Mliowahi kuamka asubuhi na kukuta hali hii naombeni ushauri!

Mliowahi kuamka asubuhi na kukuta hali hii naombeni ushauri!

Jamani kucha sina,,imenitokea hivyo Mara kadhaa!Ajabu siku zote inapotokea hivyo ninakuwa kwenye usingizi mzito,asubuhi ninapoamka ninakuta damu mbichi inachuruzika!
Itakuwa unachukuliwa kichawi kwenda kufanya kazi na kupita vichakani. Ingia kwenye maombi.
 
Hiyo ni dalili ya wachawi walipita kwako usiku...omba Mungu kabla ya kulala.
 
wala usihofu, mimu hali ishawahi kunipata, dah we acha tu, nikafikiria mbali kwamba natembelewa na wachawi, nilipaniki sanaaaaa!! nilianza kulala saa tisa au kumi natumia simu ila nikiamka imoo!! nilianza kulala sizimi taa lakini wapi! nikiamka nakuta mikwaruzo nahisi kuchanganyikiwa kwakweli, nilienda kuombewa kanisani, mimi mkristo lakini nilienda kusomewa vifungu na sheikh, nilianza kuogea chumvi, kutuma ndulele, kuchoma bangi, n.k. njia za kudhibiti wagagula ila wapiii!!! kwa sasa imepungua sana ila kwa mwezi lazima nikute kamkwaruzo shavuni, utosini, mkononi, begani au kifuani.

jibu la hii hali nililipata nilipoweza kushuhudia live kwamba hii mikwaruzo hata mchana wa jua kali inaweza kutokea,

inakuwa kwamba mwanzoni ngozi ni kama inaumuka hivi inakuwa laini sanaa, baada ya muda uvimbe huo ukikauka ndio vinatokea hivyo vimikwaruzo. ikitokea uvimbe huu upo ukiwa umelalia sehemu iliyotokea ama inasuguliwa na shuka ama blanketi basi hio sehem laini inatoa vidamu. kwa utafiti wangu wa ziada sehemu hii huwaga ukiilamba kunakuwa na ladha kama ya betri la simu kule kwenye umeme.

kinachosababisha sijui nini ila mimi nahisi labda allege ama ulimwengu wa roho ila sio level ya uchawi maana hii ni mikwaruzo si chale, zile chale huwa ni kama umepigwa wembe uliozama ndani ya nyama kabisa na huwa hazifutiki, sio hivi vimikwaruzo baada ya mda tu vinapotea.

Mambo haya nilifanya na kwa sasa ni adimu sana mimi kupata hii mikwaruzo ila sijui ni kipi sasa.

Usafi wa kitanda na kuoga, zamani kusema kweli suala la usafi nilikuwa nyuma, kwa sasa kitanda lazima kibadilishwe shuka kila wiki na lazima nioge kila siku ama nisipooga siku hio basi lazima ninawe kichwa, kwapa na mitaa ya kati.

Zamani nilikuwa na tabia ya kujichua usiku au kusex nikipata ugeni, nilikuwa na kitabia shahawa nafutia kitambaa nakificha tu sehemu kinakauka na shahawa, kitambaa hiki kinaweza kukaa hata wiki hakifuliwi, alafu pia ilikuwa kawaida naweza nisinawe baada ya kupizi, Niliacha tabia hii nilianza kuhakikisha natumia tishu kufutia shahawa, nikijifuta natupa chooni naflashi naenda bafuni kunawa mitaa ya kati hata kama nilishaoga kabla, ni mwiko kusex au kujichua masaa mawili kabla ya kuomba kuingia kulala. (exception ni kwa mke au mume tu)

Nikiri pia zamani nilikuwa nalala kama ngombe sisali, niliacha hii tabia.

kunywa dawa za minyoo, wengi mara ya mwisho kunywa hizi dawa ni shuleni, mimi niliamua nipige dozi ya hii dawa zile za kutafuna na hapo nilikuwa nina miaka mitano sijatumia dawa ya minyoo, labda huenda hili tatizo minyoo inahusika, may be
 
Back
Top Bottom