Mliowahi kutumia bati za kampuni ya BATI BOMBA LTD au kampuni zozote ndogo za mabati

Na huja kuweka mikunjo kwenye machine za aina hii
IMG_1022.jpg

IMG_1023.jpg
 
Kinachoshauriwa sana kwanza epuka matapeli wa buguruni hapo utapigwa utaambiwa ni alaf au wapi kumbe ni usanii tu umefanyika, wewe tafuta mtaalamu akishauri kwa mazingira yako rangi ipi inaweza kumudu kulingana na hali ya hewa ya hapo, na nyumba imejengwa uelekeo upi wa jua au usio na jua, unaweza kulalamika bati zinapauka kumbe fundi maiko aliijenga nyumba sehemu ambayo jua lote linamwagika muda mrefu hapo utapata matokeo pia
 
Utanzania ni kazi sana. Kitu kiuzwe 20 TZS kiwe sawa na kitu kinachouzwa 40 TZS.
Bro kiumbe anajikuna kutokana na uwezo wake. Ndio mana tunavaa jeans za 20k ila wenzetu wanaenda street soul jeans 100k

Kipindi tunavaa puma za mtumba buku 20 wenzetu wanavaa puma ya justfit ya 1.5m

Sio kwamba tunapenda
 
Hello Wadau.

Nipo stage ya kupaua nyumba. Nyumba inadai bati 110 , sasa ukigusa huku Alaf na kina Sunshare ni mkasi kweli kweli

Nina option mbili mkononi
1.nipige bati za kawaida tu
2.nipige bati za rangi toka kampuni ndogo ndogo.

Sasa hapo namba mbili nimeona kuna kampuni inaitwa Bati Bomba Ltd inajinasibu sana kuwa na bati konki master.

Naomba mwenye uzoefu kwa namna moja au nyingine na hiki kiwanda au hivi viwanda vidogo vidogo vya bati anisaidie mawazo na uzoefu wake

Hii bei ya bati itaondoa roho yangu aisee

,[emoji120][emoji120][emoji120]
Mbona bati 110 sio nyingi? Nunua bati Bomba mbona wako vizuri tu.

Pitia uzi wa Elimu kuhusu Mabati uko humu. Utaelewa na kufanya maamuzi mazuri
 
Hivi tunapozungumzia ubora wa bati tunaangalia muda mpaka bati ianze kupata kutu au muda ambao rangi itaanza kupauka?maana hizo unazosema za bei ndogo zimepitishwa na TBS,na wanatoa warranty ya miaka 10,sasa kigezo cha kuzipitisha ni nini?ina maana zinakidhi viwango.Mi naona mambo mengine hapa ni mfuko wa mtu,weka bati kulingana na uwezo wako,kwani wengi wetu nchi nzima tunaweka haya viwanda vidogo na hayo maswala ya kutu au rangi tutadanganyana tu humu...
Wapitie uzi wangu humu kuhusu Elimu ya Mabati
 
Hello Wadau.

Nipo stage ya kupaua nyumba. Nyumba inadai bati 110 , sasa ukigusa huku Alaf na kina Sunshare ni mkasi kweli kweli

Nina option mbili mkononi
1.nipige bati za kawaida tu
2.nipige bati za rangi toka kampuni ndogo ndogo.

Sasa hapo namba mbili nimeona kuna kampuni inaitwa Bati Bomba Ltd inajinasibu sana kuwa na bati konki master.

Naomba mwenye uzoefu kwa namna moja au nyingine na hiki kiwanda au hivi viwanda vidogo vidogo vya bati anisaidie mawazo na uzoefu wake

Hii bei ya bati itaondoa roho yangu aisee

,[emoji120][emoji120][emoji120]
Mkuu,Mimi nimekuwa sales officer wa kampuni mbili za mabati Kwa wakati tofauti. Watu wengi wanashindwa kuelewa kuwa kampuni zote za mabati,bati zao huwa zinapauka ila hutofautiana kutegemeana na mazingira uliyopo, pamoja na ubora wa rangi iliyokuwa prepainted kwenye materials pamoja na thickness ya coating.
Kuhusu suala la ubora wa mabati ni kweli ALAF ni leading company kwenye industry ya mabati lakini hata naye huwa anapata changamoto ya bati kupauka kabla ya muda tegemewa.
USHAURI.
Mkitaka kununua bati ni kheri muwe mnaenda kununua kiwandani Moja kwa moja na siyo kwenda kwenye maduka.
Pia suala la msingi kabisa ni kuwa HAKUNA BATI YA GAUGE 30 ILIYOTIMIA AMBAYO INAUZWA CHINI YA SH25000/= ZA UPANA MDOGO NA SH 33,000/= UPANA MKUBWA(KWA DAR) NA 27,000/= UPANA MDOGO NA 35,000/36000 ZA UPANA MKUBWA (MIKOANI).HIZO ZOTE MNAZOAMBIWA NI GJ 30 NA INAUZWA KWA 23,000/= SI KWELI BALI HIYO NI GJ 30 INAYOELEKEA KWENYE GJ 32 AU NI GJ 32 KABISA.
KWA MASWALI NA MAELEZO ZAIDI MNAWEZA KUNIULIZA MASWALI NAMI NITAJIBU KWA KILE NINACHOKIJUA.
KARIBUNI SANA KINGLION MABATI.
LAZIMA TUAMBIANE UKWELI ILI TUSAIDIANE.
 
