Mlundikano wa michango makanisani itafanya watu warudi kuabudu mizimu ya kwao

Mlundikano wa michango makanisani itafanya watu warudi kuabudu mizimu ya kwao

Ujinga wenu tu waumini wa kisasa. Mnarundikiwa mamichango haya na mnatoa ili kuwa washarika wazuri eti siku mkifa mje mzikwe vizuri kiimani. Kwani hata ukizikwa na halmashauri ya jiji au ukatupwa porini ukaliwa na wanyama huko kuendeleza food chain wewe marehemu inakusaidia au kukuathiri kivipi? Kama uko sawa na Mungu wako mbinguni si utaenda tu? Kuna mtu atakosa kwenda mbinguni kisa eti hakutoa mchango wa jengo la kanisa au hakuzikwa kikristo? Shwaini kabisa! 🚮
Aahaaaa
 
Toeni sadaka,toeni sadaka,toeni sadaka nannyi mtabarikiwa,Kila madhabahu huwa inadai sadaka za namna tofauti tofauti,hata madhabahu ya mizimu ina sadaka zake na hivyo ni lazima.
 
Toa zaka na sadaka tu ! Michango mingine yoyoyte ile usitoe, simple !!!!!
Soma hii usikariri tena;
Kumbukumbu la Torati 14:22-29
22 Usiache kutoa zaka ya fungu la kumi katika maongeo yote ya mbegu zako, yatokayo shamba mwaka baada ya mwaka.

23 Nawe utakula mbele za Bwana, Mungu wako, mahali atakapochagua apakalishe jina lake, zaka ya nafaka zako, na divai yako, na mafuta yako, na wazaliwa wa kwanza wa makundi yako ya ng'ombe na ya kondoo; ili upate kujifunza kumcha Bwana, Mungu wako, daima.

24 Na njia ikiwa ndefu mno nawe, usiweze kuzichukua kwa kuwa mahali ni mbali nawe mno atakapochagua Bwana, Mungu wako, apakalishe jina lake, hapo atakapokubarikia Bwana, Mungu wako;

25 ndipo uzibadili ziwe fedha, na kufunga zile fedha uende nazo mkononi mwako, hata mahali atakapochagua Bwana, Mungu wako;

26 na zile fedha zitumie kwa cho chote itakachotamani roho yako, ng'ombe, au kondoo, au divai, au kileo, au roho yako itakacho kwako cho chote; nawe utakula huko mbele za Bwana, Mungu wako; tena furahi, wewe na nyumba yako;

27 na Mlawi aliye ndani ya malango yako usimwache, kwani hana fungu wala urithi pamoja nawe.

28 Kila mwaka wa tatu, mwisho wake, toa fungu la kumi lote la maongeo yako ya mwaka huo, uliweke ndani ya malango yako;

29 na Mlawi kwa kuwa hana fungu wala urithi pamoja nawe, na mgeni, na yatima, na mjane aliyefiliwa na mumewe, walio ndani ya malango yako, na waje wale na kushiba; ili kwamba Bwana, Mungu wako, akubarikie katika kazi yote ya mkono wako uifanyayo.
 
Hata kwenye Mizimu pia sio bure kuna gharama za Mbuzi vinywaji kulisha wazee na posho kidogo pia
Tena kwa mizimu aseeh ukute familia yenu ilikuwa na makando kando utachinja mbuzi mpaka uone hapa Kuna kusaliti amri au uokoke
 
Soma hii usikariri tena;
Kumbukumbu la Torati 14:22-29
22 Usiache kutoa zaka ya fungu la kumi katika maongeo yote ya mbegu zako, yatokayo shamba mwaka baada ya mwaka.

23 Nawe utakula mbele za Bwana, Mungu wako, mahali atakapochagua apakalishe jina lake, zaka ya nafaka zako, na divai yako, na mafuta yako, na wazaliwa wa kwanza wa makundi yako ya ng'ombe na ya kondoo; ili upate kujifunza kumcha Bwana, Mungu wako, daima.

