Mliooa na mnaopata mshahara wa Tshs. 300,000 au chini ya hapo mnawezaje kumudu familia?

Mliooa na mnaopata mshahara wa Tshs. 300,000 au chini ya hapo mnawezaje kumudu familia?

Mkuu kwani chai inanyweka ya shiling ngapi?
Kama ni kula kuku, chipsi nyama choma hiko kiasi hakitoshi

Hapo anatakiwa aishi maisha ya kipato chake sio kufake

Leo unakula nyama kesho tembele
Maisha ndio ivyo

Hata sio ku-fake mzee,

Tu-assume una mke na mtoto mmoja

Chai tu kwa nyumbani kwa hiyo familia watatumia 3000 kima cha chini kabisa,

Wewe pia chai huko kazini kwako assumption 1000 au 1500

Haya mchana familia inakula kiasi gani na wewe unakula nini?

Usiku vipi?

Hapo hujaweka usafiri hata kama ni wa daladala

Hujaweka vocha

Bado hujanywa maji

Mzeee hiyo pesa mjini mtihani
 
Baada ya makato na kubakia 300,000 una mke na watoto, unawezaje kumudu familia kwa huo mshahara?

Tupeane uzoefu.
Mkuu by experience lazima uwe mwizi na uizoee ofisi fasta sana laki tatu kwa hapa town haitoshi hata uwe na budget gani tunaolipwa chini ya hapo ndio tunajua kweli pesa haitoshi lakini sio kwa laki tatu wizi unahusika sana ili kukamilisha mwezi
 
Take home yangu ni 229,000/ but Nina nyumba japo ya kawaida tu,mke na watoto wanakula na nyumbani kwa wazazi natoa huduma,hii kitu ni mipango tu mkuu,huwezi amini huwa nasevu na akaunti yangu haipungui million kwa tahadhari
Hpan utakuwa una viposho posho vingne unavipata
 
Nina Dogo ofisini anapata take home 200000,, kila siku Ana kunywa supu ya kuku asbh,mchana chakula cha 3000 na maji , ingawa hana family ila sielewagi,,
Acha kumfatilia mwenzako[emoji16][emoji16][emoji16]
 
Hata sio ku-fake mzee,

Tu-assume una mke na mtoto mmoja

Chai tu kwa nyumbani kwa hiyo familia watatumia 3000 kima cha chini kabisa,

Wewe pia chai huko kazini kwako assumption 1000 au 1500

Haya mchana familia inakula kiasi gani na wewe unakula nini?

Usiku vipi?

Hapo hujaweka usafiri hata kama ni wa daladala

Hujaweka vocha

Bado hujanywa maji

Mzeee hiyo pesa mjini mtihani
Chai ya 3000?

Hizo ni anasa mkuu, hiyo itakua ni soup

Kiuswazi mihogo au vitumbua vya 600 vinawatosha
Mchana watakula dagaa mchele au samaki kibua wa 3000 mpaka
Usiku wali mchele nusu inatosha baba mama na mtoto

Na chenji itabaki mkuu, hapo hata ikipigwa bajeti ya nyama nusu kilo 3000. Italiwa mchana na jioni plus mboga za majani na chenji ipo
 
Watu hawana mshahara kabisa.... MTU amekopa hadi salary slip inamdai na anaishi..

Kifupi unaishi Kwa taabu sana.

Hiyo laki tatu wadau hapo juu wanasema upunguze vitu visivyo vya lazima. Em wavitaje!?

Hela ndogo sana hiyo..
Anaishi kwa tabu kivipi mkuu,na hela aliyo ikopa alipeleka wapi?
 
Back
Top Bottom