Mliooa, hii hali mnaichukuliaje kwa Wanawake?

Mliooa, hii hali mnaichukuliaje kwa Wanawake?

Wanawake msitukane wanaume kwa upumbavu wa wavulana!
 
Habari za wakati huu,

Nipo safarini kwa muda mrefu kidogo, niko mbali na wife.

Huyu mke wangu naona sasa anataka kunikera[emoji16], yaani kila muda sms-simu, sms-simu dah

Nampigia tunaongea saana, tunapiga stori sana, lakini kila baada ya muda kidogo huyoo kabeep! Nikipiga hana jipya lolote anaanza kujing'atang'ata tu!

Siku moja nilimpa makavu[emoji4][emoji4] akatulia kidogo ila alinitumia meseji ya kulaumu ananituhumu kwamba labda niko na mwingine anaetumia nafasi yake, bla bla nyingi! mpaka nikamwonea huruma ikabdi nibembeleze mmhh!

Huyu sio kwamba ndoa ndoa ni changa, niko nae kitambo tu lakini hili kuna wakati linanikera!

Hiki ni nini[emoji848]
Muwe na shukrani mkipata watu wa kuwapenda.
 
Habari za wakati huu,

Nipo safarini kwa muda mrefu kidogo, niko mbali na wife.

Huyu mke wangu naona sasa anataka kunikera[emoji16], yaani kila muda sms-simu, sms-simu dah

Nampigia tunaongea saana, tunapiga stori sana, lakini kila baada ya muda kidogo huyoo kabeep! Nikipiga hana jipya lolote anaanza kujing'atang'ata tu!

Siku moja nilimpa makavu[emoji4][emoji4] akatulia kidogo ila alinitumia meseji ya kulaumu ananituhumu kwamba labda niko na mwingine anaetumia nafasi yake, bla bla nyingi! mpaka nikamwonea huruma ikabdi nibembeleze mmhh!

Huyu sio kwamba ndoa ndoa ni changa, niko nae kitambo tu lakini hili kuna wakati linanikera!

Hiki ni nini[emoji848]
Daah usiridie tena hii mzee, wanawake wanapenda kupendwa, kudekezwa na kubembelezwa muda wote wakati wanaume tuhitaji kuaminiwa tuu hivo hatuhitaj pigiwa masim nk. Kwa tofaut hiyo ukiendelea mkazia mkewe atatafuta mahali furaha inapatikana.
 
Ukiisoma mada na comments zilizotumwa humu kwa upande wanawake na wanaume wengi wanafikiri kupigapiga simu na kusumbuana kama watoto ndio upendo, aisee. Kweli bado tunaongozwa na movies na series za kwenye TV. Unajua wewe ni mtu mzima na huyo mwanamke au mwanaume mmekutana ukubwani na kabla ya hapo kila mtu alikuwa anafanya mishe kusogeza maisha ya songembele. Kuwa mme au mke wa mtu sisababu ya kusahau kipi kilichokuwa kinaendesha maisha ilihali hiyo hisia ya kufanyiana huo ujinga itapita tu. Tujifunze kuwa costant na stable ndani ya misimamo ya maisha yetu kwawanaume na kwawanawake. We mwanaume jua unajenga familia kwakutekeleza majukumu yako na wemwanamke pia, kuanza kuleteana mambo ya wivu na tabia za ajabu ni utoto wakati ndoa imekuhakikishia huyo ni wakwako. Mwanaume unamshauri mwenzio aogope mwanamke atachepuka, hiyo ni matter of choice, mwanamke anayechepuka kwasababu za kijinga kama hivyo basi si mke wala mama mzuri kwa watoto, kwakuwa atatafuta upenyo mwingine wahivyohivyo kuchepuka. We mwanamke unayesema mkipendwa mpendeke unajua hiyo kupigapiga simu siishara ya upendo maana hata malaya hufanya hivyo kwa wateja wake. Angalia stability na maendeleo ya familia hayo mengine yakitokea ni mara moja maana nakuhakikishia akistaafu mtafanya hivyo vitu mpaka mchokane. Tuache kuiga tamthilia, let's just be adults not teens.
 
Wanawake msitukane wanaume kwa upumbavu wa wavulana!
Kwahiyo nawewe unataka kumtukana mwanaume mwenzako kuwa ni mvulana kwakuwa hajabadilika kukidhi mahitaji ya mwanamke. Surely basi ukibadilisha kukidhi mahitaji ya mwanamke basi ujue familia itabaki hapohapo. Kabla ya kuoana si alimjua yupo hivyo kwanini leo muane kufanyiana gene manipulation kuleta uhafifu wa jitihada kufikia malengo. Unajua tabia nyingi za kipumbavu zinamzomshusha hadhi na hata kumharibu asiwe mwanaume zimeletwa na mwanamke kutaka kumbadiisha mwanaume awe sawa na yeye. Utawatukana mashoga lakini unaujua mzizi kamili kuanzia huko chini ambapo mama aliachiwa majukumu ya kulea mtoto pekeyake na mwanaume kuangaika kama mwanamke kupata starehe ya kijinga huku jukumu lake kuu akiwa amelisahau. Mwanaume ndiyo humrudisha mwanamke kwenye mstari lakini leo hii mwanamke anafanya kazi ya kumridisha mwanaume kwenye mstari. Akimbebisha hiyo mke kila siku na akalemea kwenye kazi yake unajua mwanamke huyohuyo atamuona kama tambala hataambebishe vipi. Mwanaume huona miaka ijayo ila mwanamke huangalia kesho tu. Pia hivyo vitu uviteteavyo vinachosha sana tena sana, nasiuwanaume bali ni uvulana.
 
Hata wakudanga wanawapigia Simu nyingi wanaume na wapo kutaka pesa tu na wala si penzi la dhati ya moyo.
 
Ladies give your men space to vent.

Ewe Mwanamke mpe nafasi Mwanaume wako ya kupumua na kufanya mambo mengine maana naye ni kumbe huru.

La sivyo atakukinahi na kukukifu.
 
Mapenzi ni mazoea na namna mnavyojengana kimawasiliano na mwenzio.
Ni wazi mwanzo uliifurahia ila sasa inakukera kwasasabu kuku ushamtia kamba.
Ili usiharibu anachokifanya mkeo
1. Muanzishie mtindo mwingine wa mawasiliano kwa muda upendao, ila sio ghafla taratibu mpaka atazoea.
2. Mtafutie kitu cha kumfanya awe bize, mawasiliano yatakuwa ni ya kawaida sana.
3. Uishi naye kama mtu mzima, sms na call ni wajibu ila zipo zenye maudhui yasiochosha, muda usiochosha na usipotumiwa utazimis tu.
#imarika
#kupendwa raha mzee
 
Back
Top Bottom