Watashindana hawatashinda!....hili jina Yesu,kuzim wenyewe wanajua ni hatariiiii,so tusibishane nao,tuwaombee!
Na pale Malaika walipo sema: Ewe Maryamu! Hakika Mwenyezi mungu anakubashiria (mwana) kwa neno litokalo kwake. Jina lake ni Masihi Isa mwana wa Maryamu,mwenye hishima katika dunia na Akhera, na miongoni mwa walio karibishwa (kwa Mwenyezi mungu). Qur'an 3:45
Naye atazungumza na watu katika utoto wake na katika utuuzima wake, na atakuwa katika watu wema. 3:46
Maryamu akasema: Mola wangu mlezi! Vipi nitampata mwana na hali hajanigusa mwanadamu?
Mwenyezi mungu akasema: Ndivyo vivyo hivyo,Mwenyezi mungu huumba apendacho. Anapo hukumu jambo, huliambia: kuwa! Likawa. 3:47
Na atamfunza kuandika na hikima na Taurati na Injili. 3:48
Na ni Mtume kwa wana wa Israili kuwaambia: Mimi nimekujieni na Ishara kutoka kwa Mola mlezi wenu, ya kwamba nakuundieni kwa udongo kama sura ya ndege. Kisha nampuliza anakuwa ndege kwa idhini ya Mwenyezi mungu. Na ninawaponesha vipofu wa tangu kuzaliwa na wakoma, na ninawafufua maiti kwa idhini ya Mwenyezi mungu, na ninakwambieni mnacho kila na mnacho weka akiba katika nyumba zenu. Hakika katika haya ipo Ishara kwenu ikiwa nyinyi ni wenye kuamini. 3:49
Na ninasadikisha yaliyo kuwa kabla yangu katika Taurati, na ili nikuhalalishieni baadhi ya yale mlio harimishiwa,na nimekujieni na Ishara kutokana na Mola mlezi wenu. Kwa hivyo mcheni Mwenyezi mungu na nit'iini mimi. 3:50
Hakika Mwenyezi mungu ni Mola wangu mlezi na Mola wenu mlezi. Basi muabuduni yeye. Hii ndiyo Njia Iliyo nyooka. 3:51
Isa alipo hisi kuwa kati yao pana ukafiri alisema: Nani wasaidizi wangu kwa Mwenyezi mungu? Wanafunzi wake wakasema: Sisi ni wasaidizi wa Mwenyezi mungu. Tumemuamini Mwenyezi mungu, na shuhudia kwamba sisi hakika ni Waislamu. 3:52
Mola wetu mlezi! Tumeyaamini uliyo yateremsha, na tumemfuata huyu mtume, basi tuandikie pamoja na wanaoshuhudia. 3:53
Na makafiri walipanga mipango na Mwenyezi mungu akapanga mipango, na Mwenyezi mungu ndiye mbora wa wenye kupanga.3:54
Pale Mwenyezi mungu alipo sema Ewe Isa! Mimi nitakufisha,na nitakunyanyua kwangu,na nitakutakasa na wale walio kufuru, na nitawaweka wale walio kufuata juu ya wale walio kufuru, mpaka siku ya Kiyama. Kisha marejeo yenu yatakuwa kwangu, nikuhukumuni katika yale mliyo kuwa mkikhitilafiana.3:55
Ama wale walio kufuru, nitawaadhibu adhabu kali katika dunia na akhera, wala hawatapata wa kuwanusuru.3:56
Na ama wale walio amini na wakatenda mema basi Mwenyezi mungu atawalipa ujira wao kaamili. Na Mwenyezi mungu hawapendi madhaalimu.3:57
Haya tunayo kusomea ni katika Aya na Ukumbusho wenye hikima.3:58
Hakika mfano wa Isa kwa Mwenyezi mungu ni kama mfano wa Adam;alimuumba kwa udongo kisha akamwambia: kuwa! Basi akawa.3:59
Hii ni kweli itokayo kwa Mola wako Mlezi. Basi usiwe miongoni mwa wanao fanya shaka.3:60
Watakao kuhoji katika haya baada ya kukufikilia ilimu hii waambie: Njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu,na wake zetu na wake zenu, na sisi wenyewe na nyinyi wenyewe, kisha tuombe kwa unyenyekevu tutake laana ya Mwenyezi mungu iwashukie waongo.3:61
Hakika haya ndoyo maelezo ya kweli. Na hakuna Mungu ila Mwenyezi mungu tu, na hakika Mwenyezi mungu ndiye mwenye nguvu na mwenye hikima.3:62