24 Na njia ikiwa ndefu mno nawe, usiweze kuzichukua kwa kuwa mahali ni mbali nawe mno atakapochagua Bwana, Mungu wako, apakalishe jina lake, hapo atakapokubarikia Bwana, Mungu wako;

25 ndipo uzibadili ziwe fedha, na kufunga zile fedha uende nazo mkononi mwako, hata mahali atakapochagua Bwana, Mungu wako;

26 na zile fedha zitumie kwa cho chote itakachotamani roho yako, ng'ombe, au kondoo, au divai, au kileo, au roho yako itakacho kwako cho chote; nawe utakula huko mbele za Bwana, Mungu wako; tena furahi, wewe na nyumba yako;

27 na Mlawi aliye ndani ya malango yako usimwache, kwani hana fungu wala urithi pamoja nawe.

28 Kila mwaka wa tatu, mwisho wake, toa fungu la kumi lote la maongeo yako ya mwaka huo, uliweke ndani ya malango yako;

29 na Mlawi kwa kuwa hana fungu wala urithi pamoja nawe, na mgeni, na yatima, na mjane aliyefiliwa na mumewe, walio ndani ya malango yako, na waje wale na kushiba; ili kwamba Bwana, Mungu wako, akubarikie katika kazi yote ya mkono wako uifanyayo.
Nieleweshe mkuu kwa summary nielewe
 
Wakuu huu ni ubashiri tu, muutunze huu uzi.

Hatuna miaka mingi kabla hatujafika hapo.

Michango imekuwa mingi mno.

Inabadilishwa majina tu.

Mingi haipo hata kwenye maandiko.

Tunakoelekea itakuwa gharama sana kuwa msharika.

Itakuwa ni heri uende vichakani ukaililie mizimu ya kwenu.
Tatizo lako wewe humjui Mungu. Wewe unatoa kwa wanadamu ndio maana unakwazika na utapokea laana badala ya baraka. Tumshukuru Mungu kwamba kuna makanisa mengi. Sasa kama unaona kanisani unakosali michango ni mingi si uhamie kanisa lingine? Lakini pia ujue kwamba kutoa sadaka ni ibada. Kwa hiyo ukikuta unakwazika maana yake hujafanya ibada yoyote. Biblia inasema tutor kwa moyo. Usipotoa kwa moyo unavuna laana. Sasa badala ya kushiriki kanisa unalokwenda kupokea laana hamia kanisa lingine mahali utakapomtolea Mungu kwa furaha.
Lingine hilo unalosema watu wataacha kanisa sio kweli. Bali makanisa yataendelea kuongezeka. Yale ya dini pengine yale ya kidini.
 
Wakuu huu ni ubashiri tu, muutunze huu uzi.

Hatuna miaka mingi kabla hatujafika hapo.

Michango imekuwa mingi mno.

Inabadilishwa majina tu.

Mingi haipo hata kwenye maandiko.

Tunakoelekea itakuwa gharama sana kuwa msharika.

Itakuwa ni heri uende vichakani ukaililie mizimu ya kwenu.
Acha wivu
 
Na bahati mbaya viongozi wa makanisa kazi yao ni kuhimiza na kukusanya sadaka na michango kwa waumini wao ila kusimama na wananchi kudai na kutetea haki hatuwaonekani. Wananchi wanatekwa, wanauliwa, kura zinaibwa, chaguzi zinachezewa, nchi inauzwa wao wako kimya na zaidi zaidi utasikia wakisifu watawala
 
Nikiwa Mkristo, hii hoja ni sahihi kabisa. Tumefanya kanisa kuwa sehemu ya kukusanyia sadaka. Hata RC siku hizi nasi tumepoteza mwelekeo. Unakaa umeandaa zako na hela ya sadaka mara unaona kama Padre anakuangalia wewe amekazana sadaka sadaka. Jamani, nnapokuja nimekuja na kile nilichoona nitakitoa bila kinyongo, tusikwazane, maana hiyo ni dhambi. Hata Yesu alisisitiza toa kiasi unachotoa na moyo wako ukaridhia!
 
Back
Top Bottom