PakaJimmy
JF-Expert Member
- Apr 29, 2009
- 16,199
- 8,761
Wanajamvi,
Kama ambavyo tumekuwa tunawajulisha hapa majamvini, Wana-Arusha Wing tukiwakilishwa na Blaki Womani, marejesho Filipo, Arushaone, Lily Flower Preta, werawera na miye PakaJimmy tumefanya safari ya siku 2 Tanga ambayo imekuwa ya mafanikio sana, ambapo kumbukumbu zake hazitatutoka hadi tutakapo'rip'.
Tulifika Tanga 28/12/2012, saa 9.30 jioni,na tukapokelewa na WanaTanga Dark City, KOKUTONA, CHUAKACHARA Mwanyasi na Arabela. Hakika hawa watu walijipanga sana kuhakikisha sisi wageni wao tunapata ladha ya ki-Tanga.
Dar-Wing iliwakilishwa na Chipukizi watatu ambao ni watu8, Smile na Madame B.
Jioni hiyo baada ya kuandaliwa maji ya kuoga ya iliki, tulipelekwa Tanga Beach Resort ambako tuliungana rasmi kama kundi moja la Arusha, Tanga na Dar(u can imagine how amazing it was) na tukapata picha za kumbukumbu na kufanya utambulisho....tukamalizia na Vinywaji na kuondoka eneo hilo tukielekea sehemu maaalum iitwayo NYINDA kwaajili ya mavitu ya kuchomachoma, maspice na kinywaji.
Tulikaa Nyinda hadi saa 4.30 za usiku tukifurahi, tukijadiliana na kupeana zawadi mbalimbali, ambapo baada ya hapo tulipelekwa na wenyeji wetu mahala panaitwa Nyumbani Hotel, ambako palikuwa na Live Band, hapo tena sitaelezea zaidi yaliyojiri.
Asubuhi 29/12/2012 tuliandaa usafiri kuelekea Amboni Caves, ambako hakika tulishuhudia maajabu ya Mungu na kufaidi vilivyo dhana ya UTALII WA NDANI. Tuligundua kuwa JF inahitaji gym, maana kuna wenzetu ambao ilibidi wavutwe na jeki ili waweze kupenya matundu ya kule mapangoni..Loools!
Kisha safari ya kurudi mjini ikaanza, ambapo bahati mbaya tukiwa eneo maarufu la Chumvini mwenzetu mmoja Madame B alipata ajali ndogo, ambapo ilibidi watalii sisi tutumie uzoefu kutoa huduma ya kwanza ambayo, kwa bahati nzuri ilimponya, ha ha haaa.
Moja kwa moja itinerary yetu ilituonyesha kuwa tunatakiwa kwenda Pangani ili kushuhudia Mambo ya kale sana na ya kihistoria inayoshangaza chini ya jua. Tulifika Pangani salama chini ya tour-Guide Arabela na tuligaragara sana kwenye Beaches za huko. Tulitembelea sehemu ya maungano ya Mto Pangani na Bahari ya Hindi, tukaona mji mkongwekabisa wa Pangani ambao unaaminika kuwepo tokea takriban karne ya 6 BC
Mwisho tukapata Menyu ya uhakika pale Beach, Seaside Community Centre, kwa Sister Maria-Salome!
.
Tulirudi Tanga mjini tukiwa tumechoka sana, lakini tukiwa na furaha sana ya kukamilisha ziara yetu. Jioni hiyo tulikaa tena kama group zima na kufanya debriefing au postmorterm ya tour yetu, huku tukipata vitu vitamu na vichungu..Lols!, Lakini zaidi tulikuwa tukiagana na kutakiana heri, kitendo kilichowatoa machozi baadhi ya members, maana ilikuwa ngumu sana kutamka bye bye! ...Asubuhi 30/12/2012 kila mtu alishika njia kuelekea kwao.
Ahsanteni sana, hiyo ndiyo summary ndogo sana ya tour yetu...!