Mliowahi kutumia bati za kampuni ya BATI BOMBA LTD au kampuni zozote ndogo za mabati

Mliowahi kutumia bati za kampuni ya BATI BOMBA LTD au kampuni zozote ndogo za mabati

Nimeona hapo umesema unahitaji bati 110, mm mwnyw kipindi nataka Kupaua nilikuwa nahitaji kuchukua ALAF ila kutokana na usumbufu wa pale ikabidi nitafute fundi ambaye kuna nyumba alipaua maeneo nilipo na kila nilipokuwa nikienda site ile nyumba bati lake lipo vilevile nyngn zinapauka, alafu ilikuwa imepauliwa vizuri ...nikamtafuta fundi aliyepaua nikamwambia kwanza nahitaji unipaulie tukaelewana, nikamuuliza ile nyumba bati zake za wapi? Akaniambia za Dragon ila kwautafiti wangu Dragon sikuwahi kuwaza kabisa...,mwisho wa Siku alinieleza ukweli jamaa alinunua sunshare,..nadhani mafundi Huwa wanapata chochote wakipeleka wateja...ikabidi nienda Sunshare, japo fundi aliniambia bati 110 ila mm nilikuwa sipendi bati mojamoja zinakuwa hazina muonekano mzuri zikipauliwa..ikabidi nimwambie anipimie nikakate kiwandani na nilienda na bajeti ileile ila huwezi amini kwa bati za kupima niliweza kusave kama lakin 6 hivi.

Kwaiyo kama unaweza jaribu hvyo...ila ushauri usije ukanunua bati za bei rahisi utaichukia nyumba yako.
Asante kwa Ushauri wako Kiongozi[emoji120][emoji120][emoji120]
 
Sasa hivi ukienda kuulizia Bei yake utapiga yowe[emoji23][emoji23]
Mwaka 2016 naanza kwenda Lindi kuna nyumba niliipenda sana. Nikasema nikijenga nitajenga kama hiyo. Hiyo nyumba ipo VETA lindi kwa mbele kidogo mkono wa Kushoto ukitokea Dar.

Imeezekwa na hivi hizi bati za vipisi vya vigae. Hiyo nyumba huu ni mwaka wa sita (leo nimepita hapo tena) bati liko vile vile kama jipyaaaaa , linawakaaaaaa.

Majirani mabati yamekua kama mashine za kusaga mahindi ila jamaa yake inadunda.

Pia ofiai yetu ina Kigae hivyp hivyo vya Charcoal Gray ni miaka na miaka havichuji.
 
Company - Sunbank
Contact - Lilian - 0766608764
Contact - Denis mbaga - 0712277442
Bundle Cm 80 - 16Pc’s@27,000- Tshs 464,000
Bundle Cm 90 - 16Pc’s@31,000 - Tshs 496,000
Upana wa Cm 90 - 1mitre - 12,500/=
Branch - Banda la ngoz
Gauge 30
Kofia 3Mitre - 17,000/=
Gata 3Mitre - 17,000/=
Misumari 1Kg - 10,000/=
Warranty 5yrs
———————

Company - Mabati Quality
Contact - Kwa mama mbaga - +255 764 183 844
Bundle Cm 90 - 16Pc’s@35,000 - Tshs 560,000/=
Upana wa Cm 90 - 1mitre - 11,800/=
Kofia 3Mitre - 12,000/=
Gata 3Mitre - 12,000/=
Misumari 1Kg - 9,000/=
Branch - Vingunguti
———————-

Company - Bati bomba
Contact - 0713041240 - 0689041240
Upana wa Cm 90 - 1mitre - 13,000/=
Kofia 3Mitre - 12,000/=
Gata 3Mitre - 12,000/=
Misumari 1Kg - 7,000/=
Bundle 16Pc’s@
Branch - Nyerere road/Quality centre
———————-


Sunshare..mabati - +255 625 559 221
——————

Company - Polaris
Contact - Marium - 0685234433
Bundle Cm 80 up 82-16Pc’s@25,000 -1m=12,000/=
Bundle Cm 88 up 90-16Pc’s@29,000 -1m=13,500/=
Branch - Mbez Africana
Gauge 30
Warranty 10yrs
——————-

