Mliokuwa 'mkimdhihaki ' Rais Dr. Magufuli juu ya Ununuaji wa Ndege Kubwa pateni mfano huu Kuntu wa Kenya

WaTZ wengi vichwa maji.....wengine hata uzi hawajausoma mpk mwisho wanaponda tuuu
 
Wewe huwa ni bwege siku zote,tangu lini mnyarwanda akawa na akili? Eti mnajivunia Kagame kajitu kapumbavu kanakoipeleka Rwanda kumwaga Damu.
Kenya ina uchumi mkubwa mara tatu ya Tanzania, hakuna aliyempinga Magufuli kununua ndege ,tunachopinga ni kwamba ndege haikuwa kipaumbele kwa sasa,Hujiulizi kwa nini ajali za maji Africa ,Tanzania inaongoza?MV Bukoba watu 1500 walikufa,Spicer island watu 500,MV Nyerere watu 210.
Halafu unanunua ndege inayopandwa na watu 30 tu wenye uwezo kiuchumi ,Kenya ina mizizi ya utalii Tanzania tupo nyuma mno,Rais asiyependa exposure na mataifa makubwa Tanzania itatoa wapi watalii? Kazi kuharibu pesa kwa kununua wapinzani na kurudia uchaguzi,akili za hovyo kabisa hizi.
Hizo pesa za ndege zingenunua meli maisha ya watanzania yangekuwa salama.
Wewe ni bwege uliyetukuka.[/QUOTE
Hoja makini sana,ccm sijui akili zao zikoje!!!
Kazi yao kusifia hata iwe mbaya kiasi gani watasifia tu.
 
Kuna muda huwa nawashangaa sana kama siyo mno Watanzania kwamba ni kwanini hawataki Kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuwapa ' Zawadi ' ya Rais ambaye ana ' maono ' makubwa sana ya Kimaendeleo kama aliyonayo Rais wetu Mpendwa Dr. John Pombe Joseph Magufuli a.k.a Mwanamume wa Shoka.

Kwa wale Ndugu zangu ambao mmekuwa mkipiga Kelele juu ya Ununuaji wake wa Ndege ili kuweza kuzidisha Kasi ya Utalii nchini nadhani kwa hili alilolifanya Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta sasa mtakuwa na la Kujifunza na ikibidi bado hamjachelewa kumuomba radhi Mheshimiwa Rais JPM au Kutengua ' Kauli ' zenu kwani kiukweli Rais JPM yupo sahihi kwa 100% na hizi Ndege anazozinunua zitaongeza mno Ukuaji wa Uchumi na hasa Sekta nzima ya Utalii kwa nchi ya Tanzania.

Ni kwamba Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amezindua rasmi Safari ya Ndege ya moja kwa moja kutoka Nairobi ( Kenya ) hadi New York ( Marekani / USA ) ambayo itaanza rasmi tarehe 29, October 2018 na mpaka hivi sasa tayari Watu 7000 wameshakata ' Tiketi ' zao ili kuwemo katika hiyo Safari ya Kwanza.

Kwa mujibu wa Rais Kenyatta amesema kwamba uzinduzi huu wa hii Safari ya moja kwa moja kati ya Kenya na Marekani ( USA ) kutaongeza maradufu ' mapato ' katika Sekta nzima ya Utalii ya nchini Kenya na pia Uchumi wa nchi yake utakuwa kwa haraka kwakuwa Kenya imekuwa na ' Vivutio ' vingi ambavyo Wamarekani wengi hupenda kuvitembelea mara kwa mara.

Bado nitasema na leo nasema tena bila ' Unafiki ' kwamba kama kuna ' Zawadi ' ambayo Mwenyezi Mungu ametupa Watanzania basi ni kwa kutupatia Rais mwenye maono ya kweli, yenye tija na uhakika wa Kimaendeleo kwa nchi hii Rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli a.k.a Mwanamume wa Shoka.

Hakuna Rais ninayempenda na kumkubali kama JPM na Mwenyezi Mungu ambariki sana azidi kutuletea Maendeleo Watanzania.

Source: Daily Monitor

Nawasilisha.

""Ni kwamba Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amezindua rasmi Safari ya Ndege ya moja kwa moja kutoka Nairobi ( Kenya ) hadi New York ( Marekani / USA ) ambayo itaanza rasmi tarehe 29, October 2018 na mpaka hivi sasa tayari Watu 7000 wameshakata ' Tiketi ' zao ili kuwemo katika hiyo Safari ya Kwanza. ""
Umesahau kutueleza mchakato wa kuomba kuruhusiwa kuruka moja kwa moja kutoka Kenya to USA ulianza lini, umechukua muda gani na kenya ilibidi watimize nini.
 
