Mliooa na mnaopata mshahara wa Tshs. 300,000 au chini ya hapo mnawezaje kumudu familia?

Maisha wakati mwigine yanatufanya tuwe makatili we cha kufanya kwenye hiyo 3 mpe mkeo laki 2 kisha umuweke wazi kipato chako na umwelrze kuwa ni bajeti ya chakula mwezi mzima na mara nyingi chakula huambatana na maji , cha kukila atapanga mkeo,
jitahidi mkeo awe na tabia ya kupika vitafunwa nyumbani badala ya kununua ni ghali mnoo na akipika we beba nenda navyo kazini kwa ajili ya kifungua kinywa chako!
Tena ukifika job umsifie mkeo kuwa hapendi kabisa kukuona unaondoka bila kubeba BREAKFAST, yaani mkeo ana mahaba [emoji23][emoji23][emoji23]
Laki 1 inayobakia elfu 60 tenga kwa ajili ya kodi (hapa ni lazima uishi nyumba inayoendana na kipato chako na usiishi mbali sana na kazini kwako ili ikibidi wakati mwingine ufanye mazoezi ya kutembea kwa lazima) elfu 40 itayobakia utalipia umeme na nauli yako.
Kwa ukubwa wa kipato chako
1.mshawishi mkeo awe mjasiriamali kwa kufunga vitu vidogo vidogo na kuuza ili aku boost kwenye umeme na vinguo nguo pamoja na dhalula mbali mbali
2.sahau kuhusu michango ya harusi na vichenipati
3.Jitahidi uwe unawahi kurudi nyumbani ili umsaidie mkeo kazi za kuongeza kipato badala ya kuzulula kusiko na maana
4. Ishi kulingana na neema alizokujaalia M/Mungu,usitake kushindana na waja
 
Nyumba anakaa bure? Mbona hakuna kodi hapo
 
'Asubuhi
Chai 4@ 200 = 800
Maandazi 12@ 100 =1200
Jumla 2000'

Kila kikombe cha chai sh.200,hio hesabu umeitoa wapi?Kwani hao watu si wanapika chai nyumbani au wanaenda kununua hio chai kwa mama ntilie.

'Mchana
Sembe 1kg 2000
Veg 300
Viungo 1000
Maharage 1/4 700
Nishati mkaa 1000
Jumla 5000'

Blaza unatania aisee yaani familia ya watu watatu tena mmoja akiwa hayupo ameenda zake kazini useme wanamaliza kilo ya sembe mchana?

 
Sasa nifanyaje kama take hom ilikua laki 7 nkajikuta nakatwa kwe mkopo wa ujenzi kijubwa nna kibanda changu...chakula kununua kwa mwezi, umeme wa kata ,starehe tunawaachia vijana nasubiriq nimalizie bodi ya mkopo nichukue na gari...maisha ndo haya haya kupanga ndo kuchagua
 
Hela nyingi sana hiyo,wastani wa elfu 10,000/=per day???ungetaja location ingekuwa rahisi kukufanyia bajeti.
Kodi na Mambo mengine umeyaacha iweje?au umehisi anaishi kwa wazazi?na gharama nyingine za ziada anagharamiwa na bosi?ukiyawaza hayo na mengine ndo utakuwa unaongelea budgeting!na sio singinevyo.labda utujuze mawazo yako ya hyo elfu kumi
 
Kodi na Mambo mengine umeyaacha iweje?au umehisi anaishi kwa wazazi?na gharama nyingine za ziada anagharamiwa na bosi?ukiyawaza hayo na mengine ndo utakuwa unaongelea budgeting!na sio singinevyo.labda utujuze mawazo yako ya hyo elfu kumi
Mmenikumbusha nishawahi kufanya kazi morogoro mshahara ulikuwa elfu 25 kwa mwezi.chumba elfu 5kwa mwezi kula mchana kwa bosi.usiku jitegemee.hapo hujanunua nguo.nyumbani wanapiga simu kuomba hela, bado mchepuka.kuna cku nilijaa hasira boss nikamwambia kazi ya kijinga hii siiwezi nikaachana nayo.nikaja nyumbani nikaenda shule kusoma sasahiv niko chuo kikuu mwaka wa pili.
 
[emoji23][emoji23][emoji16]
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji23]nimecheka kifala
 
25,000 au 250,0000 ??[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji23][emoji23]

Itakuwa umekosea wewe
 
Baada ya makato na kubakia 300,000 una mke na watoto, unawezaje kumudu familia kwa huo mshahara?

Tupeane uzoefu.
Kama una familia ni kujenga uaminifu kwa mangi ili kanapokwisha hako kahela upate pa kukopa ili familia isilale njaa.

Muhimu: Tunaishi katika classes tofauti wapo wanaoiona hiyo laki 3 ni kubwa mno hata kuipata inawachukua miezi.

Uhalisia: Hiyo hela haitoshi ktk muktadha huo
 
Ila kwa maisha ya sasa kuoa kwa take home 300000 ni kujitafutia dhambi kwa Mungu tu na kuitesa familia tu. mm mwili wangu unareact na matatizo, kipato changu kikiwa kidogo hata hamu ya kudindisha haiji sembuse kuoa. Hapa nilipo namiaka 4 sijala demu walast kupata hamu kisa umaskini huu
 
Miaka 4?
 
itatosha kulingana na ww mwnyw utavyopanga matumizi yako kwa ufasaha...vijana msikimbie kuoa eti kisa take home ndogo, hamjui kuwa wngne mkioa mnpt baraka nyng zaid jmn,...hakikisha unafanya vitu kulingana na uwezo wako wa kipesa ulivyo, ...na ukiwa na mwanamke anayejielewa na ni mtafutaji, basi hakika ataelewa jinc ya kupangilia muishi vp...oeni jamani ..kuoa raha...usiige mambo lkn km uwezo bd acha
 

Aisee! Wakati hiyo ndio burudani pekee ya masikini na watu wa hali ya chini!
 
Baada ya makato na kubakia 300,000 una mke na watoto, unawezaje kumudu familia kwa huo mshahara?

Tupeane uzoefu.
Tumewahi maeneo yenye mvua mara 2 kwa mwaka tunalima chakula chote dukani tunafuata kibiriti, sukari ,colgate , mishumaa na kibiriti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…