Mliooa na mnaopata mshahara wa Tshs. 300,000 au chini ya hapo mnawezaje kumudu familia?

Mliooa na mnaopata mshahara wa Tshs. 300,000 au chini ya hapo mnawezaje kumudu familia?

Take home yangu ni 229,000/ but Nina nyumba japo ya kawaida tu,mke na watoto wanakula na nyumbani kwa wazazi natoa huduma,hii kitu ni mipango tu mkuu,huwezi amini huwa nasevu na akaunti yangu haipungui million kwa tahadhari
Chuma ulete wewe mzee wa busara
 
Kodi ya nyumba Tsh 70000 umeme 15000
Maji 10000
Chakula 5000x30
Matumizi mengine 30000 kwa mwezi
Haaaa sasa apo mkuu starehe izo, chumba weka 35, umeme 15, chakula 80, matumizi mengine 40, lazima ujifunge mkanda
 
Kuna anayepokea take home 1.3m na bado maisha yanamshinda.
Issue siyo unapokea ngapi mkuu issue ni unapangiliaje maisha yako na unajiongezaje nje ya mshahara.
Hata ukilipwa take home ya 2m kama hujiongezi na hupangilii mambo utashangaa kila mwezi unakuwa mtu wa madeni tu
Mimi Nalipwa 250k.
Nakaa Gheto Na Takataka Mmoja Anaelipwa 750 !
Lakini Akishapata Hela, Ndani Ya Siku Tatu HANA HATA MIA!
Kila Kitu Nafanya Mimi, Kuanzia,
- Chakula Gheto
- Maji
- Chai Asubuhi
- Umeme
- Soup/Maziwa
Mpaka Nauli Ya Kwenda Kazini Na Kurudi, Namlipia.

Yeye Pesa Yake Ni Konyagi Na Bangi.
- Na Kwa Kuwa Mimi Siyo Mtu Wa Kujali Sana Maisha Ya Mtu, Naheshimu Sana Uhuru Wa Mtu - Ananipa Wakati Mgumu Sana.
Maana Wakati Mwingine Uko Gheto Umechill ( Maana Mimi Ni Mtu Wa Kukaa Ndani Sana ) - Jamaa Anatoa Bangi Anawasha.

- Inabidi Utoke Tu Ukae Nje.

USHAURI.
- Vijana Na Arusha Na Mbeya Punguzeni Gambe, Sigara Na Bangi.
 
Nikweli ata ukilipwa million 700 kama auna nidhamu yapesa ni kazi bure tu
 
Duuuuuuuuuuuuuuh kodi ya nyumba kibongo bongo vyumba vya uswahilini si chini ya elfu 80,000 kwa mwenye familia.,,,,Maana chumba chenye umeme ni elfu 30,viwili 60,000 ukijumlisha na sebule 90,000/ ukipata kaservant kota si chini ya laki self contained.
Miaka 10 ijayo watu wengi watalala mabarabarani
 
Mmenikumbusha nishawahi kufanya kazi morogoro mshahara ulikuwa elfu 25 kwa mwezi.chumba elfu 5kwa mwezi kula mchana kwa bosi.usiku jitegemee.hapo hujanunua nguo.nyumbani wanapiga simu kuomba hela, bado mchepuka.kuna cku nilijaa hasira boss nikamwambia kazi ya kijinga hii siiwezi nikaachana nayo.nikaja nyumbani nikaenda shule kusoma sasahiv niko chuo kikuu mwaka wa pili.
Naona ulisoma kwa uchungu sana
 
Miaka 10 ijayo watu wengi watalala mabarabarani
Hata Mimi Naliona Hilo.

Hususani Kama Magu Au Mtu Mwenye Fikra Kama Za Magu Ndo Atakuwa Bado Anafanya Maamuzi Ya Nchi.
 