Company - Haumile
Contact - rhobi - 0762753140
Bundle - 16Pc’s@25,500 - Tshs 408,000/=
Branch - Vingunguti
Transport & Nails - Free off chrgs
———————-

Company - ki Lion
Contact - 065 242 6313
Bundle - 16Pc’s@26,500 - 80cm - Tshs 424,000/=
Bundle - 16Pc’s@34,500 - 90cm - Tshs 552,000/=
Upana wa Cm 90 - 1mitre - 12,500/=
Kofia 3Mitre - 12,500/=
Gata 3Mitre - 12,500/=
Misumari 1Kg - 8,000/=
Branch - Vingunguti
Gauge - 30
——————-

Company - kiboko
Contact - +255717434444
Bundle - 16Pc’s@30,625 - Tshs 490,000/=
Upana wa Cm 90 - 1mitre - 12,500/=
Kofia 3Mitre - 15,000/=
Gata 3Mitre - 15,000/=
Misumari 1Kg - 14,000/=
Branch - Mwenge /ITV
——————-

Company - Tantu
Contact - +255 755 008 179
Bundle - 360mitre@7,000 - Tshs 2,520,000/=
Branch - mandela road -bugurun/Matumbi /Stand
——————-
 
Mimi nimewahi kuezeka nyumba kwa kutumia mabati ya rangi. Mwaka 2014 niliezeka nyumba kwa mabati ya kampuni ya Ando. Huu ni mwaka Wa 8 sasa bati lipo vizuri. Na mwaka jana nimeezeka nyumba nyingine kwa mabati ya Kampuni ya Taishan, ni mwaka sasa sijaona tatizo lolote lile, labda kwa miaka ijayo.
Kaka me nataka ninunue kwa hawa Taishan ila roho yangu inasita nishafika hadi ofisin kwao nilikuwa nataka nione shuhuda kama hizi
 
Mbona kama huyo mtu wa kinglion Mabati ni Mimi!!!!?[emoji23][emoji23][emoji23]
Mkuu nataka nikuulize!

Kuna jamaa yangu nilimuelekeza ALAF pale Tazara kiwandani unfortunately akawa hapajui so ana classmate wake ana hardware maeneo ya Buguruni akaenda lengo amuelekeze kiwanda kilipo kufika kumuelezea alichofata jamaa akamwambia anamjua agent wa ALAF anayeuza bei nzuri kama ya kiwandani.

Kilichonishangaza mimi jamaa alinipigia wakati ameshanunua bati na amenunua bei tofauti na kiwandani pungufu kama Tsh 1,000/= madai yake jamaa yake alimwambia ma-agent huwa wanapewa bei zao kwa sababu wanachukua mzigo mkubwa tofauti na akienda mteja kiwandani,nilienda kuziona zina ishara zote kwamba ni za ALAF zina muhuri wa kuchimba na mikanda kwa ndani yenye chata ya alaf but wasiwasi wangu kwa nini ziwe bei tofauti?

Hakupigwa kweli???
 
Mkuu nataka nikuulize!

Kuna jamaa yangu nilimuelekeza ALAF pale Tazara kiwandani unfortunately akawa hapajui so ana classmate wake ana hardware maeneo ...
Jamaa yako hakupigwa tofauti ya ALAF na viwanda vyote vya mabati ni moja tu;

Ukinunua bati ya ALAF kiwandani inakuwa Bei kubwa sana kulinganisha na Bei ya Agents zao waliosajiliwa.
Hii ni kwasababu agents wa Alaf wanauziwa bati kwa Bei ya punguzo Ili na wao wakatafute faida pia ALAF Wana mfumo wao wa kutegemea mauzo mengi kutoka kwa mawakala.

Lakini viwanda vingine vyote vya mabati ukienda kununua bati kiwandani ni Bei rahisi Sana kulinganisha na Bei utakayoikuta kwa wakala wao. Hii ni kwasababu viwanda hivi vinauzia mzigo mwingi sana kiwandani kuliko kwa mawakala wao.

Asante.
 
Back
Top Bottom