Mliokuwa 'mkimdhihaki ' Rais Dr. Magufuli juu ya Ununuaji wa Ndege Kubwa pateni mfano huu Kuntu wa Kenya

Kabla ya hii ajali mbona hujasema kama vivuko ni kipaombele. Kama ingeanguka precision air ungesema serikali imepatia kununua ndege au usingesema. Acha kwenda na matukio, na pia fich ujinga wako sometimes
 
Hahah. Na dio maana nikamwambia ajaribu kificha ujinga wake. Yaani sijapata ona jamaa mjinga jf kama huyu.
 
Tatzo sio ndege bali ni sheria ya manunuzi, bunge lilihusishwa mkuu?
Je, ingepitishwa bungeni, mngefanikiwa kuizuia isinunuliwe kama mlivyozoea? Mbona kila Bunge linapohusishwa, mnakimbilia hapa oohhh imepitishwa kwa kuwa Wabunge wa CCM ni wengi, sijui ooohh Bunge ni rubber stamp ya Serikali, hivyo tu yaani, dah!!
 
Hivi haujaona kuwa hapa juzi Korea wamepewa tenda ya kuunda meli ziwa Victoria , Ziwa Nyasa meli zimeundwa Tatu haujaona au unajifanya hujui na Songoro Marine wanakarabati meli za ziwa victoria au wewe hujui jamani sio kila kitu kubisha mara nyingine tuwe wakweli raisn anatutendea yaliyo mema .Pia mjifunze kufuatilia masuala badala ya kuweka uongo na kuwapotezea watu muda na kama unabisha basi bisha kwa fact badala ya kuleta porojo huku mitandaoni.
 
Hivi unajua vigezo vinavyotakiwa kupeleka ndege na kufanya Biashara hiyo USA? sisi hata IATa matatizo
 
[Q UOTE="GENTAMYCINE, post: 28515288, member: 156632"]Kuna muda huwa nawashangaa sana kama siyo mno Watanzania kwamba ni kwanini hawataki Kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuwapa ' Zawadi ' ya Rais ambaye ana ' maono ' makubwa sana ya Kimaendeleo kama aliyonayo Rais wetu Mpendwa Dr. John Pombe Joseph Magufuli a.k.a Mwanamume wa Shoka.

Kwa wale Ndugu zangu ambao mmekuwa mkipiga Kelele juu ya Ununuaji wake wa Ndege ili kuweza kuzidisha Kasi ya Utalii nchini nadhani kwa hili alilolifanya Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta sasa mtakuwa na la Kujifunza na ikibidi bado hamjachelewa kumuomba radhi Mheshimiwa Rais JPM au Kutengua ' Kauli ' zenu kwani kiukweli Rais JPM yupo sahihi kwa 100% na hizi Ndege anazozinunua zitaongeza mno Ukuaji wa Uchumi na hasa Sekta nzima ya Utalii kwa nchi ya Tanzania.

Ni kwamba Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amezindua rasmi Safari ya Ndege ya moja kwa moja kutoka Nairobi ( Kenya ) hadi New York ( Marekani / USA ) ambayo itaanza rasmi tarehe 29, October 2018 na mpaka hivi sasa tayari Watu 7000 wameshakata ' Tiketi ' zao ili kuwemo katika hiyo Safari ya Kwanza.

Kwa mujibu wa Rais Kenyatta amesema kwamba uzinduzi huu wa hii Safari ya moja kwa moja kati ya Kenya na Marekani ( USA ) kutaongeza maradufu ' mapato ' katika Sekta nzima ya Utalii ya nchini Kenya na pia Uchumi wa nchi yake utakuwa kwa haraka kwakuwa Kenya imekuwa na ' Vivutio ' vingi ambavyo Wamarekani wengi hupenda kuvitembelea mara kwa mara.

