Mlundikano wa michango makanisani itafanya watu warudi kuabudu mizimu ya kwao

Mlundikano wa michango makanisani itafanya watu warudi kuabudu mizimu ya kwao

Wakuu huu ni ubashiri tu, muutunze huu uzi.

Hatuna miaka mingi kabla hatujafika hapo.

Michango imekuwa mingi mno.

Inabadilishwa majina tu.

Mingi haipo hata kwenye maandiko.

Tunakoelekea itakuwa gharama sana kuwa msharika.

Itakuwa ni heri uende vichakani ukaililie mizimu ya kwenu.
Nilifundishwa sadaka yoyote inaleta majibu, na sadaka inatoka moyoni yaani amani ya moyo inaridhia kumtolea Mungu kwa kupenda sio kwa kulazimishwa, nimejifunza mengi pia sanaa
 
Wakuu huu ni ubashiri tu, muutunze huu uzi.

Hatuna miaka mingi kabla hatujafika hapo.

Michango imekuwa mingi mno.

Inabadilishwa majina tu.

Mingi haipo hata kwenye maandiko.

Tunakoelekea itakuwa gharama sana kuwa msharika.

Itakuwa ni heri uende vichakani ukaililie mizimu ya kwenu.
Unajua mizimu wewee?, dhahiri unatokea miongoni mwa makabila ya kishamba sana hapa Tanzania.

Watu wa Karne hii na ijayo hawatakuja kuabudu mizimu kamwe, hata wahadzabe wameanza kwenda makanisani na misikitini.
 
Toa zaka na sadaka tu ! Michango mingine yoyoyte ile usitoe, simple !!!!!
Wakat tunakua kulikua hakuna utitiri wa michango wala mapadri kutumia lugha kal kulazimisha waumin wachange yan ulikua unaenda church roho nyeupe unatoa sadako yako uliyoipanga wewe kimya kimya mana tuliambiwa sadaka ni siri LEO hii unapangiwa sadaka na hapo masimango kibao yan misa nzima padri analalamikia michango,mim nilitoka huko kitambo nikitaka kutoa sadaka natoa kwa yatima na wenye uhitaj
 
Mara bashasha ya papa, bashasha ya pasaka na krismas....Sasa papa tunamchangiaje huku!?!? Hovyo sana!

Halafu maparoko wana misuse sana hizo pesa, sema nini baadhi ya majimbo kuna utaratibu wa kufanyiwa auditing siku hizi...!

Kuna siku nilisali kkkt nikakutana na bashasha za sadaka nane. Mpk ya mfuko wa elimu

Kuna lile kanisa la chanzo Halisi....yule ndio amepanga macontena yake mbele watu wanapishana TU na bashasha kutumbukiza humo sijui hapo kumi na ngapi!

Ni ubatili balaa....

Kanisa linajenga ukumbi kwa michango ya waumini, ila nikienda kutaka fanya sherehe hapo lazima nilipe no discount!

Ubatili!
 
Wakat tunakua kulikua hakuna utitiri wa michango wala mapadri kutumia lugha kal kulazimisha waumin wachange yan ulikua unaenda church roho nyeupe unatoa sadako yako uliyoipanga wewe kimya kimya mana tuliambiwa sadaka ni siri LEO hii unapangiwa sadaka na hapo masimango kibao yan misa nzima padri analalamikia michango,mim nilitoka huko kitambo nikitaka kutoa sadaka natoa kwa yatima na wenye uhitaj
Mimi natoa sadaka na zaka tu,,,,nikihitaji kujitolea zaidi naenda kwa wasiojiweza ! Michango mingine sitoi kabisa,,,,
 
Inawezekana washirika ni maskini wanachanga elfu elfu zinaishia kwenye gharama za uendeshaji wa maisha ya mchungaji, nabii au mtume, askofu nk😎😎
Mmh apana haiwezekani sio kwa goba yetu
 
Ukitaka utajiri wa haraka hakikusha unakua m KKKT halafu jitahidi sana uingizwe kwenye kamari sorry kamati ya fedha/uchumi/maendeleo.
Hakikisha unasali Kariakoo/Msasani/Mbezi beach/ Tegeta/
Wazo/hata Kimara hutakosa pesa ndogo ndogo za kubadilisha mboga na beer mbili.
 
Nina dada yangu yupo kamati ya manunuzi kwenye usharika fulani wa KKKT, amenunua mpaka gari huku ni jobless tu
 
Back
Top Bottom