Mliowahi kukutana na tatizo hili kuhusu kampuni ya Zola naombeni ushauri

Mliowahi kukutana na tatizo hili kuhusu kampuni ya Zola naombeni ushauri

UMUNYU

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2017
Posts
726
Reaction score
564
Kampuni ya nishati ya jua ya Zola walinifungia mtambo wao, lakini ajabu tofauti na makubaliano mtambo huu uligoma kuniwashia TV, na pia umeshindwa hadi kunichajia simu!

Nimejaribu kuwasiliana na Zola wamekuwa wananiahidi uongo. Mara tutashughulikia lakini hadi leo miezi zaidi ya kumi imepita bila msaada wowote!

Mliowahi kukutana na hili tatizo naombeni ushauri wenu wa jinsi mlivyofanya ili kutatua hilo tatizo, maana Zola hawanipi ushirikiano
 
Sorry na malipo unaendelea kulipa??? Sitisha kulipia watakuja tu kufuata makusanyo hapo hapo wabane kwamba mtambo haufanyi kazi. Japo mimi sijawahi tumia bidhaa za umeme wa jua.
 
Sorry na malipo unaendelea kulipa??? Sitisha kulipia watakuja tu kufuata makusanyo hapo hapo wabane kwamba mtambo haufanyi kazi. Japo mimi sijawahi tumia bidhaa za umeme wa jua.
Malipo nimewalipa vizuri sana hadi sasa kilichobaki ni kama 20% ya deni lote
 
washakuona unakaribia kumaliza wanakufanyia kusudi,wafate ofisini kwao waletee utata haswa

Enzi hizo nilishawahi tumia mKOPA ya voda nlikula nayo good time ,deni sikumaliza nkakorokochoa mtambo,Kitu hichooo kikawaka ikawa free mandela hadi nlipopata room ya umeme.
 
Back
Top Bottom