwa sana kati ya "Upendo" wa Wazazi na "Uono"(Sight).Ndio maana wazungu walisema "Out of Sight,Out of Mind".

Hata kama leo watakutana,lakini hakutakuwa na ile "bondism" ya Mama na Watoto,sbb kile kipindi cha kutengeneza hiyo bondism kilishapita.

Hii kwa wale wafuatiliaji wa mpira watakuwa wameiona kwa Mario Baloteli,wazazi wake walimpa Mzee Baloteli raia wa Italia kumlea Mario akiwa bado mtoto mdogo sana,kiasi Mario ana upendo wa kweli kwa baba wa kufikia kuliko kwa "Biological Parents" wake.

Miaka kadhaa iliyopita niliwahi kukutana na jamaa aliyelelewa na Watawa wa Kikatoliki huko Dodoma,baada ya Wazazi wake kuwa na umasikini kiasi alikuwa na utapiamlo,alikuja kuwaona Wazazi akiwa na miaka 20.Siku alipokufa mmoja wa Wazazi wake,hakulia kama alivyolia na kugalagala kama siku aliyokufa Mtawa aliyemlea.

Tumuombee Mama Kichawele awapate watoto wake,tuombe wawe wazima...Na sisi tukumbuke kujinyima na kufanya lolote kwa ajili ya kuwekeza kwa watoto...Hujawahi kwenda kwenye msiba wa mzazi wa mwenzako na ukakuta jamaa ana-behave kama aliyefariki ni jirani na si mzazi??Ni kwa sbb wakati wa umri wa "bondism",ile bond haikushimana vilivyo.
Well put mkuu
 
MSAADA TUTANI: OMBI LA KUWASILIANA NA WATOTO WALIOPO UINGEREZA KWA ZAIDI YA MIAKA 22 SASA.

87a7dba21b625a50ae6f47a140659a2c.jpg

Picha za awali za wahusika wa waraka huu ikiwa ni pamoja na watoto Amina na Seleman Kichawela na Bw. Mahmud Hassan Mihile aliyewachukua miaka 22 iliyopita ili kuwasaidia masomo huko Uingereza.

Kutokana na kichwa cha habari hapo juu mimi AZAMA ABBASI KICHAWELE ambae kwa sasa ni mjane, mwenye namba ya simu +255 784 697319 na mkazi wa Majengo Arusha, Tanzania, na ambae ni mama wa nyumbani, nachukua nafasi hii kukutaarifu kama ifuatavyo.

Mume wangu kwa majina ABBASI ALLY KICHAWELE ambaye kwa sasa ni marehemu alikua na rafiki wake wa karibu kwa majina MAHMUD HASSAN MIHILE aliekuwa akitumia namba ya simu +441332270462 wakati huo mwenye asili ya Kisomali na uraia wa Uingereza na Tanzania walikubaliana awachukue watoto wetu ambao ni: SELEMAN ABBASI KICHAWELE aliekuwa na umri wa miaka kumi na AMINA JABIRI KICHAWELE aliekuwa na umri wa miaka saba aende nao Uingereza kwa ajili ya kuwasomesha.

Siku ya kuondoka watoto hawa ilikuwa ni mwaka 1994 na waliondoka na mke wa huyo Msomali kwa majina RAHMA MIHILE. Mji wa kwanza walioshukia huko UINGEREZA unaitwa LEICESTER. Baada ya hapo mawasiliano yaliendelea kuwepo kati ya mzazi wa kiume wa watoto na Msomali.

NB: Katika hawa watoto huyu wa kike, Amina Jabiri alikuwa ni wa mdogo wake mume wangu yaani shemeji yangu.

Kwa bahati mbaya mume wangu, aliugua maradhi ya cancer na ilipofika mwaka 1998, nikampoteza (alitangulia mbele ya haki).

Baada ya kifo cha mume wangu hakukua na mawasiliano yoyote kati yangu na huyu bwana aliyechukua watoto wangu. Alikata mawasiliano kabisa na wala hakutaka watoto wajue kuwa baba yao hayupo tena Duniani.

