Mliowahi kutumia bati za kampuni ya BATI BOMBA LTD au kampuni zozote ndogo za mabati

Mliowahi kutumia bati za kampuni ya BATI BOMBA LTD au kampuni zozote ndogo za mabati

Usijaribu hizo BATI nimewahi kulizwa 2020 yaani hata miezi 6 sikutoboa bati zishapauka hazieleweki rangi na eti wanakupa warranty ya miaka 10 upuuzi mtupu....najuta
 
Inawezekana kwani maji lita moja ya kilimanjaro bei gani mtaani na huko kwenye mahoteli yenu bei gani? Wali maharage kwa mama ntilie na wali maharage huko siju hoteli gani? Inawezekana sana
Nusu lita yale maji madogo tunauziwa elfu 8 hotel kubwa wakati mtaani jero
 
Asante sana Kiongozi. Nimeamua kujivisha mabomu huko huko Bati Bomba. Nadhan by tarehe 20 nitadaka mzigo.

Nitatoa mrejesho. Mana leo nimebonga nao bei wamekazi Kwenye 23k
Kwema kaka,
Hao jamaa Kwa bati za kupima wafahamu wanauzaje?
 
Usijaribu hizo BATI nimewahi kulizwa 2020 yaani hata miezi 6 sikutoboa bati zishapauka hazieleweki rangi na eti wanakupa warranty ya miaka 10 upuuzi mtupu....najuta
Mtoa na wote mzingatie ushauri huu
 
Kinachoshauriwa sana kwanza epuka matapeli wa buguruni hapo utapigwa utaambiwa ni alaf au wapi kumbe ni usanii tu umefanyika, wewe tafuta mtaalamu akishauri kwa mazingira yako rangi ipi inaweza kumudu kulingana na hali ya hewa ya hapo, na nyumba imejengwa uelekeo upi wa jua au usio na jua, unaweza kulalamika bati zinapauka kumbe fundi maiko aliijenga nyumba sehemu ambayo jua lote linamwagika muda mrefu hapo utapata matokeo pia
Kuna jamaa yangu yeye kauziwa mabati Buguruni gauge 30 Kwa TSH 23,000 per PC halafu ameingia kwenye jengo limeandikwa Alaf[emoji24]

Nimemwambia umeshapigwa mjomba haamini kama kapigwa!!
 
Mbona bati 110 sio nyingi? Nunua bati Bomba mbona wako vizuri tu.

Pitia uzi wa Elimu kuhusu Mabati uko humu. Utaelewa na kufanya maamuzi mazuri
Nitag huo uzi mkuu, mimi nafanya research pia bati za Taishan kama zina ubora
 
HIVi bei za bati za alaf kwa sasa zinanzia shilingi ngapi?
 
Back
Top Bottom