Mliwasikia Kitayosce walivyosema?

Kichuchunge

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2020
Posts
384
Reaction score
970
Afisa habari wa klabu ya Kitayosce, Pendo Lema amesema walikuja Dar es Salaam na wachezaji (20) kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Azam football club.

Jana asubuhi walikamilsha malipo yote ya vibali vya wachezaji wao wote (TFF) wakaambiwa mtandao unasumbua hivyo wasubiri majina ya wachezaji wao yaingizwe.

Ameendelea kusema, baadae mchana wakapewa taarifa kuwa majina (8) ya wachezaji wao yameingizwa kwenye system wasubir majina mengine.

Ameeleza kuwa, wachezaji hao (8) sio wa kikosi cha kwanza ni wale waliopanda daraja na timu kutokea Championship.

Mpaka muda wa mchezo unafika amesema majina yaliyokuwa kwenye system wanaoruhusiwa kucheza yalikuwa (8) tu hivyo ikabidi waende hivyohivyo uwanjani.

Majina yote ya wachezaji wao tayari yameingizwa kwenye system mpaka sasa, ameeleza kuwa jana usiku ndio walipewa taarifa kuwa majina yote yako verified.
 
Kwann wao siku ya mechi ndo waje walipe na kutaka wachezaji wao waingizwe kweny system?? Hebu imagine ratiba imetoka muda tuuu wao siku hyo hyo ya mechi ndo wafanye malipo serious??
Na huu ndo Utanzania wetu, mtu unafanya jambo fulan mpka kuwe kuna jambo la kulazimisha kufanya hivyo
 
Next time wayapeleke a week before..., System zetu tunazijua sisi; ukizingatia huenda TFF hawaruhusiwi kufanya haya mambo manually.....

Kwahio iwe funzo la kutokufanya vitu last minute...., Inaweza kutokea kwa watu watatu au wanne lakini sio timu nzima
 

Walikuwa wapi kufanya hivyo mapema?
 
Walikuwa wanadaiwa na mchezaji FIFA iliwafungia
 
Hiyo ratiba inetoja lini ndugubtangu? Mwez
i, wiki kabla ya ligi kuanza?.
 
Hivi tatizo ni TFF au Kitayosce?

System kusumbua ni jambo la kawaida. Kwann walisubiri hadi siku ya mechi kulipia ada ya ushiriki?

Hapa kosa si TFF.
 
Nchi hii ni full fukayose aisee kha.

Kila sekta ni jogobo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…