Kichuchunge
JF-Expert Member
- Dec 2, 2020
- 384
- 970
Afisa habari wa klabu ya Kitayosce, Pendo Lema amesema walikuja Dar es Salaam na wachezaji (20) kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Azam football club.
Jana asubuhi walikamilsha malipo yote ya vibali vya wachezaji wao wote (TFF) wakaambiwa mtandao unasumbua hivyo wasubiri majina ya wachezaji wao yaingizwe.
Ameendelea kusema, baadae mchana wakapewa taarifa kuwa majina (8) ya wachezaji wao yameingizwa kwenye system wasubir majina mengine.
Ameeleza kuwa, wachezaji hao (8) sio wa kikosi cha kwanza ni wale waliopanda daraja na timu kutokea Championship.
Mpaka muda wa mchezo unafika amesema majina yaliyokuwa kwenye system wanaoruhusiwa kucheza yalikuwa (8) tu hivyo ikabidi waende hivyohivyo uwanjani.
Majina yote ya wachezaji wao tayari yameingizwa kwenye system mpaka sasa, ameeleza kuwa jana usiku ndio walipewa taarifa kuwa majina yote yako verified.