Kipindi kile cha kitafuta marafiki kwenye gazeti nikatuma namba Yangu kwenye gazeti la majira.
Mungu si Athumani jioni ya siku ambayo gazeti limetoka nikapigiwa simu na binti akajitambulisha anaitwa Shainur Sumra nikamuuliza ,wewe ni mwarabu akasema hapana Bali ni Muhindi aliyezaliwa Tanga na hata huko India hapajui.Na yeye alipoona jina langu akadhani Mimi ni mhindi ila nilipomwambia Mimi ni mbena tena wa Njombe huku.
Dah nikaona zali tukachati baadae tukaingia kwenye mahusiano bila kuonana huku nikivuta taswira ya mrembo amazing .
Siku ya kuonana sitoisahau maana tulikutana posta pale J.M.MALL kuna casino inaitwa Le grand . Nilitamani muda uende ili tuachane kila mtu aende zake maana mtoto wa kike ana kitambi hata Mzee Kilomoni wa Simba ana afadhali.
Alipoondoka tu nilimblock na sikumuhitaji mpaka Leo sijui alinichukuliaje lakini yeye alikuwa anapiga hesabu za ndoa.