Mlipuko mkubwa watokea mji mkuu wa Lebanon, Beirut. Watu zaidi ya 78 wafariki na zaidi ya 4,000 kujeruhiwa

Mlipuko mkubwa watokea mji mkuu wa Lebanon, Beirut. Watu zaidi ya 78 wafariki na zaidi ya 4,000 kujeruhiwa

Israel was ruled out. Tangu mwanzo Israel huwa haina bifu na Lebanon bali ina bifu na Hezbollah. Hezb yenyewe iliomba kuwepo umoja katika tukio hili, hawajajiapiza kama wanavyofanyaga mara zote. Maana yake mpaka wao wanaamini ni ajari, ingawa najua wanachunguza kivyao.

Mkuu wa Usalama na Waziri Mkuu wamesema kulikuwa na ammonium nitrate tani 2750 zimehifadhiwa kwenye ghala kwa kipindi cha miaka 4-6. Hizi hutumika kutengeneza mabomu na mbolea, nyingi serikali ilikuwa inazikamata kama magendo. Kuna uzembe wa mamlaka za bandari. Mafataki pia yalikuwepo, moto ulianza kwa namna nyingine ndipo ammonium nitrate ikalipuka. Chanzo cha huo moto wa mwanzo ambao ulikuwa unatoa flash nyeupe za mwanzoni ndo bado kujulikana. Kuna mchanganyiko wa explosive substances maana ni kama warehouse ya milipuko ya aina yote. Ndo maana kuna moshi mweupe, yellow, na rangi gani sijui.

Naamini nchi nyingi zitatoa msaada maana Lebanon ni ndogo. Israel yenyewe imesema ina mazungumzo kupitia third party kutoa msaada. Qatar inatuma vitanda vya dharula kwa majeruhi, Saudi Arabia inakuja, Turkey, Iraq na wengine.
Trump kama kawaida yake anatoa taarifa bila uhakika, alidai inaonekana ni shambulizi. Kauli yake itapuuzwa.
hizi ndo taarifa za kisomi
shukran mkuu
 
Sasa hapo ndio muone maajabu ya Mungu wa kweli wa ISRAEL wala israel haijahusika kulipua na hizo material zilizolipuka walikuwa wanaandaa silaha za maangamizI dhidi yaya watu wa Mungu wa kweli wayahudi. Ukitaka mambo yako yasikunyookee kuwa adui wa Israel. Sasa hivi mataifa mengi ya kiislamu yamegundua hili Omani, saudia, UAE, Maroc n.k kwa kichinichini na kujifichajificha kama nikodemu wanampigiaga simu netanyahu. Majuzi tu hapa Somaliland wanataka diplomasia na israel hadi wenzao Mogadishu wakaja juu.

hearly
Hapa tu ndio mnaponiacha hoi... Hadi ninyi wenyewe mnajidharau mbele ya binadamu wenzenu!
 
Israel was ruled out. Tangu mwanzo Israel huwa haina bifu na Lebanon bali ina bifu na Hezbollah. Hezb yenyewe iliomba kuwepo umoja katika tukio hili, hawajajiapiza kama wanavyofanyaga mara zote. Maana yake mpaka wao wanaamini ni ajari, ingawa najua wanachunguza kivyao.

Mkuu wa Usalama na Waziri Mkuu wamesema kulikuwa na ammonium nitrate tani 2750 zimehifadhiwa kwenye ghala kwa kipindi cha miaka 4-6. Hizi hutumika kutengeneza mabomu na mbolea, nyingi serikali ilikuwa inazikamata kama magendo. Kuna uzembe wa mamlaka za bandari. Mafataki pia yalikuwepo, moto ulianza kwa namna nyingine ndipo ammonium nitrate ikalipuka. Chanzo cha huo moto wa mwanzo ambao ulikuwa unatoa flash nyeupe za mwanzoni ndo bado kujulikana. Kuna mchanganyiko wa explosive substances maana ni kama warehouse ya milipuko ya aina yote. Ndo maana kuna moshi mweupe, yellow, na rangi gani sijui.

Naamini nchi nyingi zitatoa msaada maana Lebanon ni ndogo. Israel yenyewe imesema ina mazungumzo kupitia third party kutoa msaada. Qatar inatuma vitanda vya dharula kwa majeruhi, Saudi Arabia inakuja, Turkey, Iraq na wengine.
Trump kama kawaida yake anatoa taarifa bila uhakika, alidai inaonekana ni shambulizi. Kauli yake itapuuzwa.
Sijui, ila nahisi source ya ule mlipuko wa awali ni muhimu zaidi kujulikana
 
Naona magorofa yanapepea tu kama manyoya ya njiwa anaenyonyolewa baada ya kuchinjwa! Aiseeh....
 
