Hao watoto watamu sana! Asikwambie mtu, kwenye ukuaji wangu sikuwahi kabisa kuvutiwa na wanawake wa aina hiyo lakini nilipoanza masomo rasmi ya sekondari, mzee alinipeleka shule moja binafsi hapa jijini Dar nikaanza kidato cha kwanza rasmi... lakini maadili ya shule ile hayakumpendeza mzee wangu, aliona mabadiliko ya tabia kwangu mimi kijana wake hivyo basi nilipokuwa nakaribia kukamilisha mwaka niingie kidato kinachofuata mzee ikabidi ashauriane na Kaka yangu mmoja hivi mkubwa na ana familia yake pia alikuwa mtu wa dini sana! Kaka yangu akamshauri anipeleke shule ya seminari nikaanze tena kidato cha kwanza upya! Mwanzoni taarifa zile zilinivuruga sana maana nilikuwa nishajuana na wana kibao, bebez tele na matukio kama yote shuleni.
Basi kama mjuavyo wana jamvi, tembo hashindwi na mkonga... mzazi ni mzazi tu! Mzee jambo lake likatiki akanihamisha shule, Hohehahe nikaamia Islamic school fulani hapahapa jijini Dar... na hapo ndo nilipoanza kuwahusudu hawa wanawake wa rangi nyeupe... walikuwa tele kama kunguni, na mpaka namaliza ile shule sikuwahi kuwa penzini na mwanamke mweusi.
Advance nikaenda shule ingine ya seminary hapahapa jijini Dar iko maeneo ya upanga... huko naona ndo nilienda kukubuhu na hizi mbususu nyeupe. Kwahiyo namshauri mleta mada asikate tamaa! Tembelea mazingira yao utabahatika.