Mliowahi kutumia bati za kampuni ya BATI BOMBA LTD au kampuni zozote ndogo za mabati

Mliowahi kutumia bati za kampuni ya BATI BOMBA LTD au kampuni zozote ndogo za mabati

Hello Wadau.

Nipo stage ya kupaua nyumba. Nyumba inadai bati 110, sasa ukigusa huku Alaf na kina Sunshare ni mkasi kweli kweli

Nina option mbili mkononi

1. Nipige bati za kawaida tu
2. Nipige bati za rangi toka kampuni ndogo ndogo

Sasa hapo namba mbili nimeona kuna kampuni inaitwa Bati Bomba Ltd inajinasibu sana kuwa na bati konki master.

Naomba mwenye uzoefu kwa namna moja au nyingine na hiki kiwanda au hivi viwanda vidogo vidogo vya bati anisaidie mawazo na uzoefu wake

Hii bei ya bati itaondoa roho yangu aisee

,[emoji120][emoji120][emoji120]
Mkuu chukua mzigo paua majengo wako zinaubora Mzuri tu.
 
Kuna sister napiga nae nyumba yake alipiga hii chenachenga ya C.gray toka dragon. Nyumba inawaka balaa. Since 2020 bado kanadunda fresssh
Mkuu nipo Lindi.....tafadhali ukifika hatua ya kununua bati baada ya kujiridhisha tafadhali naomba tupe mrejesho....mimi nimeshamaliza boma nazchanga naiman panapo uhai na kipato....mwakani mwezi wa sita nitanunua bati...naimani umekusanya maoni yatakayokusaidia kuamua hasa ukizingatia upo karibu na town.... usisahau feedback kaka
 
Mkuu Mimi nimekuwa sales officer wa dragon na Sasa niko na Kinglion,Si sales wa ALAF ila Kwa uzoefu wangu wa mabati naweza kutambua bati original ya ALAF kwa kuzingatia vitu viwili;
1. Muhuri wa moto ule wa vinundu(sijakua kama nitakuwa sahihi) ila ni ule muhuri unaobonyeza bati kabisa.
2. Kwenye migongo mipana katikati ya migongo huwa na vibaraza vya kumwagia maji,Sasa kwenye vile vibaraza utaona Kuna vimistari vitatu.
Naruhusu kurekebishwa pale nilipokosea.

Uko sawa- Ile SEAL au mhuri wa moto unatumika sana kuitambua ALAF .
 
Asante kwa maoni. Kama hutojali naomba nikucheki PM
bati bomba kimeo kaka mie nazijua achana nazo siuzi bati ila nakushauri chukuwa kiboko.
kwangu hapo sijawahi tumia nje ya kiboko
20221116_173723.jpg
 
Mkuu nipo Lindi.....tafadhali ukifika hatua ya kununua bati baada ya kujiridhisha tafadhali naomba tupe mrejesho....mimi nimeshamaliza boma nazchanga naiman panapo uhai na kipato....mwakani mwezi wa sita nitanunua bati...naimani umekusanya maoni yatakayokusaidia kuamua hasa ukizingatia upo karibu na town.... usisahau feedback kaka
namm pia mkuu
 
Kwani lazima uezeke na bati tafuta hata makuti uezeke uingie kwenye kibanda chako maisha mbona simple sana
 
  • Thanks
Reactions: Gru
Kwani lazima uezeke na bati tafuta hata makuti uezeke uingie kwenye kibanda chako maisha mbona simple sana
Nipo ndani. Nilianza kwa kuezeka master bedroom na kasehemu kadogo kakupigia gahwa. Sasa nataka nipige nyumba nzima
 
Hello Wadau.

Nipo stage ya kupaua nyumba. Nyumba inadai bati 110, sasa ukigusa huku Alaf na kina Sunshare ni mkasi kweli kweli

Nina option mbili mkononi

1. Nipige bati za kawaida tu
2. Nipige bati za rangi toka kampuni ndogo ndogo

Sasa hapo namba mbili nimeona kuna kampuni inaitwa Bati Bomba Ltd inajinasibu sana kuwa na bati konki master.

Naomba mwenye uzoefu kwa namna moja au nyingine na hiki kiwanda au hivi viwanda vidogo vidogo vya bati anisaidie mawazo na uzoefu wake

Hii bei ya bati itaondoa roho yangu aisee

,[emoji120][emoji120][emoji120]
Kaka ulifanikiwa kupaua kwa bati ya kampuni gani?
 
Back
Top Bottom