Mliowahi kutumia bati za kampuni ya BATI BOMBA LTD au kampuni zozote ndogo za mabati

hizi bati ni shida Kuna ndugu yangu kanunua 30g ni nyepesi sana sijui ni amepigwa au inakuaje
 
hizi bati ni shida Kuna ndugu yangu kanunua 30g ni nyepesi sana sijui ni amepigwa au inakuaje
Kuhusu wepesi ni kweli hili .
Pia bado kuna wahuni pia wanauza rejects ambazo unaweza sema ni zenyewe.

Bongo lolote linawezekana
 
Yaani bado unawaamini TBS hawa hawa pole sana,
 
Ili kufanya ulinganifu wa haki yabidi kujiuliza maswali haya kuhusu vipimo.
1. Bati unazotaka kununua zina vipimo gani kwa upana na urefu? Huwezi kufanananisha bei bila kujua upana kwa mfano kuna za upana halisi (effective width) 75cm, 80cm, 90cm nk.
2. Unene wa bati l; geji 26, 28, 30,32?

Pamoja na vipimo, kikubwa kinachotofautisha sana ubora ni kiasi cha aluzinc (aluminium na zinc) kilichotumika kulinda bati dhidi ya kutu. Kuna mabati yanatumia kiasi kidogo cha aluzinc ili kupunguza gharama za uzalishaji (aluzinc ni ghali kati ya malighali za utengenezaji wa bati).
Bati nyingi hapa Tanzania hazitengenezwi hapa, wanaagiza hapa wanakunja na kukata tu.
 
Hakuna BATI hapo nilinunua kiwandani 2020 April hata December haikufika zikapauka......kwanza bati ni nyepesi kuliko maelezo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…