Kwa bahati mbaya sikua na mtu mwingine mbadala wa kuweza kuniunganisha na huyu bwana ikizingatiwa pia mimi ni mama wa nyumbani sikuwa na PR kubwa. Leo hii ninapoandika barua hii, huu ni mwaka wa ishirini na mbili (22) toka nitengane na watoto wangu. Sisi pamoja na wanafamilia tutaendelea kutoa shukrani zetu kwa serikali ya Uingereza iwapo watoto hawa wapo salama na kwenye ajira zao. Kwetu hilo sio tatizo.

Jambo kubwa linaloniumiza ni kutokua na MAWASILIANO na watoto wangu kwa miaka ishirini na mbili sasa. Wakati mwingine najenga wasiwasi kwamba je, wako hai? Na hali hii nitaendelea nayo mpaka lini?
Huyu bwana Mahamudu (msomali) nini kimemsukuma kuwa na ujasiri wa kuwaficha watoto wangu hata nisiwe na mawasiliano nao? Ana dhamira gain?

Kutokana na maelezo mafupi hapo juu nimefikia hatua ya kuiomba ofisi yako tukufu kunisaidia kupata namna ya kuwasiliana na watoto wangu wapendwa huko waliko. Jambo hili likifanikiwa litaleta faraja sana kwangu na kwa wana familia kwa ujumla.

Pia itakuwa ni fursa kwa watoto kutambua kuwa baba yao mpendwa alishafariki lakini mimi mama yao bado nipo hai, taarifa ambazo tuna hakika hawajazipata. Naambatanisha picha za watoto ambazo walipigwa wakati wanakaribia kuondoka mwaka 1994.

Pia naambatinisha na picha ya Mahmud Hassan Mihile (Msomali) ya wakati huo aliyewachukua watoto kwa makubaliano na mume wangu.

NB: Kwa mawasiliano tumia namba hizi za barua pepe
hasatathuman@gmail.com
Au Athuman Rashid Mfinanga
Box 2614, - Arusha Tanzania
Ph: 0754375602/0784375602

Wako,
Katika ujenzi wa Taifa
Azama Abbasi Kichawele

Chanzo: Michuzi blog
hajawatoa kafara kweli? kutoa mtoto wako akaishi kwa mwingine yataka moyo.
 
Pole mamaa.... ila huyo mshomali fal.a sana...ndio maana napenda kuangalia ile movie ya captain Phillips walivyopewa noma mbaya.. I hope nawewe ukiitazama itakufariji
 
M
Hii habari ya huyu mama ina ukakasi mwingi, na hapa watu wanahukumu kwa maelezo ya upande mmoja tu huyu mama. Katika ndoa kuna mambo mengi sana.. mmoja sio mtoto wake wa kumzaa ni wa ndg wa mume na huyo mwingine ndio wake.! Inawezekana kabisa huyu mama alimkana huyo mtt sio wake akamzilia marehemu mume wake nae alipozidiwa na majukumu ndio kafanya yake na msomali.! Mama mwenye mapenzi ya dhati kwa mtoto wake huwezi muacha 22 years ndio ujitokeze huyu mama kanusa harufu ya pesa tu huu usawa wa JPM watu wanatafuta fursa.. Haiwezekani huyo mume hana ndg wa kifatilia pia. Ninahisi huyu mama alimkimbia mumewe na mtoto na ndo haya yakatokea. Hebu tusome na upande wa piili wa sarafu kuna mengi yamejificha kwenye hii story ya huyu mama ambayo hata huo ubalozi mnaomshauri aende watamuuliza wazungu hawafanyi kazi kiswahili: Tahadhari pia akawekwa chini ya ulinzi kwa child trafficking maana mumewe ni marehemu na yy ndio atwajibishwa.
Maneno mengi utafkiri malenga,sumtime ukimuongelea mzazi wa mtu uwe na adabu.
 
Back
Top Bottom