Smoke billows from the scene of the explosion


Moshi kutoka eneo lililolipuka
Lebanon inaomboleza baada ya mlipuko mkubwa katika mji mkuu wa Beirut kuwaua watu 78 na kuwajeruhi wengine 4000 siku ya Jumanne.
Mji wote uliyumbishwa na mlipuko huo, ulioanza kwa moto katika bandari kabla mlipuko huo uliofanana na wingu la uyoga kutokea.
Rasi Michel Aoun alisema kwamba tani 2,750 za ammonium nitrate zilikuwa zimewekwa vibaya katika ghala moja kwa miaka sita.
Aliitisha kikao cha dharura siku ya Jumatano , na kusema hali ya dharura ya wiki mbili imetangazwa.
Rais Aoun pia alitangaza kwamba serikali itatoa $66m za hazina ya dharura. ''Kile tunachoshuhudia ni janga kubwa'' , alisema mkuu wa kundi la msalaba mwekundu George Kettani akizungumza na vyombo vya habari. ''Kuna waathiriwa kila mahali''.
A man carries away an injured girl in Beirut


Mwanaume aliyembeba msichana aliyejeruhiwa Beirut
Maafisa walisema siku ya Jumanne kwamba uchunguzi unaendelea ili kubaini chanzo kilichosababisha mlipuko huo.
Baraza kuu la ulinzi nchini Lebanon lilisema kuwa wale waliohusika wataadhibiwa vilivyo.
Ammonium Nitrate ilikuwa imeshushwa kutoka kwa meli iliokamatwa katika bandari hiyo 2013 na kuwekwa katika ghala.
Mlipuko huo unajiri wakati mgumu kwa upande wa taifa hilo , huku likikabiliwa na mgogoro wa kiuchumi unaosababishwa na mgawanyiko wa jadi huku taifa hilo likiathiriwa na mgogoro mwengine wa virusi vya corona.
Hali ya wasiwasi pia iko juu kabla ya uamuzi wa siku ya Ijumaa kuhusu kesi ya mauaji ya aliyekuwa waziri mkuu Rafik Hariri 2005.
An injured man is evacuated from the scene


Mwanaume aliyejeruhiwa akiondolewa kutoka eneo la tukio
Je ni nini kilichotokea?
Mlipuko huo ulitokea muda mfupi baada ya mwendo wa saa kumi na mbili siku ya Jumanne.
Mwandishi wa BBC aliyekuwa katika eneo hilo aliripoti miili ya watu waliokuwa wameuawa na uharibifu mkubwa, unaoweza kuifunga bandari hiyo ya Beirut kwa muda.
Vyombo vya habari viliwaonyesha watu wakiwa wamenasa chini ya vifusi.
Shahidi mmoja alielezea mlipuko huo kuwa mkubwa hali ya kwamba unaweza kusababisha watu kuwa viziwi, huku kanda ya video ikionesha magari yalioathirika pakubwa mbali na majumba yalioharibika.
This picture taken on August 4, 2020 shows a general view of destruction along a street in the centre of Lebanon's capital Beirut


Mlipuko huo umeharibu nyumba nyingi
''Majumba yote yaliokuwa karibu na mlipuko huu yameanguka . Ninatembea juu ya vigae na vifusi wakati wa usiku'', shahidi mmoja karibu na bandari hiyo aliambia AFP.
Hospitali zilidaiwa kushindwa kuhimili idadi ya watu na majumba mengi yaliharibiwa.
Mlipuko huo ulisikika umbali wa kilomita 240 katika kisiwa cha Cyprus mashariki mwa bahari ya mediterenean, huku watu katika eneo hilo wakisema walidhania lilikuwa tetemeko la ardhi.
Je ammonium nitrate ni nini?
Amonium nitrate ina matumizi tofauti, lakini matumizi yake mawili maarufu zaidi ni kilimo kama mbolea na kutengeza vilipuzi.
Inalipuka kwa haraka inapokutana na moto , na inapolipuka , hutoa gesi yenye sumu ikiwemo ile ya nitrogen oxide na gesi ya ammonia.
A migrant worker reacts in shock following an explosion at the Beirut Port