Tatzo sio ndege bali ni sheria ya manunuzi, bunge lilihusishwa mkuu?
Mkuu afadhali umemjibu huyu kenge maji!Ila wale wanowakamata wachochezi mbona wana ubaguzi?huyu angefa kukamatwa na kuhojiwa ni wapi watanzania wamepinga kununuliwa kwa ndege?Watu walihoji mchakato mzima wa ununuzi wa hizo ndege haukuwa shirikishi kwa vyombo husika ili nao watoe ushauri wao n.k!
 
Kuna muda huwa nawashangaa sana kama siyo mno Watanzania kwamba ni kwanini hawataki Kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuwapa ' Zawadi ' ya Rais ambaye ana ' maono ' makubwa sana ya Kimaendeleo kama aliyonayo Rais wetu Mpendwa Dr. John Pombe Joseph Magufuli a.k.a Mwanamume wa Shoka.

Kwa wale Ndugu zangu ambao mmekuwa mkipiga Kelele juu ya Ununuaji wake wa Ndege ili kuweza kuzidisha Kasi ya Utalii nchini nadhani kwa hili alilolifanya Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta sasa mtakuwa na la Kujifunza na ikibidi bado hamjachelewa kumuomba radhi Mheshimiwa Rais JPM au Kutengua ' Kauli ' zenu kwani kiukweli Rais JPM yupo sahihi kwa 100% na hizi Ndege anazozinunua zitaongeza mno Ukuaji wa Uchumi na hasa Sekta nzima ya Utalii kwa nchi ya Tanzania.

Ni kwamba Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amezindua rasmi Safari ya Ndege ya moja kwa moja kutoka Nairobi ( Kenya ) hadi New York ( Marekani / USA ) ambayo itaanza rasmi tarehe 29, October 2018 na mpaka hivi sasa tayari Watu 7000 wameshakata ' Tiketi ' zao ili kuwemo katika hiyo Safari ya Kwanza.

Kwa mujibu wa Rais Kenyatta amesema kwamba uzinduzi huu wa hii Safari ya moja kwa moja kati ya Kenya na Marekani ( USA ) kutaongeza maradufu ' mapato ' katika Sekta nzima ya Utalii ya nchini Kenya na pia Uchumi wa nchi yake utakuwa kwa haraka kwakuwa Kenya imekuwa na ' Vivutio ' vingi ambavyo Wamarekani wengi hupenda kuvitembelea mara kwa mara.

Bado nitasema na leo nasema tena bila ' Unafiki ' kwamba kama kuna ' Zawadi ' ambayo Mwenyezi Mungu ametupa Watanzania basi ni kwa kutupatia Rais mwenye maono ya kweli, yenye tija na uhakika wa Kimaendeleo kwa nchi hii Rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli a.k.a Mwanamume wa Shoka.

Hakuna Rais ninayempenda na kumkubali kama JPM na Mwenyezi Mungu ambariki sana azidi kutuletea Maendeleo Watanzania.

Source: Daily Monitor

Nawasilisha.
Ndege na kukua kwa utalii vinauhusiano upi? Naomba nieleweshwe, ndege inakuzaje utalii kwa mfano. (NB mjinga akieleweshwa upevuka)
 
Tatzo sio ndege bali ni sheria ya manunuzi, bunge lilihusishwa mkuu?

We bunge hilo la miaka kenda haijakuwa na idea ya kufufua shirika la ndege, leo kaja JPM unaanza litaka bunge cjui lifanye nn na ndilo liloshindwa miaka yote kufufua hilo shirika...Watanzania tumelogwa na nanii[emoji22][emoji22][emoji22]...pathetic...JPM endelea kuinua Tanzania
 
For me kununua ndege na kutoweza kuongeza salary kwa wafanyakaxi was serikali kwa miaka 3 is bullshit
 
Fafanua kwa undani Kenyatta kafanyaje mkuu
Mkuu soma bandiko lore utaekewa,usisome kwa miemko.
Kasema rais Kenyatta kazindua safari za ndege moja kwa moja kutoka Nairobi mpaka new York marikani.
Kutokana na kitendo hicho watalii watakaozuru Kenya wataongezaka maradufu,na kukuza sects ya utalii ya Kenya na uchumi wa nchi hiyo kwa ujumla.
 
