Mliokuwa 'mkimdhihaki ' Rais Dr. Magufuli juu ya Ununuaji wa Ndege Kubwa pateni mfano huu Kuntu wa Kenya

Kwa hili na mengine mengi anayoyafanya naunga mkono kwa % kubwa

Tatizo wengi sio kuwa hawataki maendeleo bali ni ubishi wa kupinga kila kitu
 
umesikika ila tuheshimu tu sheria na mihimili mingine
 
Mkuu GENTAMYCINE hongera kwa uzi na ninakupongeza sana kwa utetezi wako kwa JPM. Naheshimu michango yako kwani huwa sio mnafiki na huwa unanyoosha bila kupindisha hata Mavunde hilo analijua.

Tuje kwenye mada yako, nionavyo kuna upotoshaji wa wazi kwenye wanaomkosoa JPM kwa kuwekwa kwenye kundi la kumpinga japo sio kosa hata akipingwa, upotoshaji huu unafanyika kwa makusudi ama pasipo au kwa kufuata mkumbo. Tuko sisi tuliosema na tutaendea kusema na kukosoa bila kuyumbayumba kwani tunachosimamia tunakiamini. Tulisema ndege ni jambo jema, lakini kwa hali za walio wengi hapa nchini ambao ni wakulima ni vyema kipaombele kingekuwa kwenye kilimo. Mimi ama wanaoamini kwamba kilimo kilipsawa kuwa kipaombele kisha ndege baadae, ni kwamba tungeleta maendeleo ya watu kwanza, kisha maendeleo ya vitu. Iwapo ingetokea kwamba tuliokosoa kununua ndege kwanza tungeenda kuilipua hapo sawa, lakini tumetumia haki yetu ya kukosoa na kusema kipi kilipaswa kuwa kipaombele kosa letu liko wapi?

Inaonekana ww na mashabiki wake na hata yeye mwenyewe mnakwepa hoja zetu za ukosoaji kwa kichaka cha kupingwa, na hamtumii neno ukosoaji bali huwa mnasema kumpinga rais ili mpate public sympathy. Na kwa bahati nzuri hilo neno ya kwamba rais anapingwa kwa kila jambo linaenea vizuri bila wananchi kupata upande wa pili maana sasa hivi kinachosikika kwenye media ni atakacho rais. Huku kwenye mitandao pakee ndio kumebaki na mijadala huru kama hivi. Msipotoshe japo mna haki ya kumtetea mpendavyo na sisi tuna haki ya kumkosoa tupendavyo kwani ndio demokrasia as long as hakuna anayekwenda kuharibu hiyo miundo mbinu.
 
Hayo ni matokeo mazuri ya ziara yake kule kwa Trump,hayo hayawezekani ikiwa tumejifungia tu ndani.Ushirikishwaji muhimu pia
 
Mkuu kwanza kabisa rekebisha,yey sio zawadi tena iliyotoka kwa Mungu,atakuwa katokea upande mwingine ila ni mahaba yako kwake,binafsi nasikitika sana kuwa chini ya hu utawala.
 
Kichaa jiwe alichaguliwa na majambazi ya ccm ila Mungu ameamua kumuacha tu kwa maana Mungu ni pendo apenda wote.
 
we mbweha nimekuuliza kiistarabu kutokana na maelezo yako kwenye mada, soma ulichoandika kwenye mada na maelezo uliyatoa baadae
 
Hatuna jins sasa zaidi ya kuunga mkono Juhundi za awamu ya Tano
Kuunga mkono juhudi ni pamoja na kuiga matendo yake ambayo watu "wanaamini" ni mazuri. hakika kama Watanzania wote wangeunga mkono "juhudi zake" basi yale mazishi ya Ukara asingekuwepo mtu hata mmoja mana wote wangukuwa wanakunywa chai na waalikwa wao walio waita majumbani.
 
Kazi kununua wapinzani? Alaa kumbe wapo sokoni wanajiuza hao wapinzani ! Kama mahangu vile au ?
 
Sema kunitukana , sio kututukana ! Sawa bwege ?
 
Sheria ingefuatwa ndo tungefaidika nini? sanasana hadi hivi leo tungekuwa tunaambiwa stori za "michakato inaendelea"....
Go JPM Gooo!
Maadam unachofanya kinaonekana na wananchi tunakiappreciate waachie hao wanaotaka sheria waendelee kuzisubiri.
Achana nao hao , sheria sheria mbona mbowe kala hela za sabodo sheria haijafuatwa ?
 
Jinyonge sasa ndo kashanunua
 
Hujatuambia Kenyatta kafanya nini kwenye bandiko lako
The problem is, you jump to comments section without going through what is written. Learn to be keen. It will help you not to expose such damning weakness on your part.
 
Kwa mujibu wa Rais Kenyatta amesema
Amesema Amesema..
Inapendeza tuchukue mifano kwa mambo yaliyotokea siyo kwa yanayotarajiwa kutokea, ikipatikana faida ndiyo tunaweza Kumsifu Jiwe..
Wanasiasa kazi yao ni Kusema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…