Mkuu,Mimi nimekuwa sales officer wa kampuni mbili za mabati Kwa wakati tofauti. Watu wengi wanashindwa kuelewa kuwa kampuni zote za mabati,bati zao huwa zinapauka ila hutofautiana kutegemeana na mazingira uliyopo, pamoja na ubora wa rangi iliyokuwa prepainted kwenye materials pamoja na thickness ya coating.
Kuhusu suala la ubora wa mabati ni kweli ALAF ni leading company kwenye industry ya mabati lakini hata naye huwa anapata changamoto ya bati kupauka kabla ya muda tegemewa.
USHAURI.
Mkitaka kununua bati ni kheri muwe mnaenda kununua kiwandani Moja kwa moja na siyo kwenda kwenye maduka.
Pia suala la msingi kabisa ni kuwa HAKUNA BATI YA GAUGE 30 ILIYOTIMIA AMBAYO INAUZWA CHINI YA SH25000/= ZA UPANA MDOGO NA SH 33,000/= UPANA MKUBWA(KWA DAR) NA 27,000/= UPANA MDOGO NA 35,000/36000 ZA UPANA MKUBWA (MIKOANI).HIZO ZOTE MNAZOAMBIWA NI GJ 30 NA INAUZWA KWA 23,000/= SI KWELI BALI HIYO NI GJ 30 INAYOELEKEA KWENYE GJ 32 AU NI GJ 32 KABISA.
KWA MASWALI NA MAELEZO ZAIDI MNAWEZA KUNIULIZA MASWALI NAMI NITAJIBU KWA KILE NINACHOKIJUA.
KARIBUNI SANA KINGLION MABATI.
LAZIMA TUAMBIANE UKWELI ILI TUSAIDIANE.