Ndugu P.D Nzige
Kutokana na uzoefu wangu kwenye ujenzi mimi huwa nafanya hivi,naangalia nikiweka za kawaida nitaokoa kiasi gani nikiweka za rangi nitapata hasara kiasi gani?mf bati nyeupe ya kawaida dukani ni 27,000/= ALAF kiwandani ni 37,500/= (currently price nimenunua juzi mwezi august) tofauti yake ni Tsh 10,500/=so kwa kesi yako ukisema uende na za kawaida it mean uta-save Tsh 1,155,000/= tu ambayo kwenye ujenzi wa nyumba ya bati 110 tuseme kwa ukubwa wake ukisema ifanye kitu kuendeleza ujenzi hakuna kitu itafanya kama ungependezesha kwenye paa.
Miaka mitatu mbele kama utaweka bati za kawaida utazichukia utataka uzipige rangi na itaku-cost siyo chini ya 700K na siyo rangi ya kudumu itakutaka tena baada ya muda fulani uirudie kwa gharama kama hiyo au zaidi.tofauti ya million 1 isikufanye nyumba yako ikose kupendeza weka kitu kizuri hata hizi za kichina achana nazo utakuta zinauzwa Tsh 33,000/= tofauti 4,500/= tu na ALAF ila kama kuweka bati za kawaida uta-save zaidi ya 2 mill weka tofauti na hivyo usiweke