Binafsi naingiza laki 4 kwa mwezi, nina familia ya jumla ya watu 6 kila siku naacha nyumbani elfu 5 ..nipo mkoani kijijini kidogo.. Nilikopa na nimejenga maisha yanaenda
 
Huu ndio uzi unaotakiwa watu wamechangia kwa kuongea ukweli kabisa kutokana na uzoefu wao, Kwa maeneo ya vijijini ukijibana 300,000/- inatosha kibishi hivyohivyo.
Kijijini 300,000 unaishi maisha ya luxury mbona.
Kama kule kwetu ambako ndizi, mboga na maharage ni shambani
 
Nawaomba muweke maelezo ya ni kiasi gani kitatumika kwenye
Kodi ya nyumba
Uszafiri
Chakula
Umeme
Maji
Mawasiliano
Mavazi

Jifanye una mke na watoto wawili kisha tuwekee bajeti yako hapo sio kelele kama za wakulima wa matikiti wa Facebook
Kodi 80,000 vyumba 2 (kimoja chako na mke, kingine watoto 2)
Nauli 24,000 kwa mwezi
Maji 7,000
Umeme 15,000
Chakula 150,000

Jumla 276,000,
mke naye anajiongeza kwa vibiashara vya genge

Zilizobaki unaweza nunua vitu kama nguo, viatu n.k

Maisha mbona bomba tu
 
Mimi Nalipwa 250k.
Nakaa Gheto Na Takataka Mmoja Anaelipwa 750 !
Lakini Akishapata Hela, Ndani Ya Siku Tatu HANA HATA MIA!
Kila Kitu Nafanya Mimi, Kuanzia,
- Chakula Gheto
- Maji
- Chai Asubuhi
- Umeme
- Soup/Maziwa
Mpaka Nauli Ya Kwenda Kazini Na Kurudi, Namlipia.

Yeye Pesa Yake Ni Konyagi Na Bangi.
- Na Kwa Kuwa Mimi Siyo Mtu Wa Kujali Sana Maisha Ya Mtu, Naheshimu Sana Uhuru Wa Mtu - Ananipa Wakati Mgumu Sana.
Maana Wakati Mwingine Uko Gheto Umechill ( Maana Mimi Ni Mtu Wa Kukaa Ndani Sana ) - Jamaa Anatoa Bangi Anawasha.

- Inabidi Utoke Tu Ukae Nje.

USHAURI.
- Vijana Na Arusha Na Mbeya Punguzeni Gambe, Sigara Na Bangi.
Hahaa uhame hapo Mianzini /Ilboru kwa wahuni..
Pole sana mkuu
 
Mmenikumbusha nishawahi kufanya kazi morogoro mshahara ulikuwa elfu 25 kwa mwezi.chumba elfu 5kwa mwezi kula mchana kwa bosi.usiku jitegemee.hapo hujanunua nguo.nyumbani wanapiga simu kuomba hela, bado mchepuka.kuna cku nilijaa hasira boss nikamwambia kazi ya kijinga hii siiwezi nikaachana nayo.nikaja nyumbani nikaenda shule kusoma sasahiv niko chuo kikuu mwaka wa pili.
Ilikuwa mwaka gani isijekuwa ni miaka ya 2000 huko, maana kuna watu walikuwa wakifanya kazi kwa mshahara wa 10,000 na wanaishi poa tu
 
'Asubuhi
Chai 4@ 200 = 800
Maandazi 12@ 100 =1200
Jumla 2000'

Kila kikombe cha chai sh.200,hio hesabu umeitoa wapi?Kwani hao watu si wanapika chai nyumbani au wanaenda kununua hio chai kwa mama ntilie.

'Mchana
Sembe 1kg 2000
Veg 300
Viungo 1000
Maharage 1/4 700
Nishati mkaa 1000
Jumla 5000'

Blaza unatania aisee yaani familia ya watu watatu tena mmoja akiwa hayupo ameenda zake kazini useme wanamaliza kilo ya sembe mchana?
Hahaa, hapo sasa
Eti mchana tu
wanapikia mkaa wa 1000
Viungo vya 1000,
Maharage ya 700!
 
Back
Top Bottom