Bro kiumbe anajikuna kutokana na uwezo wake. Ndio mana tunavaa jeans za 20k ila wenzetu wanaenda street soul jeans 100k

Kipindi tunavaa puma za mtumba buku 20 wenzetu wanavaa puma ya justfit ya 1.5m

Sio kwamba tunapenda
Sawa.
 
Mkuu,Mimi nimekuwa sales officer wa kampuni mbili za mabati Kwa wakati tofauti. Watu wengi wanashindwa kuelewa kuwa kampuni zote za mabati,bati zao huwa zinapauka ila hutofautiana kutegemeana na mazingira uliyopo, pamoja na ubora wa rangi iliyokuwa prepainted kwenye materials pamoja na thickness ya coating.
Kuhusu suala la ubora wa mabati ni kweli ALAF ni leading company kwenye industry ya mabati lakini hata naye huwa anapata changamoto ya bati kupauka kabla ya muda tegemewa.
USHAURI.
Mkitaka kununua bati ni kheri muwe mnaenda kununua kiwandani Moja kwa moja na siyo kwenda kwenye maduka.
Pia suala la msingi kabisa ni kuwa HAKUNA BATI YA GAUGE 30 ILIYOTIMIA AMBAYO INAUZWA CHINI YA SH25000/= ZA UPANA MDOGO NA SH 33,000/= UPANA MKUBWA(KWA DAR) NA 27,000/= UPANA MDOGO NA 35,000/36000 ZA UPANA MKUBWA (MIKOANI).HIZO ZOTE MNAZOAMBIWA NI GJ 30 NA INAUZWA KWA 23,000/= SI KWELI BALI HIYO NI GJ 30 INAYOELEKEA KWENYE GJ 32 AU NI GJ 32 KABISA.
KWA MASWALI NA MAELEZO ZAIDI MNAWEZA KUNIULIZA MASWALI NAMI NITAJIBU KWA KILE NINACHOKIJUA.
KARIBUNI SANA KINGLION MABATI.
LAZIMA TUAMBIANE UKWELI ILI TUSAIDIANE.
Aisee. Kila siku najifunza jipya.
Sasa nitawezaje kujiridhisha/kuthibitisha gauge ya bati before kununua ? (Yani nitajiridhisha vipi kuwa bati husika imetimia)
 
Njia asilia ni kutumia mikono,ukiishika unaweza kujua kuwa hii bati ni gj ngapi lakini kwakuwa ni mgeni wa mabati ni vyema ukaambatana na fundi wa kupaua akakusaidie kubaini.
 
Mkuu kwanza fahamu hamna bati isiopauka rangi hasa kwa mazingira ya kama dar es salaam kinachotofautiana n muda wa kuchelewa kupauka tu ndo unatofautiana, nina shuhuda nyingi za bati toka alaf na sunshire ya kupauka baada ya muda kwa dar es salaam, unaweza fanya utafiti wa nyumba iliojengwa kwa bati ya alaf ilio na miaka mitano toka iwekwe then angalia hali ya bati yake.
Kwa kulijua ilo mi binafsi niliamua niweke bati bomba tu kwenye kibanda changu na ishaanza pauka ingawa rate ya kupauka n ndogo, alaf au sunshire utaingia gharama kubwa tu then baada ya miaka isiozid mitatu utaja jilaum kwa gharama ulizotumia na matokeo unayoyapata.

Na wasichokijua watu kwenye wepesi wa bati una tegemea na gage ya hio bati unayonunua huwez fananisha wepesi wa bati bila kujua kama zina gage sawa au laaa, ila bat kama n gage 30 bac wepesi wake kampuni zote unafanana tu.
Wewe jamaa unajua sana. Nimekupendea hapo uliposema kuwa hakuna bati isiyopauka.