Birds of a feather fly together...ndege wafananao huruka pamoja. Toka nizaliwe sijawahi kumuona, kumsikia wala kumshuhudia kichaa akimshambulia kichaa mwenzake. Vichaa hushambulia wasio vichaa na hali hii imedhihirishwa na inazidi kudhihirishwa hadi humu JF. Vichaa lazima watamtetea kichaa mwenzao, hawashambuliani...hii ni tahadhari tu kwa wana Jamiiforums!
 
Kipengere gani kiliko kiukwa mzee??
Tenda ilitangazwa lini na wapi?Sheria ya manunuzi ya Umma inataka kutangazwa kwa zabuni katika gazeti la serikali!
Kwa namna ya ununuzi wa JPM,ni rahisi kwa yeye kula 10% ili kuwapa tenda kampuni husika!
 
So wao wanenda USA sisi tunaenda INDIA.
wewe huoni Tofauti?
Hivi kwa sasa ATCL ni mwanachama wa IATA? Je bado tunalitegemea shirika la HAHN watusaidie kuuza tiketi zetu za ndege? Hapo ndipo tunapotofautiana na nchi kama ya Kenya, wananunua ndege wakijua wataitumiaje. Ni ukichaa kununua mswaki kama huna meno!
 
Kweli hapa ninaona tofauti kubwa kweli kweli, wenzetu wananunua ndege na kufanya safari za moja kwa moja kati ya Nairobi na New York, sisi tunanunua ndege na kufanya safari za moja kwa moja kati ya Dar na mwanza, na pia Dar na Kilimanjaro. Dah! Sina cha kusema zaidi.
 
Kuna muda huwa nawashangaa sana kama siyo mno Watanzania kwamba ni kwanini hawataki Kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuwapa ' Zawadi ' ya Rais ambaye ana ' maono ' makubwa sana ya Kimaendeleo kama aliyonayo Rais wetu Mpendwa Dr. John Pombe Joseph Magufuli a.k.a Mwanamume wa Shoka.

Kwa wale Ndugu zangu ambao mmekuwa mkipiga Kelele juu ya Ununuaji wake wa Ndege ili kuweza kuzidisha Kasi ya Utalii nchini nadhani kwa hili alilolifanya Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta sasa mtakuwa na la Kujifunza na ikibidi bado hamjachelewa kumuomba radhi Mheshimiwa Rais JPM au Kutengua ' Kauli ' zenu kwani kiukweli Rais JPM yupo sahihi kwa 100% na hizi Ndege anazozinunua zitaongeza mno Ukuaji wa Uchumi na hasa Sekta nzima ya Utalii kwa nchi ya Tanzania.

Ni kwamba Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amezindua rasmi Safari ya Ndege ya moja kwa moja kutoka Nairobi ( Kenya ) hadi New York ( Marekani / USA ) ambayo itaanza rasmi tarehe 29, October 2018 na mpaka hivi sasa tayari Watu 7000 wameshakata ' Tiketi ' zao ili kuwemo katika hiyo Safari ya Kwanza.

Kwa mujibu wa Rais Kenyatta amesema kwamba uzinduzi huu wa hii Safari ya moja kwa moja kati ya Kenya na Marekani ( USA ) kutaongeza maradufu ' mapato ' katika Sekta nzima ya Utalii ya nchini Kenya na pia Uchumi wa nchi yake utakuwa kwa haraka kwakuwa Kenya imekuwa na ' Vivutio ' vingi ambavyo Wamarekani wengi hupenda kuvitembelea mara kwa mara.

Bado nitasema na leo nasema tena bila ' Unafiki ' kwamba kama kuna ' Zawadi ' ambayo Mwenyezi Mungu ametupa Watanzania basi ni kwa kutupatia Rais mwenye maono ya kweli, yenye tija na uhakika wa Kimaendeleo kwa nchi hii Rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli a.k.a Mwanamume wa Shoka.

Hakuna Rais ninayempenda na kumkubali kama JPM na Mwenyezi Mungu ambariki sana azidi kutuletea Maendeleo Watanzania.

Source: Daily Monitor

Nawasilisha.
Watu 7000 wajiandikisha au wamekata ticket kuwemo kwenye safari hiyo ya kwanza? Yaani Kenya hata wangerusha dreamliner zote nane kwenda JFK bado haziwezi beba watu 7000 Kwa safari moja
 
Back
Top Bottom