Mliooa na mnaopata mshahara wa Tshs. 300,000 au chini ya hapo mnawezaje kumudu familia?

Yani mimi tu peke yangu bila family haitoshi kabisa,

Labda nipige dash asubuhi na mchana.

Hiyo 10,000 ni kama nauli na vocha tu.

Ila life liko tofauti sana aisee,kuna watu wanajua ku budget hiyo mtu hadi anasave kabisa.
 
Huu ushauri ni bora sana..

Wazee wengi huwa wanashuri sana hii kitu
 
Subiri waje wanaopataga hizo 300,000/= kwa.Ila pia wamejenga na wanatumia magari yao binafsi kuja ofisin na kila siku mafuta ya 15,000.pia mchana lunch yao si chini ya 10,000.Pia kila jioni wanasimamisha magari yao daily pale kipawa kununua samaki wabichi wa angalau 5,000-10,000 kwa ajili ya nyumbani usiku na matunda pale Goms ya 2,000 na zaidi.Pia pleadge zao za michango ya kila send off na harusi pia watoto wao pia wanasoma pale pale Tusiime,Heritage,Atlas ,canosa etc
 
Mkuu chukua daftari dogo au karatasi.... Andika mahitaji yako ya muhimu kwa mwezi mzima.... Pia andika matumizi yako inayotumia pindi unapoipata hiyo laki 3....hapo utaona kuna mambo yasiyo ya msingi huwa inafika pesa basi hayo uyapunguze mkuu....
 
Watu hawana mshahara kabisa.... MTU amekopa hadi salary slip inamdai na anaishi..

Kifupi unaishi Kwa taabu sana.

Hiyo laki tatu wadau hapo juu wanasema upunguze vitu visivyo vya lazima. Em wavitaje!?

Hela ndogo sana hiyo..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…