Hali ilivyokuwa mitaani baada tu ya kutokea mlipuko
Na kwasababu ni rahisi kulipuka, kuna masharti makali kuhusu jinsi ambavyo inafaa kuhifadhiwa ili kusalia salama ikiwemo sharti kwamba eneo la kuihifadhi linafaa kuzuiwa kuvutia moto.
Je hali ikoje nchini Lebanon?
Lebanon inakabiliwa na mgogoro wa kisiasa , huku maandamano dhidi ya serikali kwa kushindwa kukabiliana na tatizo la kushuka kwa uchumi tangu mgogoro wa kiuchumi wa 1975-1990.
Wengi wanalaumu maafisa wakuu serikalini ambao wanatawala siasa kwa miaka kadhaa na kujilimbikizia mali , huku wakishindwa kufanya mabadiliko muhimu ya kutatua tatizo la taifa hilo.
Raia wanakabiliwa na tatizo la kukatwa kwa umeme kila siku, ukosefu wa maji safi ya kunywa na huduma ya afya .
Beirut after the explosion


Eneo karibu na bandari ya Beirut lilivyoathirika na mlipuko
Kumekuwa na hofu katika mpaka na Israel, ambayo ilisema wiki iliopita kwamba ilizuia jaribio la Hezbollah kuingia katika himaya ya Israe
lakini afisa mmoja mkuu wa Israel ameambia BBC kwamba Israel haina uhusiano wowote na mlipuko wa Beirut.
Mlipuko huo ulitokea karibu na eneo ambalo mlipuko mkubwa wa gari ulimuua waziri huyo wa zamani Hariri.
 
Huu ni mlipuko wa ammonium nitrate ambayo ilikuwa kwenye ghala. Na huo mzigo inasemekana ni wa Hezbollah. Hii ndio imeonesha ni kwanini nchi nyingi zimezuia matumizi ya hiyo mbolea katika kilimo baada ya watu kuanza kuzitumia kufanya mambo ya ugaidi.

Ila kwa ammonium mpaka itoe mlipuko mkubwa vile ni hadi iwe imechanganywa na ratio flani ya diesel ndio blasts inakuwa na mshindo na mlipuko mkubwa vile. Ishu ni je hiyo diesel ilipatikana vipi hadi ikajimix na hiyo ammonium? Je imetokea kama ajali au tukio la kupangwa?

Pia inawezekana huo mlipuko wa ammonium umetokea kama deviation ila target labda ilikuwa ghala jingine lenye silaha. Hivyo kwa huo mlipuko wa ammonium itafanya uchunguzi kuishia hapo kwenye hiyo ammonium.
Iran lazima akomalie hiyo show maana hizbolah ni derivative yao, na mfaransa ni muuza bidhaa za nyuklia wa siri mashariki ya kati.
 
Kwa kiwango hiki cha ammonium nitrate tuseme wana afadhali ya kuwa na vifo na uharibifu kidogo. Mwaka 1947 mlipuko wa tani 2000 za hii compound mjini Texas, Marekani ulisababisha watu 581 kufa. Mwaka 1995 shambulizi la kigaidi la mabomu ya kutengenezwa kwa mkono ya compound hii liliua watu 168 mjini Oklahoma, Marekani.

Maofisa wamedai tani hizi 2750 zilikamatwa kutoka kwenye meli moja kama magendo mwaka 2014. Mzigo utakuwa ulishapungua makali kwa kuhifadhiwa hivyo na kukaa muda mrefu. Kingine cha msaada hakukuwepo chain reaction kwenye viwanda, mabomba ya mafuta, mifumo ya umeme au majengo ya watu.
Pia eneo hilo limesemekana linakaliwa zaidi na wakristo lina maeneo ya starehe ambayo siyo makazi ya watu kuna pubs na viwanja kadhaa. Kwa vile haikuwa weekend na ni jioni, naamini watu hawakuwa wengi sana around.

Hospitali nne ziliharibiwa kiasi na mlipuko na wafanyakazi wake walijeruhiwa hivyo hazikuweza kutoa msaada sana. Waziri wa afya amesema wanahitaji msaada wa kila kitu kwa kuwa wana upungufu wa kila kitu. Depot ya chanjo zotei inasemekana imeharibika.

Source: Compilation ya vyombo vya habari vya mabeberu kama NY Times, BBC, Aljazeera, DW, Haaretz, Reuters, etc.
IMG_20200805_110157.jpg
IMG_20200805_110136.jpg
IMG_20200805_110115.jpg
IMG_20200805_110104.jpg
 
Allah aendelee kuwaponya wote waliopata ajali, na awape subra wote waliofiwa.


Lebanon ni ndugu zetu haswaa, tunawapenda kwa ajili ya Allah.
 
Back
Top Bottom