Bado nitasema na leo nasema tena bila ' Unafiki ' kwamba kama kuna ' Zawadi ' ambayo Mwenyezi Mungu ametupa Watanzania basi ni kwa kutupatia Rais mwenye maono ya kweli, yenye tija na uhakika wa Kimaendeleo kwa nchi hii Rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli a.k.a Mwanamume wa Shoka.

Hakuna Rais ninayempenda na kumkubali kama JPM na Mwenyezi Mungu ambariki sana azidi kutuletea Maendeleo Watanzania.

Source: Daily Monitor

Nawasilisha.[/QUOTE]
KQ ni mwanachama wa IATA, KQ, wako kwenye alliance na mashirika kama KLM, Air Tanzania in safari ndefu sana
 
Swala la serikali kumiliki ndege kwangu mimi naona kuna changamoto kubwa sana kutokana na ushindani mkubwa kutoka kwa sekta binafsi.
Ni bora kufikiria namna nyingine ya kukuza sekta ya utalii bila kuingia gharama kubwa za ndege.
 
Kipi bora, kuwa na natioal carrier halafu nchi ipate hasara kila mwaka au hizo hela za kununulia ndege zielekezwe kwenye miradi itakayonufaisha wananchi wote.
Mwambie huyo mkuu kajaa mahaba ya kijinga kabisa.
 
Hebu basi twende kwa logic. Mimi binafsi naamini siyo tatizo kwa Tanzania kuwa na shirika imara la ndege. tatizo langu ni njia ambazo Rais wetu ametumia katika kuliinua shirika la ndege. Natambua kwamba njia mbalimbali za uchumi zinategemeana. kuna vipaumbele ambavyo tunatakiwa kuanza navyo, ili twende sawa. Unapofikia hatua ya kukuza shirika la ndege, angalau kuna sekta zitategemea uwepo wa ndege, ambazo nazo ziko imara. Ukiangalia Kenya ambao wanatuzidi mara nyingi sana katika mifumo ya utalii, kuanzia utangazaji, connection za tour operators, uwepo wa watalii wengi tayari, na miundo mbinu iliyoimarika, wana uhakika wa safari za moja kwa moja zitalipa. ukiangalia sisi Tanzania, tuko nyuma mno katika kujitangaza, maana yake fungu tunaloweza kutenga kwa ajili hiyo ni dogo sana. sioni kwa vipi tunaweza kuiga Kenya moja kwa moja kama anavyotaka kutuaminisha mleta uzi.
 
Wakenya wanapinga sana ununuzi wa ndege. Wanalalamika wanasema hiyo hela ingepelekwa kwenye vitu vingine na vile tz ni maskini.
hawajakubaliana na suala la tz kununua ndege.
ni Bora Ange nunua vivuko nchi mzima kwanza watu wameuwawa wetu bado wako kwenye siasa
 
Zai zaid tunahijaji vipa umbele vielewke km ni kufunga mikanda tujue siyo kufunga mikanda bila Tahadhali 'If you do not know where you are going any road will take you there'
 

Aisee

Kuna any correlation kati ya kununua Bombardia za hapo Bongo na safari za ndege za KQ kutoka Nairobi kwenda NYC USA?

Halafu watu wote wanaotetea serikali "sikivu" ya CCM kuna vitu vyao binafsi hua wanaficha...
 

..sisi tuliweza kukuza utalii wetu bila kuhitaji shirika la ndege.

..mashirika ya ndege ya nchi majirani zetu ama yamekufa, au yanaendeshwa kwa HASARA.

..ATCL ni hasara ya kujitakia tu. Shirika hilo ni KUPE anayekuja kunyonya kodi za masikini wa Tz.
 
Wakenya wanapinga sana ununuzi wa ndege. Wanalalamika wanasema hiyo hela ingepelekwa kwenye vitu vingine na vile tz ni maskini.
hawajakubaliana na suala la tz kununua ndege.
Makunya uwivu umewajaa mpaka....,...
Majanga yameanza kuwakumba sasa wanaisoma number milele walahi
 
Umeamdika totally upupu walahi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…