Nimeona hapo umesema unahitaji bati 110, mm mwnyw kipindi nataka Kupaua nilikuwa nahitaji kuchukua ALAF ila kutokana na usumbufu wa pale ikabidi nitafute fundi ambaye kuna nyumba alipaua maeneo nilipo na kila nilipokuwa nikienda site ile nyumba bati lake lipo vilevile nyngn zinapauka, alafu ilikuwa imepauliwa vizuri ...nikamtafuta fundi aliyepaua nikamwambia kwanza nahitaji unipaulie tukaelewana, nikamuuliza ile nyumba bati zake za wapi? Akaniambia za Dragon ila kwautafiti wangu Dragon sikuwahi kuwaza kabisa...,mwisho wa Siku alinieleza ukweli jamaa alinunua sunshare,..nadhani mafundi Huwa wanapata chochote wakipeleka wateja...ikabidi nienda Sunshare, japo fundi aliniambia bati 110 ila mm nilikuwa sipendi bati mojamoja zinakuwa hazina muonekano mzuri zikipauliwa..ikabidi nimwambie anipimie nikakate kiwandani na nilienda na bajeti ileile ila huwezi amini kwa bati za kupima niliweza kusave kama lakin 6 hivi.
Kwaiyo kama unaweza jaribu hvyo...ila ushauri usije ukanunua bati za bei rahisi utaichukia nyumba yako.