Wakati nataka kupaua, site kwangu walikuja makampuni mengi sana. Walikuja Alaf, Dragon, Taishan, Kinglion, Najenga Tanzania, SunBank etc. Wote walipita kunipa elimu na kunishawishi ninunue bidhaa kutoka kwao.

Katika watu/makampuni wote waliopita, nilimuelewa zaidi mtu wa mabati ya Kinglion (ingawa siku ya mwisho, sikununua mabati yake bali nilinunua mabati ya Taishan).

Aliniambia hivi, hakuna mabati yasiyopauka. Bati ni kama nguo. Nguo ukiinunua leo dukani, jinsi itakavyokuwa inang'aa ni tofauti kabisa na itakavyokuwa baada ya miaka michache ijayo kutokana kufuliwa na kupigwa na jua. Hivyo hivyo kwa mabati. Bati likipigwa na jua, likinyeshewa na mvua na likipulizwa na upepo lazima rangi ififie. Lakini akaniambia pia kuwa, ubora wa mabati ya makampuni yote ni ule ule isipokuwa wapo wengine tayari wametengeneza jina (wapo sokoni) siku nyingi.

Binafsi naamini, mabati yote ni sawa. Ni suala la mteja kuchagua kutokana na bajeti yake na rangi aitakayo.
 
Hivi tunapozungumzia ubora wa bati tunaangalia muda mpaka bati ianze kupata kutu au muda ambao rangi itaanza kupauka?maana hizo unazosema za bei ndogo zimepitishwa na TBS,na wanatoa warranty ya miaka 10,sasa kigezo cha kuzipitisha ni nini?ina maana zinakidhi viwango.Mi naona mambo mengine hapa ni mfuko wa mtu,weka bati kulingana na uwezo wako,kwani wengi wetu nchi nzima tunaweka haya viwanda vidogo na hayo maswala ya kutu au rangi tutadanganyana tu humu...

Mkuu ulichoandika unakielewa? Umeanza vizuri ila mwisho hatari tupu!
Kwahiyo hujui tofauti ya sunshare, Alaf na hao wengine?

Anyway maoni yako ni uhuru wako na yanaheshimiwa!
 
Aisee. Kila siku najifunza jipya.
Sasa nitawezaje kujiridhisha/kuthibitisha gauge ya bati before kununua ? (Yani nitajiridhisha vipi kuwa bati husika imetimia)
Labda uwe na vernier Caliper ili ukapime thickness ya bati. Wanakupa kipeperushi, unaangalia..gauge 30 ni thickness ya ngapi? Unapima.

Otherwise, waamini tu wenye kiwanda/wauzaji.
 
Wewe jamaa unajua sana. Nimekupendea hapo uliposema kuwa hakuna bati isiyopauka.

Wakati nataka kupaua, site kwangu walikuja makampuni mengi sana. Walikuja Alaf, Dragon, Taishan, Kinglion, Najenga Tanzania, SunBank etc. Wote walipita kunipa elimu na kunishawishi ninunue bidhaa kutoka kwao.

Katika watu/makampuni wote waliopita, nilimuelewa zaidi mtu wa mabati ya Kinglion (ingawa siku ya mwisho, sikununua mabati yake bali nilinunua mabati ya Taishan).

Aliniambia hivi, hakuna mabati yasiyopauka. Bati ni kama nguo. Nguo ukiinunua leo dukani, jinsi itakavyokuwa inang'aa ni tofauti kabisa na itakavyokuwa baada ya miaka michache ijayo kutokana kufuliwa na kupigwa na jua. Hivyo hivyo kwa mabati. Bati likipigwa na jua, likinyeshewa na mvua na likipulizwa na upepo lazima rangi ififie. Lakini akaniambia pia kuwa, ubora wa mabati ya makampuni yote ni ule ule isipokuwa wapo wengine tayari wametengeneza jina (wapo sokoni) siku nyingi.

Binafsi naamini, mabati yote ni sawa. Ni suala la mteja kuchagua kutokana na bajeti yake na rangi aitakayo.
Mbona kama huyo mtu wa kinglion Mabati ni Mimi!!!!?[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Nataman sana ila mambo yameumana balaa. Budget kikomo. Nishasqueez to the last point

Na siwezi fika mwezi Feb bila kuwa sijapaua aisee

Hapo ada ya dogo inadai na huku nategemea chalii tena
Acha ujinga mkuu. Leo unataka slope baada ya miaka 3 utaanza kulalamika bati mbaya, jikaze nunua ALAF kama kweli unaipenda nyumba yako.

RAHISI NI GHARAMA.
 
Back
Top Bottom